Swali kwa Wasioamini Mungu (Atheists) juu ya udhalimu wafanyao Watu kwa watu wengine

Swali kwa Wasioamini Mungu (Atheists) juu ya udhalimu wafanyao Watu kwa watu wengine

weka uthibitisho
Naanzia hapa, kwanba Ng'ombe haliwi ?
Nyani gani? we umejuaje?
Sababu Nyani haishi kama Mbwa.
Unaweza kuniambia ni mungu gani ambaye hao nyani wanamjua?
Mungu ambaye ameumba ulimwengu na kuwawekea nidhamu ya kuishi viumbe wake.
Kwanza kwanini swali lako lijikite kwenye "nani"?
Swali rahisi sana. Natumia tamko "Nani" sababu linahusiha mwenye maarifa, mjuzi, mwenye kujua,mwenye nguvu.
ni kwa mtazamo wa kiislamu bila shaka.
Huo ndiyo usahihi, unachotakiwa wewe ni kuonyesha kwamba haya si sahihi na uweke ukweli wako hapa.
wanyama hawana commonsense halafu nataka uniambie ni aina gani ya mungu ambaye anajulikana na wanyama
Hili nimeshalijibu tayari.
wanaishi kwasababu mazingira wanayoishi yana support uhai. Wako wapi dragons na dinosaurs?
Hayo mazingira nani ameyaweka ? Yamejiweka au yametokea from nothing ?

Hakuna mwenye uthibitisho ya kuwa Dragons au Dinosaurs walikuwepo au kupata kuishi zaidi ya dhana na udanganyifu.
Kwa ukristo kila mtu ataenda mbinguni ikiwa tu atabatizwa, kwa maana hiyo utakubali kwamba wote walio kinyume na ukristo hawataenda mbinguni kwasababu mafundisho kutoka ukristo yamesema hivyo
Lipime hili kwa akili yako kisha uhakiki maandiko ya Wakristo utajua ni kweli au stori ?

Dini ya kweli haipingani na akili ikiyo salama kadhalika uhalisia wa mambo. Hii ndiyo sifa anuai ya Uislamu.

Swali la kwanza ili Wakristo wawe wa kweli, itabidi tuhakiki maandiko yao na watuambie Ukristo umeletwa na nani na ilikuwaje ukawa hivi ulivyo ?
ni kwa mujibu wa mtazamo wa dini ya kiislamu huwezi kutumia madai hayo kama facts katika ulimwengu wote na wakati hakuna observable evidence to support such claims.
Kabla hujajibu hoja uwe unaisoma na kuitafakkari kisha uone inajibika au haijibiki.

Unakubali kwamba ukizaliwa una kuwa huna kitu katika maarifa, na ukikiri ya kuwa mimi nimekuwa muislamu sababu wazazi wangu ni waislamu, lakini kwangu mimi halikuishia hapa bali hoja na yale yakiyomo katika Qur'aan na Hadithi yamenifanya niwe imara zaidi.

Ithibati hili iko wazi kabisa, tafuta mtu ambaye yupo cream hana uchafu katika akili yake, kisha mpe habari za kuwa hii dunia imeumbwa na aliyeumba ni mkamilifu wala hana mshirika, akikataa njoo utoe ushuhuda hapa.
Hata kujibu swali kwa mtindo wa swali nayo ni itifaki
Itakuwa hujui maana ya tamko itifaki.Ngoja nikupe faida, tamko "itifaki" ni tamko lenye asili ya kiaribu lenye maana "makubaliano" baina ya pande mbili. Swali, itifaki ipi umeizingatia hapa.

Kama huo uliouliza
Siyo kweli, sababu ulicho kiuliza ni kinyume na ulichojibu, na hakitoi jibi la moja kwa moja. Sharti, la swali kuwa ni jibu la swali,halitegemei maelezo ya ziada toka kwa muuliza swali, yaani muulizaji akiulizwa swali anajua hili ni jibu.
Ungejibu halafu tungeona kama halitoi majibu ya swali lako
Maelezo yako yalithibitisha ya kuwa huna swali wala maelezo yenye kujibi swali langu.
 
Kwa uelewa wangu naona Mtoa Mada anaonesha kama "ATHEISM" ni kama imani fulani ambayo ina mafundisho yake maalum yaani kuna doctrines na maandiko kwaajili ya atheists wote.

ATHEISM kwa uelewa wangu ni logical knowledge na sio belief.. Ni kitendo cha kutokukubaliana na uwepo wa any "deity"

Kitendo cha kujua kama hakuna uwepo wa chochote chenye uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote na sifa zote za kuupa Uungu chochote kile katika ulimwengu pasipo kuwa na uthibitisho wa kimantiki.

Kuna mahala katika posts zake huko juu ana demands mafundisho ya ATHEIST ambayo yana elezea hatima ya watu "waliofanya uovu" hapa duniani. Atheism haina mafundisho ila ina arguments tu ambazo zinahitaji uthibitisho wa kimantiki.

Mwisho kabisa Kwangu mimi naona sula la uovu kwanza ni relative matter, inategemea na perceptions ya muhusika. Kuna jambo kwako ni uovu ila kwa mwingine sio uovu na ni jambo la kawaida kabisa. Hivyo kuhukumu huu ni uovu na huu sio uovu ni sula ambalo linahitaji utashi wa muhusika.
 
Acha nicheke tu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hizi dini bana, na ka swali kafupi tu mkuu vp binadamu alie lelewa na mnyama kwanini awe na tabia zote za mnyama sio za binadamu
Ika si mnyama. Vipi mbwa alie lelewa na mwanadamu huwa na tabia binadamu ? Au humfanya asiwe na tabia za mbwa...?
 
Swali la muhimu kabisa ni kwanini karuhusu hayo majitu makatili kufanya huo ukatili na yeye amekaa kimya tu bila kusema au kufanya chochote.
 
Mkuu ukooo juu nimeona hutaki kujibiwa swali kwa swali me nimekuuliza unanipa swali baada ya jibu
Sijakataa kujibiwa swali kwa swali, kama ukisoma kwa umakini, nilimuuliza ni wakati gani swali hujibu swali. Maana yake swali hujibiwa kwa swali kwa masharti, na sharti moja wapo nimekidhi ndiyo maana nikakupa jibu kwa swali kwa kinyume cha swali lako, likawa swali kimejibu swali.
Sema sio mbaya sawa binadamu ni mnyama asaa kwanini akilelewa na nyani mfano,
Binadamu si mnyama, bali binadamu ni binadamu.
ana iga tabia zote za nyani mpaka mawasiliano yao ila hawezi ongea(kama ni kanuni yake amewekewa na muumba kwanini asiweze ongea).
Ukimtia katika mazingira hayo lazima arudi kwenye asili yake ya kuongea na anaongea. Ila muweke mbwa na tunaishi, vipi ushawahi kuona mbwa akiongea ?
Ila icho kitu ni tofauti kwa nyani akilelewa na binadamu hawezi acha asili yake(hao wote ni wanyama kwa maelezo yako)
Na mwanadamu hawezi acha asili yake, lazima atafakari kama wengine ika tofauti ni mazingira tu.
tuseme tu ukweli kua dini tunarithi kutoka kwa wazazi ilo la kusema mtu akizaliwa anakua anajua kanuni zote uoo ni uongo
Nani amesema haya ? Nilicho sema anakuwa na hali ya kupokea na kuamini juu ya uumbaji.
mkuu binadamu anazaliwa ubongo ukiwa hauna kumbukumbu wala taarifa yoyote vyote anapata kulingana na vitu vinavyo mzunguka(reincarnation hapa labda inaweza nikosoa).
Siyo kwamba ubongo hauna kumbukumbu, bali usahihi ni kuwa anazaliwa hajui chochote, yaani kama karatasi nyeupe.
 
Swali la muhimu kabisa ni kwanini karuhusu hayo majitu makatili kufanya huo ukatili na yeye amekaa kimya tu bila kusema au kufanya chochote.
Ndiyo maana kuna KIFO.
 
Hua napenda kutumia dhana ya "empath" kuswitch upande wa mwingine (vipi kama ndio mimi nafanyiwa hili jambo)

Hii ni moja wapo ya njia bora na nzuri zaidi inayoweza kufanya uelewe hisia za mwingine dhidi ya jambo ambalo liko mbele yake

Mfano: nimeibiwa chakula kilichokuwa mezani na bahati nzuri nimefanikisha kumkamata mwizi, akaja jirani yangu ambaye ni mtu wa dini akaniambia nimkate mkono kwasababu dini yake ndivyo inavyosema kwa wezi.
Umepotosha, uislam hausemi mwizi akatwe mkopo bali akiiba akalishwe chini na kuambiwa wizi mbaya na kupewa mawaidha ya kutosha akirudia tena ndio akatwe mkono...
Kabla ya yote nitachukua uhusika wa huyo mwizi na kuanza kufikiri, je ningekuwa mimi ningejiskiaje kukatwa mkono? Bila shaka nitajiskia vibaya na nitaumia sana kupoteza kiuongo changu kwasababu kama nilikua kamili viungo vyote lakini sikuweza kufanya kazi itakayoniwezesha kunilisha mpaka nikaamua kuiba je vipi kama mkono mmoja ukatwe nitaishije??

"Huruma" ni matokeo ya feelsings zinazokuja baada ya "empathy" hapo nitakuwa nimeweza kujua namna ambavyo mwizi atajisikia
Umeandika kimaskhara sana yani...Hakuna mtenda kosa ambae haFeel vibaya akitendewa vibaya Duniani inamaana ukifikiri mtendaji atajisikiaje Dunia ingekuwa na uovu mkubwa minajua nikikuchinja mkono wako utafikiria mimi nitajiakiaje ukinikata mkono pia So hutonikana hii inamaana
*nitaiba
*nitauwa watu
*nita baka
*nitalawiti
*nitafanya kilakitu kwasababu najua sitatendewa ubaya kwasababu nitaofanyia ubaya watawaza feeling zangu wataona nitajisikia vibaya nitaachw

Ulichoandika ni theory
Mfano wa pili: Kuna siku moja nilikuwa kariakoo nikachomolewa walet na kibaka ambayo ndani kulikuwa na 30k. Wakati nageuka nilimuona mwizi ameshika walet yangu anakimbia, nikaanza kumfukuza kimyakimya nilipomkamata nikaichukua walet yangu baada ya kuhakikisha pesa ipo vile vile nikamuacha mi nikasepa zangu

Sasa nilipomsimulia mshkaji wangu kilicho nitokea akaniambia kwanini ulikuwa unamkimbiza wakati ungepiga kelele za kuita mwizi asingefika mbali?

Nikamuambia hilo wazo lilinijia ila sikuona kama ni wazo bora..akauliza kwanini? Nikamjibu unahakika ukipiga kelele watu wanakusaidia kukuchukulia mali yako kutoka kwa mwizi au wanachukua sheria mkononi kwa kumpiga mwizi?

Nikamwambua, vipi kama ningepiga kelele halafu raia wajitokeze wampige hadi kufa?

Unafikiri hapo mimi nitajiskiaje? nitatafsiri kwamba ni raia wameua hivyo mimi sina hatia? Hapana hapo ni mimi ndio ningekuwa muuaji na ningeweza kujiwekea rekodi mbaya katika maisha yangu ya kusababisha mtu kufa kwa pesa ndogo tu 30k.

Kiukweli hilo lingenichukua miaka mingi sana kuja kusahau pengine kunisababishia msongo wa mawazo kwa kuniona mwenye hatia ya kuua mtu

Back to your post

Kama ulikuwa ukidhani huruma au kujua jambo baya na lipi zuri kunahitaji kumuamini mungu utakua unakosea

Wanyama wana experience emotions, wana feel love, wanahisi huzuni na tena bila hata kujua nini maana ya mungu

Utanisikitisha sana leo hii kuonekana unahitaji mungu ili uweze kujua baya na zuri kiasi cha kuonesha umezidiwa hadi na wanyama ambao wanaweza kufanya hivyo pasipo mungu


Mwisho bado mujajibu alichouliza mtoa mada

Je aliyeuwa watu 1000 na hakuhukumiwa na mkono wa sheria kafa tu natural je kwake ndio ishaisha??
 
Ndiyo maana kuna KIFO.
Jamaa hachana na huu mjadala wa kipuuzi swali ulilouliza hakuna anayejibu wanazalisha mada nyengine tu.

Hachana na mjadala wa kipuuzi kama huu.
 
Roho haiendi mbinguni au motoni (pure imagination ) inaenda kuanzisha maisha katika umbo jingine . Ukiwa unaishi jitahidi kucheza vizuri katika maisha . Kauli ya kusema namuachia Mungu ni kukata tamaa .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Umepotosha, uislam hausemi mwizi akatwe mkopo bali akiiba akalishwe chini na kuambiwa wizi mbaya na kupewa mawaidha ya kutosha akirudia tena ndio akatwe mkono...

Umeandika kimaskhara sana yani...Hakuna mtenda kosa ambae haFeel vibaya akitendewa vibaya Duniani inamaana ukifikiri mtendaji atajisikiaje Dunia ingekuwa na uovu mkubwa minajua nikikuchinja mkono wako utafikiria mimi nitajiakiaje ukinikata mkono pia So hutonikana hii inamaana
*nitaiba
*nitauwa watu
*nita baka
*nitalawiti
*nitafanya kilakitu kwasababu najua sitatendewa ubaya kwasababu nitaofanyia ubaya watawaza feeling zangu wataona nitajisikia vibaya nitaachw

Ulichoandika ni theory



Mwisho bado mujajibu alichouliza mtoa mada

Je aliyeuwa watu 1000 na hakuhukumiwa na mkono wa sheria kafa tu natural je kwake ndio ishaisha??
Unaweza kunipa maelezo nini kinamaanisha kwenye hii verse?

Allah says in the Quraan (5:38) - "As to the thief, Male or female, cut off his or her hands: a punishment by way of example, from Allah, for their crime: and Allah is Exalted in power."
 
Naanzia hapa, kwanba Ng'ombe haliwi ?
Haliwi na nini (nani) ?
Sababu Nyani haishi kama Mbwa.

Mungu ambaye ameumba ulimwengu na kuwawekea nidhamu ya kuishi viumbe wake.
Nini kinachokufanya uhisi huu ulimwengu umeumbwa na mungu?

Ni kwasababu kuran imesema?


Swali rahisi sana. Natumia tamko "Nani" sababu linahusiha mwenye maarifa, mjuzi, mwenye kujua,mwenye nguvu.
Sasa hii hutumika pale ambapo tayari ushapata uhakika


Huo ndiyo usahihi, unachotakiwa wewe ni kuonyesha kwamba haya si sahihi na uweke ukweli wako hapa.
Kutafuta majibu kwa kuuliza kwa dhana ya "nani" katika vitu ambavyo huvijui kunakufanya uonekane umejiwekea dhana yako kichwani kwasababu jibu linaweza likawa katika mfumo wa nini
Hili nimeshalijibu tayari.

Hayo mazingira nani ameyaweka ?
Ushajisetia kwamba jibu ni lazima liwe nani, umefunga ubongo kwa makusudi kwamba kivyovyote vile jibu lazima lifanane na hilo la mfukoni mwako
Yamejiweka au yametokea from nothing ?
Kwani haiwezekani kilichopo kikawepo bila chanzo?
Hakuna mwenye uthibitisho ya kuwa Dragons au Dinosaurs walikuwepo au kupata kuishi zaidi ya dhana na udanganyifu.
Sawa
Lipime hili kwa akili yako kisha uhakiki maandiko ya Wakristo utajua ni kweli au stori ?
Kama kila kitu kitakuwa kinakubalika kulingana na mtazamo wa mtu anavyoliona basi hukutakiwa kuweka madai kwamba kila kiumbe kilizaliwa kiislamu.


Dini ya kweli haipingani na akili ikiyo salama kadhalika uhalisia wa mambo. Hii ndiyo sifa anuai ya Uislamu.
Kila dini ina falsafa hizo hizo, niambie dini gani ambayo imejikataa kuwa sio dini ya kweli na kuipoint dini yako?

Au niambie wewe unakubalika kwenye dini gani nyingine tofauti na yako?
Swali la kwanza ili Wakristo wawe wa kweli, itabidi tuhakiki maandiko yao na watuambie Ukristo umeletwa na nani na ilikuwaje ukawa hivi ulivyo ?
Hii sio hoja, kumjua nani aliyeandika kitabu hakufanyi habari za hivyo vitabu kuwa kweli

Kuna vitabu vingi vimeandikwa na waandishi hawajulikani, so kwa hoja yako hapo huwezi kujua ukweli au uwongo kwasababu hujamjua mwandishi?
Kabla hujajibu hoja uwe unaisoma na kuitafakkari kisha uone inajibika au haijibiki.

Unakubali kwamba ukizaliwa una kuwa huna kitu katika maarifa, na ukikiri ya kuwa mimi nimekuwa muislamu sababu wazazi wangu ni waislamu, lakini kwangu mimi halikuishia hapa bali hoja na yale yakiyomo katika Qur'aan na Hadithi yamenifanya niwe imara zaidi.
Labda uniambie kati ya kuran na mtu nani aliyekuwa wa kwanza ku exist?

Halafu bado unazunguka pale pale kwenye muktadha wa kiislamu.

Ni sahihi wewe kujiona hivyo ulivyo kwa mujibu wa dini yako lakini kumbuka mafundisho hayo hayawezi kuwa sahihi kwa aliyekinyume na wewe
Ithibati hili iko wazi kabisa, tafuta mtu ambaye yupo cream hana uchafu katika akili yake, kisha mpe habari za kuwa hii dunia imeumbwa na aliyeumba ni mkamilifu wala hana mshirika, akikataa njoo utoe ushuhuda hapa.
Kwanza umeshajiwekea mazingira ya kukataa majibu, kwamba yeyote atakayekupa jibu ambalo haliendani na mafundisho ya dini yako atakuwa hayupo cream
Itakuwa hujui maana ya tamko itifaki.Ngoja nikupe faida, tamko "itifaki" ni tamko lenye asili ya kiaribu lenye maana "makubaliano" baina ya pande mbili. Swali, itifaki ipi umeizingatia hapa.


Siyo kweli, sababu ulicho kiuliza ni kinyume na ulichojibu, na hakitoi jibi la moja kwa moja. Sharti, la swali kuwa ni jibu la swali,halitegemei maelezo ya ziada toka kwa muuliza swali, yaani muulizaji akiulizwa swali anajua hili ni jibu.

Maelezo yako yalithibitisha ya kuwa huna swali wala maelezo yenye kujibi swali langu.
How?
 
Jamaa hachana na huu mjadala wa kipuuzi swali ulilouliza hakuna anayejibu wanazalisha mada nyengine tu.

Hachana na mjadala wa kipuuzi kama huu.
Siyo "hachana" sahihi ni "achana".
 
Haliwi na nini (nani) ?
Mwanadamu ana kula ng'ombe au hali ng'ombe ?

Kuna nini anakula ng'ombe ?
Nini kinachokufanya uhisi huu ulimwengu umeumbwa na mungu?
Hakuna kinachonifanya nihisi bali nina uhakika ya kuwa dunia imeumbwa na Mola, sababu hakuna kinyume chake.
kwasababu
Qur'aan imefafanua zaidi, ila akili na maumbile huonyesha ishara ya kuwa dunia na vilivyomo vimeumbwa. Huu tunaita "Self evident Truth". Ukiuona Ulimwengu akili yako inakupa muelekeo gani ? Kwamba ulimwengu umetokea from nothing au hauna chanzo ?
Sasa hii hutumika pale ambapo tayari ushapata uhakika
Si kweli,sababu lugha uhukumu, na tamko "nini" kwa kile kisicho na maarifa na kisicho weza kuunda, wala kutengeneza wala kuwa na lengo. Tafakari usiwe unaandika mambo bila kutafakari.


Naendelea....
 
Mwanadamu ana kula ng'ombe au hali ng'ombe ?

Kuna nini anakula ng'ombe ?
Inategemeana

Ni sawa na mimi nikuuulize watu wanakula nguruwe au hali nguruwe?


Hakuna kinachonifanya nihisi bali nina uhakika ya kuwa dunia imeumbwa na Mola, sababu hakuna kinyume chake.
Una uthibitisho?

Qur'aan imefafanua zaidi, ila akili na maumbile huonyesha ishara ya kuwa dunia na vilivyomo vimeumbwa. Huu tunaita "Self evident Truth". Ukiuona Ulimwengu akili yako inakupa muelekeo gani ? Kwamba ulimwengu umetokea from nothing au hauna chanzo ?
Self evident truth is completeley fallacy

Kwamba madai fulani yanatakiwa kukubaliwa kua ni kweli pasipo kua na ushahidi au uthibitisho ambao haujawekwa kwasababu inajulikana dhahiri

Self evident truth ni njia ya uwasilishaji wa hoja ambayo haihitaji uthubitisho au explanation kwa mantiki hiyo utajikuta unakubali hata jambo la uwongo
Si kweli,sababu lugha uhukumu, na tamko "nini" kwa kile kisicho na maarifa na kisicho weza kuunda, wala kutengeneza wala kuwa na lengo. Tafakari usiwe unaandika mambo bila kutafakari.


Naendelea....
Sawa
 
Kutafuta majibu kwa kuuliza kwa dhana ya "nani" katika vitu ambavyo huvijui kunakufanya uonekane umejiwekea dhana yako kichwani kwasababu jibu linaweza likawa katika mfumo wa nini
Jifunze kutumia tamko "dhana" kwa usahihi wake. Hakuna dhana ya nani, katika uhakika usio na shaka, sababu tamko "nani" ni kwa kuuliza juu ya yule mwenye kujua mwenye maarifa yaani mwanadamu, na nini ni kwa hayawani. Sasa tupe sababu za kwanini isiwe "nani? " na iwe nini au mfano wake.

Tuonyeshe wapi tamko "nini" linakaa katika munasaba wa asiyekuwa Hayawani ?

Kadhalika "nini" si mfumo bali ni tamko tu la kuulizia swali kwa kile kisicho na akili. Jitahidi kuyapa maneno stahiki zake.
Ushajisetia kwamba jibu ni lazima liwe nani, umefunga ubongo kwa makusudi kwamba kivyovyote vile jibu lazima lifanane na hilo la mfukoni mwako
Sasa mbona unahangaika kijana, wewe onyesha nilipo kisea kisha tuambie kwanini isiwe "nani? " na iwe vinginevyo. Usipoteze muda sasa. Maana unazidi kuonekana kituko.
Kipi hicho,embu tatajie.
Kwani haiwezekani kilichopo kikawepo bila chanzo?
Mimi najua ni Mola pekee ndiyo hana chanzo. Je na wewe unakubaliana na mimi katika hili ? Kama unakinzana na mimi, naomba uniambie ni kipi hicho kipo pasi na chanzo ?
Kama kila kitu kitakuwa kinakubalika kulingana na mtazamo wa mtu anavyoliona basi hukutakiwa kuweka madai kwamba kila kiumbe kilizaliwa kiislamu.
Hili unalisema wewe, ndiyo maana nimekuhimiza kuhakiki unachokidai sababu ukweli ni mmoja na uko wazi.
Kila dini ina falsafa hizo hizo, niambie dini gani ambayo imejikataa kuwa sio dini ya kweli na kuipoint dini yako?
Dini yangu haina Falsafa ndiyo maana ni ya kweli na haipingani na uhalisia na akili iliyo salama.

Dini hizo nyingine zinapingana na hayo niliyo yataja na asili ni matamanio ya nafsi wmya watu fulani kwa malengo maalumu.
Au niambie wewe unakubalika kwenye dini gani nyingine tofauti na yako?
Hili swali sijalielewa. Naomba ufafanuzi.
Hii sio hoja, kumjua nani aliyeandika kitabu hakufanyi habari za hivyo
Nimecheka kidogo, kisha nikahitimisha hujui jabari za vitabu, nakuonyesha umuhimu wa kumjua muandishi ili tujue habari amezipata wapi ? Kwa kuzembea hili leo hii Ukristi umekuwa na upagani mwingi, ushirikina mwingi, sababu Mitume hawakuwahi kuwa washirikina, wala wapagani waka hawakuwa Waongo.

Au kupatikane njia nyingine ya kweli zaidi kuipa nguvu hii ya muandishi asiye julikana.
Kuna vitabu vingi vimeandikwa na waandishi hawajulikani, so kwa hoja yako hapo huwezi kujua ukweli au uwongo kwasababu hujamjua mwandishi?
Katika elimu ya uhakiki wa habari, habari zao hazifanyiwi kazi mpaka kupatikane mapito mengine ya kweli yenue kuipa nguvu habari hiyo au kitabu hicho, katika istihali husemwa "Majhuuli (Yaani muandishi au mpokezi wa habari hajulikani). Hii ni njia mojawapo ya kudhoofisha habari.

Na ndio maana kuna habari nyingine hutakiwi kuzikataa wala kuzikubali.

Naendelea....
 
Self evident truth is completeley
Hili tatizi lingine, utakuwa huujui huu ukweli. Ng'amua huu mfano wa "Self Evident Truth". Ukiona simu unaona nini yaani nini kina kuijia katika kuona kwako hiyo simu ?
Kwamba madai fulani yanatakiwa kukubaliwa kua ni kweli pasipo kua na ushahidi au uthibitisho ambao haujawekwa kwasababu inajulikana dhahiri
Ukiona nyumba unataka ushahidi gani kuonyesha ya kuwa hiyo nyumba imejengwa na kusanifiwa na mtu mwenye ujuzi juu ya ujenzi na ameijenga hiyo nyumba kwa lengo maalumu ?

Au tukikuona wewe, kuna hitaji ushahidi gani kuonyesha ya kuwa wewe umetokana na baba na mama, na baba yako ni mkubwa kiumri kuliko wewe ?

Nilijua tu ya kuwa huujui huu ukweli timilifu.

Naendelea....
 
Labda uniambie kati ya kuran na mtu nani aliyekuwa wa kwanza ku exist?
Bila shaka unamzungumzia Adamu. Adamu ndiyo alianza kuwepo. Naama, hoja yako iko wapi hapo ?
Halafu bado unazunguka pale pale kwenye muktadha wa kiislamu.
Sasa unataka niende wapi kwingine wakati Uislamu ndiyo Ukweli wenyewe na sisi sote tuko hapa kuutafuta ukweli.

Usipate shida,wewe onyesha uongo wa Uislamu.
Ni sahihi wewe kujiona hivyo ulivyo kwa mujibu wa dini yako lakini kumbuka mafundisho hayo hayawezi kuwa sahihi kwa aliyekinyume na wewe
Safi kabisa sasa yule ambaye yuko kinyume na mimi anatakiwa kuonyesha ukweli wake. Rahisi sana.
Kwanza umeshajiwekea mazingira ya kukataa majibu, kwamba yeyote atakayekupa jibu ambalo haliendani na mafundisho ya dini yako atakuwa hayupo cream
Akinipa majibu sahihi nitakubaliana nae tu, hamna namna.
 
Back
Top Bottom