Kwani kusema hili jambo ni baya na hili ni zuri ni lazima uamini Mungu?
Kwani kusema hili jambo ni baya na hili ni zuri ni lazima uamini Mungu?
Mbona sheria walizojiwekea watu tu katika secular settings zinahukumu wauaji bila kuhitaji msahafu wa Mungu?
Walioshiriki mauaji ya Wayahudi Ujerumani walihukumiwa na mahakama ya Nuremberg wakapatikana na hatia.
Mahakama ya nuremberg haikuwa ya kidini.
Wanaouliza maswali wamesoma historia?
Hapa unataka kujenga hoja gani?Hitler, Stalin, Iddi Amini, Mobutu na wengine wengi ambao walifanya ukatili wa kutisha na hawakuukabili mkono wa sheria ndio kusema hatima yao iliishia pale walipokufa tu?!
Hapa unataka kujenga hoja gani?
Kwamba lazima kuna Mungu na hukumu baada ya kifo kwa sababu watu wakatili hawawezi kufanya ukatili wao halafu mwisho wao ukawa kifo tu wasilipie ukatili wao?
Ukisema hivyo, utakuwa sawa na mtu aliyetembea kilomita mia, akagundua kwamba kapoteza hela yake noti ya shilingi 10,000 sehemu fulani katika safari yake. Halafu hapo alipo ndiyo sehemu pekee yenye taa, hivyo, anaamini lazima noti yake imepotelea hapo, kwa sababu hapo ndipo sehemu pekee yenye taa!
Logical non sequitur.
Hilo linawezekana kuwa kweli, ingawa nalo linajadilika tofauti.Asilimia kubwa ya binadamu wakiamini na wakiwa na uhakika hakuna hukumu baada ya kifo, kwamba zaidi ya hizi hukumu za duniani hakuna kitakachoendelea dunia inaweza kuwa uwanja wa fujo na mahali hatari sana.
Ni heri watu waendelee kuamini kuna hukumu baada ya kifo.
Kaka wewe umenielewa vizuri sana.Hitler, Stalin, Iddi Amini, Mobutu na wengine wengi ambao walifanya ukatili wa kutisha na hawakuukabili mkono wa sheria ndio kusema hatima yao iliishia pale walipokufa tu?!
Jiangalie wewe mwenyewe kisha tafakari, utapata jibu.Unadhibitisha vipi kuwa mungu yupo?? tuanzie hapa kwanza
Poa.Mkuu jaribu kuhoji ama kuuliza maswali ya maana zaidi ya haya kiongozi.
Naamini bado unaweza kuuliza maswali yenye mantiki zaidi.
Ahsante
Hujaelewa nilichokiandika. Nawazungumzia Wakana Mungu wanasemaje juu ya hilo ?Kwani kusema hili jambo ni baya na hili ni zuri ni lazima uamini Mungu?
Mbona sheria walizojiwekea watu tu katika secular settings zinahukumu wauaji bila kuhitaji msahafu wa Mungu?
Walioshiriki mauaji ya Wayahudi Ujerumani walihukumiwa na mahakama ya Nuremberg wakapatikana na hatia.
Soma historia ya kesi maarufu za wafuasi wa Nazi, za "The Nuremberg Trials". Soma historia ya Rudolf Hess.
Mahakama ya nuremberg haikuwa ya kidini.
Wanaouliza maswali wamesoma historia?
Nimecheka sana we jamaa sio aisee,, hiyo avi + id + ulichocoment yaani,,😂😂Survive for fitness hata Simba anaingaika kila siku huku na kule ili apate kuwa mfalme wa nyika ila ukileta vurugu anakubutuwa
Iko hivi hapa duniani lazima watu wababe wanyonge wakatili wapole wachawi wema wanafki waoga wajasiri wawepo ili kuweza kubalance maisha hao wababe wezi wenye kufldhulumu ndiio wajanja habari za duniani zinaisha hapa hapa duniani
Nataka nikuonyeshe ya kuwa alichokiandika ni UONGO na hawezi kuthibitisha. Kisha utanionyesha ukweli wa alichokiandika hapo.Post no #10 Kiranga kaeleza vizuri mno ni swala la kutafakari tu mkuu,,
Watu wanajua Mungu yupo na wanafanya maasi, hii ni sababu ya uhuru aliotupa,na wewe unaamini ya kuwa Mungu hayupo /na ushahidi huna/ unafanya maasi.Unachoonekana kusema hapo ni kwamba, imani ya kuwepo Mungu ni muhimu hata kama Mungu hayupo, kwa sababu watu wakijua Mungu hayupo na hakuna hukumu ya mabaya baada ya kifo, watafanya maasi sana.
Unaposema haya ni maelezo mazuri ila natakiwa kufikiria, ukitakiwa umuukize maejuaje ya kuwa Mungu hayupo na akuthibitishie kisha asema yaliyofata. Kadhalika akwambie ingekuwaje hii dunia pasi na aliyeiumba mwenye maarifa, msanifu, mjuzi wa kila kitu na mwenye malengo juu ya kuiumba hii dunia.Mimi najua Mungu hayupo, na kwa sababu najua Mungu hayupo, mara nyingi watu wanapoomba msaada nakuwa wa kwanza kusaidia.
Hii kauli si ya kweli,na nyinyi mnaiita "Strawman Argument", yaani una potosha ukweli kwa kuweka jambo nusu au lisilokuwepo. wanaosema kauli hii hugawanyika na huwa na sababu, wapo hutoa msaada kwanza kulingana na uwezo hukur wakitarajia malipo toka kwa Mola, huku kilichobakia Mola atamsaidia, kadhalika husema hivyo kwa yale ambayo yako nje ya yule alitakwa msaada.Watu wanaamini uwepo wa Mungu wengi wao wakiombwa msaada huishia kusema "Mungu atakusaidia".
Post no #10 Kiranga kaeleza vizuri mno ni swala la kutafakari tu mkuu,,
Wanamuachia
Hapa mpaka nikajiuliza ameeleza nini hapa mpaka unasema ametoa maelezo mazuri ?Wanamuachia Mungu kazi ya kusaidia. Mtu anakosa msaada.
Hii si kweli sababu imani hiyo huamrisha watu wafanye mema, na huonyesha ubora wa watu kufanua mema, kwahiyo ukiona watu wanafanya maovu ujue hawaifanyii kazi imani hiyo. Hii nayo ni aina ya upotoshaji.Kwa hivyo, imani ya kuwepo kwa Mungu mara nyingine inakwamisha mema kufanyika.
Hili swali rahisi sana, sababu watu hao wamepewa uhuru wa kuchagua kufanya mema au maovu. Ndiyo maana utakuta mtu anaamini hilo na anaiba, anazini na mfano wake.Pia, naweza kukuuliza, mbona leo watu wengi wanasema wanaamini kuna Mungu na hukumu na bado wanafanya maasi mengi sana tu?
Sasa kwa wale ambao mkono wa sheria ulikuwa mfupi kwao na haukuwafikia kifo ndiyo "karma" kwao ? Na wale waliodhulumiwa na wao malipo yao ni nini na faraja yao huipata wapi ? Hitimisho la hapa ni kuwa Ubudha ukijengeka katika msingi wa ujinga na matamanio na si elimu na ithibati.Na zaidi, kuna watu wengi sana kama baadhi ya Buddhists ambao hawaamini Mungu yupo, wao wanaamini katika "karma" tu,
Swali la msingi ni je ubaya unaupimaje na uzuri unaupimaje...? Maana wapo wanao kufa kabla ya kuyadiriki mazuri yao na mabaya yao kwa mujibu wa hiyo Karma.kwamba, ukifanya mambo mazuri, mazuri yatakurudia, na ukifanya mambo mabaya, mabaya yatakurudia.
Uzuri wa maisha unaupimaje ?Na hawa jqmii zao zinaenda vizuri tu bila kuhitqji uwepo wa Mungu? Tena wengine wanaishi vizuri kuliko jqmamii zinazoamini uwepo wa Mungu