Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Mmmh🙄🙄🤔View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Tarehe 29 Septemba 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya, Paul Ntumo, alimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Dickson Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.
Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinaipa mahakama mamlaka ya kutoa adhabu mojawapo kati ya tatu. Kuna:
Kwa mujibu wa busara ya Mahakama ya Hakmu Mkazi wa Mbeya, kitendo cha kuendesha kanisa kabla ya kupata usajili ni "interdmediate offense" na hivyo kuamua kutoa adhabu ya kifungo kwa Mwakipesile.
- Ama adhabu ya kulipa faini, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha chini (minor offenses),
- Au adhabu ya kifungo, kwa makosa yenye ukubwa wa kati (intermediate offenses),
- Au adhabu zote mbili kwa pamoja, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses).
Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,
View: https://youtu.be/JSVmJqUmbHg
Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe mahakama iliona kwamba Akram alifanya "minor offense." Hivyo Akram alitozwa faini, badala ya kifungo.
View: https://youtu.be/-FWpqOItZrI
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Na tatizo liko hivi:
- Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji au shehe ni mahakama ya hovyo sana.
- Mahakama inayomheshimu mwarabu na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza kabwela sio mahakama kamwe.
- Mahakama inayotukuza watu wenye mamlaka ya kisasa na kutwatweza wanyonge inakuwa na watendaji ambao wana tatizo la ukamilifu wa kimaadili.
- Kwa ujumla, mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "good ends may justify any means, including evil means," haitakiwi nchini Tanzania.
Hivyo, tunapenda kutoa mapendekezo yafuatayo kwa vigogo wa nchi hii, na hasa wale wenye mapenzi mema, na wanaojali kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo zile tunu kuu za taifa hili linaloitwa Tanzania:
1. Mheshimwa Jaji Mkuu achukue hatua za kulinda heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta uhiari wa kimamlaka (discretionary powers) walio nao mahakikmu na majaji katika hatua ya kutamka adhabu, kwa kuhakikisha sheria zote zinazotaja adhabu zinatoa vigezo vya kutofautisha kinaganaga kati ya aina zifuatazo za adhabu za kimahakama:
(a) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha ukomo wa chini (minor offenses) yanayostahili adhabu ya kulipa faini kama yakithibitishwa;(b) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha kati (intermediate offenses) yanayostahili adhabu ya kifungo kama yakithibitishwa; na(c) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses) yanayostahili adhabu zote mbili kwa pamoja kama yakithibitishwa.(d) Makosa yenye ukubwba wa kiwango cha ukomo wa juu kabisa (heinous offenses) yanayostahili adhabu ya kifo kama yakithibitishwa.
2. Mheshimiwa Rais Samia atumie mamlaka yake kama Mkuu wa cnhi kufuta mara moha adhabu aliyopewa Mchungaji Mwakipesile ili kuzuia matope yanayoweza kumrukia mabegani mwake.
3. Rais Samia amwagize Waziri wa Mambo ya ndani, Mhandisi Hamad Masauni, kumpa Mchungaji Mwakipesile usajili aliouomba, maana, utafiti wetu unaonyesha kwamba, hatua zote zinazotakiwa kisheria tayari Mwakipesile amezifuata. Kanuni za utwala wa sheria na misingi ya Katiba ya nchi kuhusu uhuru wa kuabudu ifuatwe.
Tunawasilisha.
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================
MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ
View attachment 2766818
Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.
Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.
Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.
Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:
View attachment 2766815
View attachment 2766816
View attachment 2766817
Yaani huyu Akram Aziz alikutwa na makosa ya kuwa na silaha hizi zote akizitumia kwa ujangili kinyume cha sheria na ikathibitika hivyo pasipo shaka yoyote lakini hakimu akaona kosa hilo kuwa ni "minor offense" na hivyo kutozwa faini ya pesa tu?
Kama ni hivyo, basi ninakubaliana na wewe kuwa mahakimu/majaji wetu na mahakama zetu kwa ujumla wake zimeshanunuliwa na mfumo wa uovu dhidi ya haki na hivyo wao ndio wana dictate kesi iweje na hukumu iwe ya namna gani..!
====================================================
KKUHUSU MCH. MBARIKIWA DICKSON MWAKIPESILE NA HUKUMU YAKE.
Kiukweli Mch Mbarikiwa Mwakipesile ni binadamu kama tulivyo mimi na wewe na kila mmoja anayesoma. Ana mapungufu na madhaifu yake ya kibinadamu.
Ni kweli pia kuwa katika mfumo wake wa maisha ni mtu mwenye ujasiri wa ajabu kidogo na huutumia ujasiri huo kumtuhumu na kumshambulia yeyote kwa maneno awe mtu wa kawaida, kiongozi wa serikali au kisiasa, wachungaji wenzake nk nk ili mradi tu amhisi kuwa anakosea au amemkosea yeye mwenyewe binafsi..
Lakini kutumia udhaifu wake usiovunja sheria yoyote isipokuwa tu eti tu kwa kuwa hapatani na baadhi ya viongozi wa kisiasa na serikali wenye nguvu na mamlaka za kiserikali kumkomoa kwa kesi za uongo na kisha kumfunga gerezani wakidhani wanaondoa kero na kikwazo cha kuendelea desturi zao za uovu na uonevu, ni kosa kubwa na baya sana..
Inashangaza mno kuoina mahakama ikiwa ime - compromise na waovu hawa na kuacha sheria na adili..
Mkono wa Bwana uwe juu ya wahalifu hawa wote..