Swali kwa waliooa tu: Mlipataje wanawake wa kuoa?

Swali kwa waliooa tu: Mlipataje wanawake wa kuoa?

Hili la kununiwa katikati ya vacation linanifanya nikutilie mashaka wewe mwenyewe na perfomance yako ya kitandani pamoja na namna ya kumhandel mwanamke muwapo falaghani!

Ni hayo tu, mambo mawili ya muhimu sana nadhani ndiyo yaliyokuangusha.

Mpo likizo badala ya kumshuhulikia kumfurahisha, wewe na misimu ya kikazi tu na kuchezea laptop na show yako hiyo ya tia maji-tia maji, kwa nini usinuniwe?

Umekiri mwenyewe kupenda zaidi kazi yako, kwa hiyo ulikalia lap top badala ya maongezi ya kimapenzi, jirekebishe.

Mi wa kwangu nilimpata kwa nongwa za vitisho.

Nilimtongoza akanitukana, nikaweka mazingira ya ushahidi nikamburuza serikali za mtaa.

Kufika Serikali za mtaa nikaisongesha Katani.

Katani nikaisongesha nahakamani.

Kabla sijaenda mahakamani nikatuma mamluki wangu kwake kumtisha namna atakavyodhalilika na hii kesi, maana anapambana na mtu wa Serikali.

Nikaona ametuma watu kumuombea msamaha na kuomba anilipe yaishe tusiende mahakamani.

Nikavimba kichwa nikakataa nikidai hiyo ni dharau kubwa sana mtu kutuma maombi ya msamaha kupitia kwa watu wengine, kwa nini asije mwenyewe kama anajutia kosa lake kweli?

Aliposikia hivyo akaanza kunitafuta mwenyewe ili tuyamalize.

Na aliponipata tuliyamaliza kweli, maana hadi leo tupo pamoja na wajukuu juu!

Kuna wanawake wengine mpaka uwe mbabe ndiyo anakuheshimu na kukupenda.
Sema unazingua kumwambia mwana asiipende kazi yake huo nao ni ufala mwingine kazi yake ndio mke wa kwanza.
 
Aise mimi nilisema nitatafuta mke wakati sina kazi ya kueleweka! Na kila mwanamke niliyempata kipindi kile nilikuwa namleta ghetoni kwangu kwa lengo la kuona mazingira tu! Wasichana wengi waliokuwa wanakuja gheto baada ya hapo hata simu zangu walikuwa hawapokei baada ya kuondoka! Baadaye alitokea mwanamke mmoja aliyekuja ghetoni na yeye aliyakubali yale mazingira na tukaanza mahusiano mpaka leo ndiye mke wangu miaka 6 sasa! Naweza kusema miongoni mwa wanawake kumi bora sio kwa sura kwa tabia nzuri za wife material yeye basi ni namba moja! Mpaka leo nina kazi nzuri hajawahi kubadilika! Wewe uwe na hela usiwe na hela utamfurahia tu! Kipindi chote cha uchumba sikuwahi kumpa zawadi yoyote na kipindi chote cha uchumba na mahusiano hatukuwahi kufanya mapenzi!! Ndivyo nilivyompata mke wangu
Usemalo ni kweli kabisa hawa wanawake kupata mke uwe broke, ukiwa na hela utapata wasaka fursa tuu.
So hapo maghetoni ulikuwa na godoro, ndoo mbili za maji na nini kingine mwanawane?
 
Kwa hiyo akamie kuongeza idadi ya single mamaz?
Sasa out of ten none amekubari proposal yake! Maana yake Ke wengi wanapenda kuwa single mother! Muoaji yupo tena mwenye kazi na kipato halari, na pipa anakwea bado tu mtu utakuwa na mashaka naye. Huyu jamaa kulea mtoto hatashindwa na ushauri wangu umezingatia asije Lea watoto kama wajukuu, astaafu ndio mtoto anagia darasa la Sita ( mtaala wa elimu umebadirika hakuna la Saba tena)

Ndio maana mwisho nimemuuliza mwenyewe labda show zake hawazielewi aka team kiba100 na hajui kukitumia vizuri.

Watu huku tuna ndoa zetu lakini bado tunasumbiliwa bara na visiwani, nashindwa kuelewa jamaa anakosea wapi.

Pia namshauri anaweza piga masters pale udsm au IFM container la first year likishuka atafute kama watatu hivi ndani yake atapata tu mtu.
 
Hbr wana JF,

Mwaka jana nilipata binti mmoja ambae tulifahamiana kwa muda kidogo tukaanza mahusiano. Nilimpenda sana, nikajitahidi kumtimizia kila analohitaji. Nilijifunza kwenye mahusiano yangu ya awali, nikasema huyu nifanye tofauti sasa na mimi niwe na familia. Mwanzo mapenzi yalikua motomoto, tukaanza kupanga mipango ya ndoa kabisa huu mwaka tuwe mume na mke.

Baada ya miezi kadhaa, akaanza kubadilika. Nakumbuka alianza kununa tukiwa vacation Zanzibar. Akawa kama ana moods hivi, ukimuuliza kuna changamoto gani hasemi. Nikaona mambo ya kike labda nitulie. Basi kuanzia hapo akawa kama anani dharau na hanijali tena kama mwanzo. Nilikua naumia ila nikawa navumilia. Lakini kwa tabia zile alizoanzisha ikanilazimisha baadhi ya mambo tulipanga kufanya - kama kwenda kujitambulisha kwao tusitishe kwanza maana sikua namuelewa, anasahau mpaka tarehe muhimu kwenye mahusiano yetu kitu ambacho sio cha kawaida. Baada ya muda nikaenda nje ya nchi kikazi, katika nchi ambayo tulikua tunapishana masaa na hapo ndio mapicha picha yakazidi akawa hapokei simu kabisa akidai yuko busy etc. Kwa muda wote niliokua nje ya nchi kama miezi miwili hatukuwahi kuongea kwenye simu, kila nikijaribu kumtafuta anasema yuko busy atanicheki lakini hafanyi hivyo. Basi nikaanza kufanya maamuzi magumu, nikaacha kumpa monthly allowance na kumnunulia zawadi kama nilivyokua nafanya mwanzo. Nilivyorudi nchini, bado nikamtafuta kujua tatizo ni nini na nakumbuka pamoja na tofauti tulizokua nazo bado nilitoka ulaya na zawadi kadhaa nimemchukulia nikampa. Kikao hakikuenda sawa, binti akaniambia hana feelings na mimi na nikitaka kuwasiliana nae lazima nifanye appointment au nitafute mwanamke mwingine wa kua nae. Aisee, kikao kiliishia hapo. To cut the story short, mahusiano yaliisha pia.

Hii ni case moja tu kati ya nyingi ambazo nimeshakumbana nazo. Katika miaka 10 iliyopita nishakua kwenye mahusiano mengi sana na yamekwama kwa sababu tofauti tofauti, ingawa hii ya juzi iliniuma maana nilijitahidi kufanya kila kitu inavyotakiwa na mhusika mwenyewe pia nilijua anajitambua maana at 31 ni mtu mzima sio mtoto mdogo ni mwanamke aliepitia mengi. Mwaka umeanza nimekata tamaa kama naweza kweli na mimi siku moja kupata mke, nikaanzisha familia na kua na watoto. Kila kitu ninacho - kazi nzuri, kipato kizuri yani ni mke tu ndio imekua changamoto. Kuna wakati najilaumu labda ningekua nakunywa pombe & mtu wa starehe huenda ingekua rahisi kwangu maana haya maisha ya kua busy na kazi muda wote nayo ni changamoto sikutani na watu ila ndio nafanyaje sasa na pesa naitaka pia.

Naomba ushauri wadau, nifanyeje?!


NB:
Niliwahi kuandika uzi humu wa kutafuta : A wife is needed
Oga usitumie akili yako pekee kutafuta mke mshirikishe mungu mimi nilihisi ukiwa na pesa au tajiri kama mimi wanawake watakupenda kumbe ndivyo sivyo aisee nimeamua kumwangukia mungu
 
Kwahiyo wewe 31 ndio unaona umri umeenda uoe!? Aiseeh
Alafu wewe wanawake hawapendi mambo ya kuwafanyia kila wanachotaka au wanachosema, wanakuona sio mascular enough
Ila nimegundua kuna namna hauupigi mwingi
Kuna ushauri wa member Joanah, hebu uzingatie

Mleta mada anafikisha miaka 37 mwaka huu
 
Sasa out of ten none amekubari proposal yake! Maana yake Ke wengi wanapenda kuwa single mother! Muoaji yupo tena mwenye kazi na kipato halari, na pipa anakwea bado tu mtu utakuwa na mashaka naye. Huyu jamaa kulea mtoto hatashindwa na ushauri wangu umezingatia asije Lea watoto kama wajukuu, astaafu ndio mtoto anagia darasa la Sita ( mtaala wa elimu umebadirika hakuna la Saba tena)

Ndio maana mwisho nimemuuliza mwenyewe labda show zake hawazielewi aka team kiba100 na hajui kukitumia vizuri.

Watu huku tuna ndoa zetu lakini bado tunasumbiliwa bara na visiwani, nashindwa kuelewa jamaa anakosea wapi.

Pia namshauri anaweza piga masters pale udsm au IFM container la first year likishuka atafute kama watatu hivi ndani yake atapata tu mtu.

KWa hiyo mkuu mwanamke akimkataa mwanaume maana yake anataka kuwa single mama sio?

Kukwea pipa ndo umeona moja ya kigezo kikubwa cha mwanaume mwenye malengo,upendo wa kweli ee?yani aina hii ya mwanaume sio ya kuikataa?
 
Usemalo ni kweli kabisa hawa wanawake kupata mke uwe broke, ukiwa na hela utapata wasaka fursa tuu.
So hapo maghetoni ulikuwa na godoro, ndoo mbili za maji na nini kingine mwanawane?
Nilikuwa na kitanda, godoro, na vyombo vya kupikia na gas! Kukaa tunakaa kitandani! Na tulianza hivyo hivyo mpaka sasa tulikofikia hakuna mwanamke anaweza kunikataa kwa maisha haya!
 
Back
Top Bottom