Swali kwa Jaji Mkuu: Je, ni haki kwa kina Rostam Aziz kutozwa faini badala ya kifungo lakini kina Mbarikiwa kupewa kifungo badala ya faini?

Swali kwa Jaji Mkuu: Je, ni haki kwa kina Rostam Aziz kutozwa faini badala ya kifungo lakini kina Mbarikiwa kupewa kifungo badala ya faini?

Tofauti ya kesi hizo mbili ni kuwa Akramu hakushindana/kutunishia serikali misuli kama Mbarikiwa alivyo kuwa anafanya hivi karibuni kwenye mitandao. Yeye Mbarikiwa ni Mchungaji ila kaweka maandiko ya kuheshimu mamlaka kando. Kwa utaratibu huo ataanza kujifunza. Ajifunze kwa Kakobe na Muhingira!
Unaheshimu mamlaka ipi? Kwanini hakushtakiwa kwa kutoheshimu mamlaka?
 
Hili la kumfunga Mbarikiwa linaongeza mzozo zaidi badala ya kupunguza kero kwa watawala.Naona makelele yanapigwa zaidi baada ya hili tukio kutokea.Mwisho wa siku naona kuna kukata rufaa na serikali kumuachilia Mbarikiwa kwa mtindo huo🤔
 
View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Tarehe 29 Septemba 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya, Paul Ntumo, alimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Dickson Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.

Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinaipa mahakama mamlaka ya kutoa adhabu mojawapo kati ya tatu. Kuna:
  1. Ama adhabu ya kulipa faini, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha chini (minor offenses),
  2. Au adhabu ya kifungo, kwa makosa yenye ukubwa wa kati (intermediate offenses),
  3. Au adhabu zote mbili kwa pamoja, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses).
Kwa mujibu wa busara ya Mahakama ya Hakmu Mkazi wa Mbeya, kitendo cha kuendesha kanisa kabla ya kupata usajili ni "interdmediate offense" na hivyo kuamua kutoa adhabu ya kifungo kwa Mwakipesile.

Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,


View: https://youtu.be/JSVmJqUmbHg

Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe mahakama iliona kwamba Akram alifanya "minor offense." Hivyo Akram alitozwa faini, badala ya kifungo.


View: https://youtu.be/-FWpqOItZrI

Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Na tatizo liko hivi:

  1. Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji au shehe ni mahakama ya hovyo sana.
  2. Mahakama inayomheshimu mwarabu na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe.
  3. Mahakama inayotukuza watu wenye mamlaka ya kisasa na kutwatweza wanyonge inakuwa na watendaji ambao wana tatizo la ukamilifu wa kimaadili.
  4. Kwa ujumla, mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.

Hivyo, tunapenda kutoa mapendekezo yafuatayo kwa vigogo wa nchi hii, na hasa wale wenye mapenzi mema, na wanaojali kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo zile tunu kuu za taifa hili linaloitwa Tanzania:

1. Mheshimwa Jaji Mkuu achukue hatua za kulinda heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta uhiari wa kimamlaka (discretionary powers) walio nao mahakikmu na majaji katika hatua ya kutamka adhabu, kwa kuhakikisha sheria zote zinazotaja adhabu zinatoa vigezo vya kutofautisha kinaganaga kati ya aina zifuatazo za adhabu za kimahakama:

(a) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha ukomo wa chini (minor offenses) yanayostahili adhabu ya kulipa faini kama yakithibitishwa;​
(b) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha kati (intermediate offenses) yanayostahili adhabu ya kifungo kama yakithibitishwa; na​
(c) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses) yanayostahili adhabu zote mbili kwa pamoja kama yakithibitishwa.​
(d) Makosa yenye ukubwba wa kiwango cha ukomo wa juu kabisa (heinous offenses) yanayostahili adhabu ya kifo kama yakithibitishwa.​

2. Mheshimiwa Rais Samia atumie mamlaka yake kama Mkuu wa cnhi kufuta mara moha adhabu aliyopewa Mchungaji Mwakipesile ili kuzuia matope yanayoweza kumrukia mabegani mwake.

3. Rais Samia amwagize Waziri wa Mambo ya ndani, Mhandisi Hamad Masauni, kumpa Mchungaji Mwakipesile usajili aliouomba, maana, utafiti wetu unaonyesha kwamba, hatua zote zinazotakiwa kisheria tayari Mwakipesile amezifuata. Kanuni za utwala wa sheria na misingi ya Katiba ya nchi kuhusu uhuru wa kuabudu ifuatwe.

Tunawasilisha.

Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023


============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================

MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ​


View attachment 2766818

Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.

Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.

Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.

Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:

View attachment 2766815

View attachment 2766816

View attachment 2766817

Let's make a deal, scratch my back I will scratch yours, give me channel 10 I'll give you your young brother, fine.
 
Baada ya kifo cha mwanae alifuata sheria kupata haki yake?

Kilichotokea ni kumdhoofisha kwa kutumia mbinu ya INDIVIDUAL PROPHYLAXIS. Mbarikiwa ameeleza sana kilichotokea kwa kutumia lugha ya walei. Lakini wenye akili tukajua kinachoendelea. Kama huelewi kanuni hii hutaelewa. Lakini, kubwa ni kwamba, chini ya mbinu huu, raia wa kawaida kama Mbarikiwa hawezi kupambana na operations zinazoratibuwa na eagle's house.
 
Kilichotokea ni kumdhoofisha kwa kutumia mbinu ya INDIVIDUAL PROPHYLAXIS. Mbarikiwa ameeleza sana kilichotokea kwa kutumia lugha ya walei. Lakini wenye akili tukajua kinachoendelea. Kama huelewi kanuni hii hutaelewa. Lakini, kubwa ni kwamba, chini ya mbinu huu, raia wa kawaida kama Mbarikiwa hawezi kupambana na operations zinazoratibuwa na eagle's house.
Mama Amon kama hujaolewa naomba nafasi ndani ya moyo wako ili unifundishe hiyo INDIVIDUAL PROPHYLAXIS tukiwa wawili chumbani.
 
Back
Top Bottom