Swali kwa wasomi wa Jiografia na Fizikia wenye akili zao, kama ulienda shule kukariri pita mbali

Hao uwatakao wataishia kujing'atang'ata tu hapa kama kwenye ule uzi wenye poll.
Acha tu sisi fom foo feliya tujitutumue maana wao wakija wanaleta hoja za kukaririshwa

Ni kwamba
Hakuna dunia inayozunguka hata spidi ya 0.000000001 km/h. Dunia ni stationery
Jua na mwezi ndivyo vinavyomove always
Hakuna kitu force of gravity bali ni utaalamu wa kihisabati umebuniwa tu kisha kitu ikabalance
Dunia (ardhi) haiko curved wala bahari wala anga ukitaka kuamini watafute wataalamu wa bahari na anga hususani marubani ila tafuta walio waaminifu hasa
 
Majibu ni haya hapa.

Kwa kuongezea tu tunaposema dunia geographically ina structure mbili.

1. Internal structure of the earth na,
2. External structure of the earth.

Internal structure inajumuisha uso/ardhi ya dunia kwenda katikati ya kitovu cha dunia, chini huko yanakopatikana madini gas na mafuta.

External structure inahusisha anga ambalo lina matabaka adhaa(>5)(atmosphere)

Katika matabaka ya anga kuna mengine yanapitisha ndege ndogo za kiraia mengine yanasaport ndege kubwa za mizigo, mengine yanasapoti ndege na rocket zenye speed/mwendo kasi mithili ya kasi ya sauti (supersonic)

Matabaka mengine ni yanatabia au sifa ya kupitisha mawimbi ya mawasiliano kama vile radio hata mtandao ya simu(Internet), jingine ndio hili la chinichini ambako mawingu yanaundwa na kufanyia mvua.

Kwaiyo tunaposema dunia tunajumuisha na umbali wa kilomita kadhaa kwenda huko juu angani ukimaliza umbali huo wa anga la dunia... Kuendelea huko mbele ni mbali sana ni nje ya dunia na hata kani ya mvutano inatoweka (force of gravity).

Huko sasa ndio kinaweza kikaninginizwa kitu na kisiasiliwe na nguvu yoyote ya dunia Kwahiyo dunia ikiwa inazunguka chenyewe kiko pale pale.
 
Hili ni swali fikirishi mno! Linataka logic sana kulijibu
 
Ukiwa ndani ya gari ukiruka ndani Kwa ndani Huwa unaachwa na gari? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ nimejiwazia kaujinga fulani hapa! Enewei wasomi mnisaidie hapo


Nani aliyewahi kupima spidi ya dunia akapata hizo 1674km/h?
Kasi ya mzunguko wa Dunia imetokana na kazi za wanasayansi kadhaa waliogundua jinsi Dunia inavyozunguka na jinsi ya kupima kasi yake.

Hii inahusiana na uelewa wa mzunguko wa Dunia na urefu wa siku, kazi iliyofanywa na wanasayansi kama Galileo Galilei, Isaac Newton, na Jean Foucault.

Hapa kuna njia rahisi ya kuelewa jinsi kasi ya mzunguko wa Dunia (1,674 km/saa) ilivyopatikana:



1. Urefu wa mzunguko wa Dunia: Dunia ni duara, na mduara wake wa ikweta ni karibu kilomita 40,075. Hii ni umbali unaozunguka Dunia yote kwenye mstari wa ikweta.

2. Muda wa mzunguko wa Dunia:
Dunia inazunguka mara moja kila baada ya takriban masaa 24 (siku moja).

3. Hesabu ya kasi ya mzunguko.
- Kasi ya mzunguko inapatikana kwa kugawa urefu wa mzunguko wa Dunia na muda wa mzunguko.

lugha nyepesi ya kimahesabu

Kasi ya mzunguko=40,075 km Γ· 24 saa β‰ˆ 1,674 km/saa


Mtu ambaye aliweka bayana mzunguko wa Dunia kwa kutumia majaribio ya kifedha na ya kitaalamu ni Jean Foucault. Mnamo mwaka 1851, alitumia pendulum maarufu inayoitwa Pendulum ya Foucault ili kuthibitisha kuwa Dunia inazunguka. Pendulum hiyo inaonyesha mzunguko wa Dunia kutokana na jinsi mwelekeo wa mzunguko wa pendulum unavyobadilika polepole kwa siku nzima.

Kwa hiyo, kasi ya Dunia ilipimwa kwa kuchanganya uelewa wa kijiografia, hesabu, na majaribio kama ya Foucault, na wanasayansi wa sasa wanaweza kudhibitisha kwa vifaa vya kisasa kama satellites.

Naimani umepata kitu hapo.
 
Uzito wa njiwa utakuwa kilo ngapi?
 
Watu wanajadili mambo ya sayansi,wewe unaleta mambo ya kufananisha kusoma kuran kutoka kushoto kwenda kulia.
Kuna wakati hata kama una chuki na imani fulani yakupasa ufiche maana tunakuona kituko
 
Ndio maana nakwambia kua wewe ni punguani,vicomment vyako vingi hapa JF vimejaa upumbavu ulioujaza kichwani,

Hii mada inahusiana nini na mambo ya Udini?
 


Kwa kutumia kanuni ya Newton ya pili ya mwendo na uhifadhi wa nguvu (conservation of momentum).

Ndege (aeroplane) bado itakuwa imebeba uzito ule ule wa kilograms 1000 wa njiwa, hata kama watakuwa wanaruka ndani ya ndege bila kugusa sakafu.

Hii ni kwa sababu uzito wao bado utaathiri ndege hata kama wapo angani ndani ya ndege hiyo.

Kiaje inakuwa hivo?​

  1. Njiwa wanatumia hewa ya ndani ya ndege kupaa: Wakati njiwa wanapaa, wanapiga mbawa zao, na kusababisha mgandamizo (pressure) wa hewa chini yao. Hewa hii inasukumwa chini na mbawa zao, na kisha inasukuma njiwa juu. Lakini kwa kuwa hiyo hewa iko ndani ya ndege, nguvu ya kusukuma hewa chini inahamishiwa sakafuni mwa ndege (aeroplane)
  2. Uhifadhi wa nguvu: Nguvu wanayotumia njiwa kupaa (kusukuma hewa) inasambazwa kwenye sakafu ya ndege. Hii ina maana kwamba hata kama hawagusi moja kwa moja sakafu, hewa wanayoisukuma chini bado inaleta shinikizo kwa ndege, na kwa hivyo uzito wao unahamishwa kwenye ndege.
  3. Mfano wa lifti: Fikiria uko kwenye lifti yenye mzigo mzito, na kisha ukaanza kuruka ndani ya lifti. Wakati unaruka, unatumia nguvu dhidi ya sakafu ya lifti ili kusukuma mwili wako juu. Hata kama umekatika kutoka kwenye sakafu kwa muda mfupi, lifti bado inabeba uzito wako kwa sababu nguvu unayotumia kuruka inatokana na lifti yenyewe. Vivyo hivyo sawa na njiwa ndani ya ndege.
Kwa hiyo, hata kama njiwa wanapaa ndani ya ndege, uzito wao bado unaathiri ndege kwa njia ya mgandamizo wa hewa, na ndege inabeba uzito wao wote wa kilogramu 1000.

Kwako mwalimu kashasha. 😊
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† haya ya kusema assume halafu kwenye conclusion unasema therefore!!
 
Watu wanajadili mambo ya sayansi,wewe unaleta mambo ya kufananisha kusoma kuran kutoka kushoto kwenda kulia.
Kuna wakati hata kama una chuki na imani fulani yakupasa ufiche maana tunakuona kituko
Hako ka kiumbe ndio kalivyo,kameona hakana cha kuchangia hapa ndio kakaamua kuleta upuuzi wake,ni kamtu kamoja kasikokua na faida yeyote ile zaidi ya ujinga tu.
 
Nilitaka kujibu lakini naona kama umemaliza mambo yote muhimu.

I second this answer.
 
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…