Wakati padri Mzungu anahukumiwa kifungo cha siku 1 baada ya kukutwa na meno ya tembo sijui kama ulikuwa ushazaliwa.
Tafuta pesa. Ndugu
u need to grow up.Kwahiyo wewe sasa unampangia hakimu namna ya kuhukumu?
The same as youYo
u need to grow up.
View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Tarehe 29 Septemba 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya, Paul Ntumo, alimhukumu kifungo cha miaka mitatu na siku 14 jela, Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Dickson Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.
Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinaipa mahakama mamlaka ya kutoa adhabu mojawapo kati ya tatu. Kuna:
Kwa mujibu wa busara ya Mahakama ya Hakmu Mkazi wa Mbeya, kitendo cha kuendesha kanisa kabla ya kupata usajili ni "interdmediate offense" na hivyo kuamua kutoa adhabu ya kifungo kwa Mwakipesile.
- Ama adhabu ya kulipa faini, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha chini (minor offenses),
- Au adhabu ya kifungo, kwa makosa yenye ukubwa wa kati (intermediate offenses),
- Au adhabu zote mbili kwa pamoja, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses).
Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,
View: https://youtu.be/JSVmJqUmbHg
Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe mahakama iliona kwamba Akram alifanya "minor offense." Hivyo Akram alitozwa faini, badala ya kifungo.
View: https://youtu.be/-FWpqOItZrI
Huku kutotabirika kwa maamuzi ya mahakama kunazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Na tatizo liko hivi:
Hivyo, tunapenda kutoa mapendekezo yafuatayo kwa vigogo wa nchi hii, na hasa wale wenye mapenzi mema, na wanaojali kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo, zile tunu kuu za taifa hili linaloitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
- Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji au shehe ni mahakama ya hovyo sana.
- Mahakama inayomheshimu mwarabu na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama.
- Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza makabwela sio mahakama kamwe.
- Mahakama inayotukuza watu wenye mamlaka ya kisasa na kutwatweza wanyonge inakuwa na watendaji ambao wana tatizo la ombwe la kimaadili.
- Kwa ujumla, mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "matokeo mazuri yanaweza kuhalalisha mbinu yoyote, hata kama ni mbinu haramu," haitakiwi katika Tanzania ya Nyerere.
1. Mheshimwa Jaji Mkuu achukue hatua za kulinda heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta uhiari wa kimamlaka (discretionary powers) walio nao mahakikmu na majaji katika hatua ya kutamka adhabu, kwa kuhakikisha sheria zote zinazotaja adhabu zinatoa vigezo vya kutofautisha kinaganaga kati ya aina zifuatazo za adhabu za kimahakama:
(a) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha ukomo wa chini (minor offenses) yanayostahili adhabu ya kulipa faini kama yakithibitishwa;(b) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha kati (intermediate offenses) yanayostahili adhabu ya kifungo kama yakithibitishwa; na(c) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses) yanayostahili adhabu zote mbili kwa pamoja kama yakithibitishwa.(d) Makosa yenye ukubwba wa kiwango cha ukomo wa juu kabisa (heinous offenses) yanayostahili adhabu ya kifo kama yakithibitishwa.
2. Mheshimiwa Rais Samia atumie mamlaka yake kama Mkuu wa cnhi kufuta mara moha adhabu aliyopewa Mchungaji Mwakipesile ili kuzuia matope yanayoweza kumrukia mabegani mwake.
3. Rais Samia amwagize Waziri wa Mambo ya ndani, Mhandisi Hamad Masauni, kumpa Mchungaji Mwakipesile usajili aliouomba, maana, utafiti wetu unaonyesha kwamba, hatua zote zinazotakiwa kisheria tayari Mwakipesile amezifuata. Kanuni za utwala wa sheria na misingi ya Katiba ya nchi kuhusu uhuru wa kuabudu ifuatwe.
Tunawasilisha.
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================
MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ
View attachment 2766818
Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.
Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.
Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.
Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:
View attachment 2766815
View attachment 2766816
View attachment 2766817
Kwahiyo wewe sasa unampangia hakimu namna ya kuhukumu?
Hii kesi ya Mdogo wake azizi ya Mwaka 2019 enzi za JPM nadhani kuna namna waliimaliza nje ya mahakama.
Eti mbarikiwa? Mbarikiwa wa nini? Huyo mtu ni mwehu na anatengeneza "cult" ya wehu. Naipongeza Serikali kwa hatua madhubuti waliochukua. Naye Kibwetere alianza hivihivi akawateka watu kwa kusingizia dini kisha akawachoma moto.
Tusije ilaumu Serikali baadaye kwa kuendeleza vidhehebu uchwara
Mama Amon umetisha sana. Hongera sana kwa hili bandiko lako.View attachment 2766809

Duniani mambo hayako hivyo.....huyo utaona anapanda na vyeo kwa ujasiri wake.
Anapiga hela za kutosha na utamwona akikwe mapipa hapa na pale kula bata ulaya na marekani.
Dunia hii mambo yanavyokwenda ni kunyume nyume.
Jinai haizeekei wala kufa. Haijalishi ka operate kwa miaka 3 bila kukamatwa lakini la msingi ni kwamba hana kibali. Na watoa kibali wamempima wameona hastahili kuwa registeredHahah!!! Kwaiy anayo yafanya Zumaridi kwa kuuza Binadamu ni sawa na anayo yafanya Mwamposa ni sawa wenyew hawatakiwi kuhukumiwa kwa sabab ya Makosa yao ni differ na ya wengine aisee...
Binafsi mm sioni Kosa la hiyo mbarikiwa kama swala ni kibali kwann hawakumfungia kanisa kuliko kumkamata na kumfunga yeye. Na ali-operate hilo Kanisa Miaka 3 je hapo serikali ilikua haijaona.
Ndugusheria na Katiba zipo kwa. Ajili ya kutenda haki kwann umhukum huyu Alfu mwingine usimhukum basi hakuna umhimu basi wa Kuwa na sheria kama hiyo sheria ipo kwa ajili ya watu malum lakin wengine haihukum Bora isiwepo.
Zumaridi asingetakiwa awe uraiani akina Mwamposa wanasababisha vifo vya watu lakin sheria hazichukuliw, lakin kosa tu kibali
mkuu think Twice
AWAMU ya Tano watu walisema Kuwa Magufuri alikua dictator ambaye alikua hataki akosolewe, akapita imekuja hii AWAMU hii Sasa ndo tumeshuhudia mambo mengi ya ajabu mno kama Taifa tunaenda Wrong direction, huwez funga uhuru wa watu wakati huo katiba inawaruhusu, Je! Hiyo katiba ipo kwa ajili ya masikini tu syo wanasiasa!! Na matajiri. Hivyo kwa sheria zipo kwa ajili ya masikini.
Zumaridi amepatikana na makosa ya Biashara za Binadamu Huku akichukua watoto wadogo akiwafanya mazombie!! Lakin mtu huyo baada ya mda mfupi kachiwa, Na wakina Mwamposa wanaendesha makongomano yanayo ua watu mbona hakuna sheria Inayo chukuliwa. Je! Huyo Mbarikiwa kosa lake ni lipi kudai haki yake.
Mh Sa100 haya ni ya mda kumbuka ww upo kwa ajili ya kulinda katiba pamoja na kuliongoza Taifa katka njia sahihi na siyo kuwafunika makombe wasiongee huyo siyo Uongozi Bora na siyo Democracy hiyo tunayo sema tunayo, ni Bora isiwepo tu tujue Kuwa no udikiteta hamna uchaguzi huru tunasema tuna demoracy gani hiyo??🚮🚮
Siyo kila mwehu anatibiwa hospitali. Huyo pimbi anastahili Mahabusu ndiyo atapata tiba yakeSasa Kama ni mwehu wamemfunga wa Nini. Unajua sheria inasemaje kuhusu mwehu kutiwa hatiani?.
Kesi yeyeto ni interest na biashara pia inategemea umeingia kwa mguu gani, ukiingia 18 zao hata kama una pesa lazima wakushikishe ukuta kwanza uwe na adabu
sasa alikuwa anafanya ujinga ili apigwe fain
Jinai haizeekei wala kufa. Haijalishi ka operate kwa miaka 3 bila kukamatwa lakini la msingi ni kwamba hana kibali. Na watoa kibali wamempima wameona hastahili kuwa registered
Siyo kila mwehu anatibiwa hospitali. Huyo pimbi anastahili Mahabusu ndiyo atapata tiba yake