Swali kwa Wasioamini Mungu (Atheists) juu ya udhalimu wafanyao Watu kwa watu wengine

Swali kwa Wasioamini Mungu (Atheists) juu ya udhalimu wafanyao Watu kwa watu wengine

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
29,126
Reaction score
29,352
Mjadala wa maadili hasa juu ya wema na uovu ni mjadala mkubwa na mzito sana kwa Wakana Mungu(Atheists) na unawasumbua sana, sijajua hawa tulio nao humu JF ila kwa wale wakubwa hasa kina Richard Dawkins na mfano wao, ndiyo maana leo hii nimekuja na hili la uovu na wema ili tupate kuwasikia wanalihukumu vipi hili.

Wakana Mungu mnatuambiaje hatima au mnahukumu vipi juu ya Mauaji ya Adolf Hitler kwa Wayahudi wale? Kwamba je alikuwa sawa au siyo sawa, na kama si sawa ni ipi stahiki yake, je ni kuwa kafa na jambo limeishia pale au inakuwaje?

Lakini mnasemaje juu ya mafisadi na wanao wadhulumu watu na kuendelea kutamba kwa mali zao au mfano wake, kwamba wakifa ndiyo iwe basi tu?

Shukrani.
 
Waenga wanasema adui yako muombee njaa adui yako mmalize.awakuwa wajinga
 
Kiranga na Napoleone mje huku mtie neno.
Kwani kusema hili jambo ni baya na hili ni zuri ni lazima uamini Mungu?

Mbona sheria walizojiwekea watu tu katika secular settings zinahukumu wauaji bila kuhitaji msahafu wa Mungu?

Walioshiriki mauaji ya Wayahudi Ujerumani walihukumiwa na mahakama ya Nuremberg wakapatikana na hatia.

Soma historia ya kesi maarufu za wafuasi wa Nazi, za "The Nuremberg Trials". Soma historia ya Rudolf Hess.

Mahakama ya Nuremberg haikuwa ya kidini.

Wanaouliza maswali wamesoma historia?
 
Hitler, Stalin, Iddi Amini, Mobutu na wengine wengi ambao walifanya ukatili wa kutisha na hawakuukabili mkono wa sheria ndio kusema hatima yao iliishia pale walipokufa tu?!
Kwani kusema hili jambo ni baya na hili ni zuri ni lazima uamini Mungu?

Mbona sheria walizojiwekea watu tu katika secular settings zinahukumu wauaji bila kuhitaji msahafu wa Mungu?

Walioshiriki mauaji ya Wayahudi Ujerumani walihukumiwa na mahakama ya Nuremberg wakapatikana na hatia.

Mahakama ya nuremberg haikuwa ya kidini.

Hapa unataka kujenga hoja gani?

Kwamba lazima kuna Mungu na hukumu baada ya kifo kwa sababu watu wakatili hawawezi kufanya ukatili wao halafu mwisho wao ukawa kifo tu wasilipie ukatili wao?

Ukisema hivyo, utakuwa sawa na mtu aliyetembea kilomita mia, akagundua kwamba kapoteza hela yake noti ya shilingi 10,000 sehemu fulani katika safari yake. Halafu hapo alipo ndiyo sehemu pekee yenye taa, hivyo, anaamini lazima noti yake imepotelea hapo, kwa sababu hapo ndipo sehemu pekee yenye taa!

Logical non sequitur.
 
Unadhibitisha vipi kuwa mungu yupo?? tuanzie hapa kwanza
 
Asilimia kubwa ya binadamu wakiamini na wakiwa na uhakika hakuna hukumu baada ya kifo, kwamba zaidi ya hizi hukumu za duniani hakuna kitakachoendelea dunia inaweza kuwa uwanja wa fujo na mahali hatari sana.
Ni heri watu waendelee kuamini kuna hukumu baada ya kifo.

Hilo linawezekana kuwa kweli, ingawa nalo linajadilika tofauti.

Lakini hiyo ni habari tofauti, haithibitishi kwamba Mungu yupo.

Unachoonekana kusema hapo ni kwamba, imani ya kuwepo Mungu ni muhimu hata kama Mungu hayupo, kwa sababu watu wakijua Mungu hayupo na hakuna hukumu ya mabaya baada ya kifo, watafanya maasi sana.

That's a different argument.

Na hata hii argument nayo ina mapungufu.

Mimi najua Mungu hayupo, na kwa sababu najua Mungu hayupo, mara nyingi watu wanapoomba msaada nakuwa wa kwanza kusaidia. Kwa sababu najua Mungu hayupo, hawezi kumsaidia. Watu wanaamini uwepo wa Mungu wengi wao wakiombwa msaada huishia kusema "Mungu atakusaidia". Wanamuachia Mungu kazi ya kusaidia. Mtu anakosa msaada.

Kwa hivyo, imani ya kuwepo kwa Mungu mara nyingine inakwamisha mema kufanyika.

Pia, naweza kukuuliza, mbona leo watu wengi wanasema wanaamini kuna Mungu na hukumu na bado wanafanya maasi mengi sana tu?

Na zaidi, kuna watu wengi sana kama baadhi ya Buddhists ambao hawaamini Mungu yupo, wao wanaamini katika "karma" tu, kwamba, ukifanya mambo mazuri, mazuri yatakurudia, na ukifanya mambo mabaya, mabaya yatakurudia. Na hawa jamii zao zinaenda vizuri tu bila kuhitaji uwepo wa Mungu? Tena wengine wanaishi vizuri kuliko jamamii zinazoamini uwepo wa Mungu.
 
Kwaiyo ndugu jurjan unataka wenzio wakaungue ndo ufurahi naona watu mtaumia sana siku ya ukumu Mungu akiwasamehee.wa kina nduli na osama.
 
Hitler, Stalin, Iddi Amini, Mobutu na wengine wengi ambao walifanya ukatili wa kutisha na hawakuukabili mkono wa sheria ndio kusema hatima yao iliishia pale walipokufa tu?!
Kaka wewe umenielewa vizuri sana.
 
Kwani kusema hili jambo ni baya na hili ni zuri ni lazima uamini Mungu?

Mbona sheria walizojiwekea watu tu katika secular settings zinahukumu wauaji bila kuhitaji msahafu wa Mungu?

Walioshiriki mauaji ya Wayahudi Ujerumani walihukumiwa na mahakama ya Nuremberg wakapatikana na hatia.

Soma historia ya kesi maarufu za wafuasi wa Nazi, za "The Nuremberg Trials". Soma historia ya Rudolf Hess.

Mahakama ya nuremberg haikuwa ya kidini.

Wanaouliza maswali wamesoma historia?
Hujaelewa nilichokiandika. Nawazungumzia Wakana Mungu wanasemaje juu ya hilo ?
 
Survive for fitness hata Simba anaingaika kila siku huku na kule ili apate kuwa mfalme wa nyika ila ukileta vurugu anakubutuwa
Iko hivi hapa duniani lazima watu wababe wanyonge wakatili wapole wachawi wema wanafki waoga wajasiri wawepo ili kuweza kubalance maisha hao wababe wezi wenye kufldhulumu ndiio wajanja habari za duniani zinaisha hapa hapa duniani
 
Nimecheka sana we jamaa sio aisee,, hiyo avi + id + ulichocoment yaani,,😂😂
 
Post no #10 Kiranga kaeleza vizuri mno ni swala la kutafakari tu mkuu,,
Nataka nikuonyeshe ya kuwa alichokiandika ni UONGO na hawezi kuthibitisha. Kisha utanionyesha ukweli wa alichokiandika hapo.
Unachoonekana kusema hapo ni kwamba, imani ya kuwepo Mungu ni muhimu hata kama Mungu hayupo, kwa sababu watu wakijua Mungu hayupo na hakuna hukumu ya mabaya baada ya kifo, watafanya maasi sana.
Watu wanajua Mungu yupo na wanafanya maasi, hii ni sababu ya uhuru aliotupa,na wewe unaamini ya kuwa Mungu hayupo /na ushahidi huna/ unafanya maasi.
Mimi najua Mungu hayupo, na kwa sababu najua Mungu hayupo, mara nyingi watu wanapoomba msaada nakuwa wa kwanza kusaidia.
Unaposema haya ni maelezo mazuri ila natakiwa kufikiria, ukitakiwa umuukize maejuaje ya kuwa Mungu hayupo na akuthibitishie kisha asema yaliyofata. Kadhalika akwambie ingekuwaje hii dunia pasi na aliyeiumba mwenye maarifa, msanifu, mjuzi wa kila kitu na mwenye malengo juu ya kuiumba hii dunia.

Lakini katika suala la msaada hili ni hiari na msaa umegawanyika sehemu mbili, ule ambao uko ndani ya uwezo wa mwanadamu na ule ambao uko nje ya uwezo wa mwanadamu, hapa ulitakiwa umuulize vipi kuhusu yale ambayo huwezi kumsaidia kama vile kumzuia asife au mfano wake, yaani bila shaka anaongelea yale ambayo yako ndaniya uwezo, na kufikiri kwa namna hii ni kufikiri kitoto.

Hapa tunahitimisha ya kuwa mpaka yeye anaamua kumsaidia mtu, ni Mola ametaka iwe hivyo nidyo maana imekuwa.
Watu wanaamini uwepo wa Mungu wengi wao wakiombwa msaada huishia kusema "Mungu atakusaidia".
Hii kauli si ya kweli,na nyinyi mnaiita "Strawman Argument", yaani una potosha ukweli kwa kuweka jambo nusu au lisilokuwepo. wanaosema kauli hii hugawanyika na huwa na sababu, wapo hutoa msaada kwanza kulingana na uwezo hukur wakitarajia malipo toka kwa Mola, huku kilichobakia Mola atamsaidia, kadhalika husema hivyo kwa yale ambayo yako nje ya yule alitakwa msaada.

Naendelea....
 
Post no #10 Kiranga kaeleza vizuri mno ni swala la kutafakari tu mkuu,,
Wanamuachia

Wanamuachia Mungu kazi ya kusaidia. Mtu anakosa msaada.
Hapa mpaka nikajiuliza ameeleza nini hapa mpaka unasema ametoa maelezo mazuri ?

Hili,liko wazi na watu hutoa msaada kwa kadiri ya uwezo na kwa yale ambayo yako nje ya uwezo wao.
Kwa hivyo, imani ya kuwepo kwa Mungu mara nyingine inakwamisha mema kufanyika.
Hii si kweli sababu imani hiyo huamrisha watu wafanye mema, na huonyesha ubora wa watu kufanua mema, kwahiyo ukiona watu wanafanya maovu ujue hawaifanyii kazi imani hiyo. Hii nayo ni aina ya upotoshaji.
Pia, naweza kukuuliza, mbona leo watu wengi wanasema wanaamini kuna Mungu na hukumu na bado wanafanya maasi mengi sana tu?
Hili swali rahisi sana, sababu watu hao wamepewa uhuru wa kuchagua kufanya mema au maovu. Ndiyo maana utakuta mtu anaamini hilo na anaiba, anazini na mfano wake.
Na zaidi, kuna watu wengi sana kama baadhi ya Buddhists ambao hawaamini Mungu yupo, wao wanaamini katika "karma" tu,
Sasa kwa wale ambao mkono wa sheria ulikuwa mfupi kwao na haukuwafikia kifo ndiyo "karma" kwao ? Na wale waliodhulumiwa na wao malipo yao ni nini na faraja yao huipata wapi ? Hitimisho la hapa ni kuwa Ubudha ukijengeka katika msingi wa ujinga na matamanio na si elimu na ithibati.
kwamba, ukifanya mambo mazuri, mazuri yatakurudia, na ukifanya mambo mabaya, mabaya yatakurudia.
Swali la msingi ni je ubaya unaupimaje na uzuri unaupimaje...? Maana wapo wanao kufa kabla ya kuyadiriki mazuri yao na mabaya yao kwa mujibu wa hiyo Karma.
Na hawa jqmii zao zinaenda vizuri tu bila kuhitqji uwepo wa Mungu? Tena wengine wanaishi vizuri kuliko jqmamii zinazoamini uwepo wa Mungu
Uzuri wa maisha unaupimaje ?

Lakini vyote hivi vinafanyika kwa kukata yeuw muumba ndiyo maana vinakuwa hivi vilivyo.

Kazi yangu nimemaliza, sasa nakuuliza swali, naomba unionyeshe uzuri wa maelezo ya mdau na ukweli wake uko wapi ?
 
Back
Top Bottom