Swali: Kwanini project nyingi ndogo ndogo za afrika ili ziendelee, inabidi tuombe pesa toka huko kwa wazungu? Kwetu hatuna matajiri?

Swali: Kwanini project nyingi ndogo ndogo za afrika ili ziendelee, inabidi tuombe pesa toka huko kwa wazungu? Kwetu hatuna matajiri?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Habarini:

Sizungumzii project kuuubwa, k.v ujenzi wa SGR au bwawa la umeme nazungumzia project za kawaida kama ujenzi wa choo cha wanafunzi, au darasa au maabara kwenye shule, au ujenzi wa vyumba vya waalimu, kisima, dispensary etc

Sometimes unakuta hela inayohitajika sio pesa nyingi sana, maybe tsh million 5 tu, ila kuipata mpaka aombwe mtu alietoka ujerumani aje achangie.

Nilishudia kwenye taasisi moja ya kidini, mishahara ya baadhi ya wafanyakazi ya mwezi huo, ililipwa na hela ya lunch ya mtu alietoka ulaya.

Ina maana Tanzania hatuna watanzania wenzetu ambao wako vizuri kiuchumi, wa ku sponsor hivyo vitu.

Mfano kama mtanzania ni tajiri, ameona kwenye shule ya serikali kuna ubovu wa majengo na uhaba wa vitendea kazi, process za kuomba afadhili ujenzi wa hio shule bure bila kutegemea malipo, inakuwa vipi? Au kuna ugumu wanawekewa.

Binafsi nikiona mzungu anakuja Tanzania kufadhili mradi, sijui kutugea vitabu, vyandarua, kutujengea darasa, daah huwa nahisi tunadharaulika sana.
 
Back
Top Bottom