Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Sijaelewa vizuri hivi suala la kununua ndege likikua ni siri?

Nani alipaswa kutunza siri ya ununuzi wa ndege hiyo?
Kwa nini aliyepaswa kutunza siri ya kununua ndege hiyo hakufanya hivyo.

Je, ndege imezuiliwa kwa Tamko la Lisu au ni wadai wetu wenyewe waliamua baada ya kuambiwa kuwa tumeweka order ya kutengenezewa ndege Canada na itakamilika tarehe fulani tena bei yake ni sh. Kadhaa.

Serikali isimtupie Lisu lawama wao wenyewe ndio walioanza kutoa siri mahali wanapokwenada kutengenezwa ndege. Bila shaka hawakujua madhara yake . Waliangalia umaarufu wa kisasa tu kuwa serikali imenunua ndege. Walikua kila siku ndio ishu kwenye vyombo vya habari.
Ina maana hao wanaoitwa maadui wetu walikua hawasikii matambo ya serikali kuwa wameweka order ya ndege mpya?
Wakati mwingine serikali inunue vitu vyake kimya kimya sio lazima waweke hadharani kila inachofanya tena kinakuwa ni gia ya kisiasa.
Mbona wakinunua magari ya kifahari hawatangazi kuwa yanaingia lini na yameanza lini kutengenezwa! Kama tumeshajua kuwa tuna maadui kama tunavyoambiwa leo basi serikalia iwe ya kwanza kutunza siri zake na isiwaambie hata wananchi kupitia vyombo vya habari mana wao wakiona watapata maujiko kwa wananchi wajue pia wapinzani wanatafuta maujiko?

Japo pia siamini katika kuficha ukweli unaoihusu jamii nzima.
Tukiweka mfumo wa kuficha maovu ya viongozi tutafanikiwa kujenga ufisadi mkubwa sana kwa wakubwa .
Mana ukifichua kuwa kuna pesa za nchi zimefichwa nje ya nchi na ukashirikiana na wale walioko nje kupata ushahidi utaitwa msaliti,mhaini, kibaraka na asiye na uzalendo kwa sababu utakaowatuhumu ni lazima wawe ni wale wenye madaraka itakua ni vigumu kusikilizwa.

Je, ni ukweli upi utakaoitwa wakizalendo kama wanaoutoa watakamatwa na kutangazwa kuwa ni maadui wa nchi.

Je, hali hii ya kuficha ukweli kwa sababu ya kulindana mana mimi sioni kuwa ni kulinda maslahi ya nchi bali kulinda maslahi ya watawala na nafasi zao ukiendelea na watu wakaficha siri zote ni lini ufisadi utapungua ? Mana binadamu anatabia ya ubinafsi pale anapohisi yuko peke yake na haonekani.

Mfumo wa vyama vingi unaendana na uwazi na sio siri.

Ndio maana umetolea
Mfano wa familia ukasahau kuwa siri za familia ni jambo la mtu binafsi. Ni mtu na nafsi yake mwenyewe. Umezini wewe mwenyewe lakini akitokea mtu anayemtaka mkeo halafu akapata ushahidi wa kweli kuwa ulizini basi atampelekea mkeo ili kwake iwe rahisi kuvuruga ile imani ya mkeo kwako.
Ndivyo inavyofanyika kwenye siasa pia. Wapinzani wakigundua siri ya watawala basi wanaiweka wazi ili kuwaambia wananchi kuwa mnatawaliwa na watu waliokoasa umakini na wanalipa taifa hasara?

Dawa ya siri ni kuwa mkweli na mwaminifu.
Kutoa siri za wahalifu walioliibia taifa itajenga umakini na itakuwa ni fundisho kwa wale wanaotumia madaraka vibaya na kulisababishia taifa hasara.

Tangu waziri fulani alipobainika kuwa alikwenda kwa siri kuweka mikataba ya madini nje ya nchi mpaka leo haikuwahi tena kurudiwa hali kama ile kwa kuwa ilikemewa hadharani.

Tuwe wazalendo kwa kurudisha Azimio la Arusha na miiko ya maadili ya uongozi iwekwe kwenye katiba hata kama ni kuweka kiraka kwenye katiba iliyopo na sio uzalendo wa kuficha maovu ili kuwalinda waovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi.

Huu ni uzi kuhusu Swali la Morality: Jee ni Lazima Kuusema Kila Ukweli Unaousikia?. Kwenye Medani za Siasa, Kabla ya Kuusema Ukweli Tunausikia, Jee Tutangulize Mbele Maslahi ya Taifa Kwa Kuupima Kwanza, Ukweli Huo Una Matokeo Gani, au Ukisikia Lolote, Lisema Tuu kwa Sababu ni la Ukweli?.

Jee Ili Kupata Manufaa ya Kisiasa, Jee ni Lazima Wanasiasa Wetu, Tupoliticise Kila Kitu?.

Declaration of interest.
Mimi Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu ya mwana habari, (carninal rule ni " tell the truth, no matter what!", hivyo mimi mtu mkweli daima, na ni muumini wa ile ahadi ya mwana TANU " Nitasema kweli daima, fina kwangu mwiko", ila katika kuusema ukweli au kuandika ukweli, pia ninatanguliza maslahi ya taifa kwa kujiuliza jee ukweli huu ukisemwa, utajenga, au utabomoa?.

Ukiona japo ni ukweli lakini utabomoa, then ukweli huo, siusemi, kama ukweli niliousema kwenye bandiko hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...

Hii Kamata Kamata ya Kila Waompinga Magufuli, Ni Magufuli Anawatuma au Wanajipendekeza Tuu?.
My honest opinion, ingawa ni kweli rais Magufuli apendi critics, mimi nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu toka kwenye kinywa chake na sio kwa kuhadithiwa kuwa anapenda challenge, ila hizo challenge ziwe ni ukosoaji wa kweli wenye nia njema, hivyo naamini hizi kamata kamata zinazoendelea ma kuwakamata karibu kila wanasiasa wanaompinga rais Magufuli, siamini kama ni Magufuli anawatuma!, naamini hivyo ni kazi ya polisi ambao wana jikomba komba tuu ili kuonekana wanafanya kazi.

Kwenye siasa za multipasim duniani kote, kazi ya the opposition ni kuopose kila kitu kinachofanywa na chama tawala hata kiwe ni kitu kizuri namna gani!, that is their right, kupinga, ndio maana wanaitwa wapinzani. Na serikali zote zinazoheshimu demokrasia ya kweli, lazima zikubali kupingwa.

Nimeishi kidogo UK na US, na Uswiss. Uingereza pale Times Squire katibu kila ni maandamano. US ulle mtaa jirani na Capitol Hill kuna uwanja unakuwa huru kupinga chochote, Uswiss uwanja huru wa kupinga, ni pale uwanja wa wazi nje ya ukumbi wa Bunge, the The Bundes House. Hivyo sioni mantiki ya sababu zozote wanaompinga rais kubughudhiwa!, this is not demokracy, Tanzania sio nchi ya kidikiteta!.

Wito kwa IGP, Kamanda Sirro, controll vijana wako watekeleze majukumu yao kwa sheria taratibu na kanuni na sio kwa kutaka kujipendekeza au kujikomba komba!.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti ...

Jee Wapinzani Kazi yao ni Kupinga Tuu Kila Kitu au Kukosoa Tuu Hakuna Kupongeza Hata kwa Mazuri?.
Japo kazi ya upinzani ni kupinga na kukosoa, lakini tunapokuja kwenye issues muhimu kwa maslahi ya taifa, maslahi yataifa ndio yanatangulizwa mbele, sisi sote kama Watanzania, we stand as one, tunakuwa watu wamoja, hakuna tena siasa za vyama, wala siasa za watu, tunaitanguliza mbele Tanzania, kila kitu kinafuatia baadae.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...
Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El ...

Conclusion
Namalizia kwa haya maswali ya msingi, japo kuhusu ni hoja za morality kusema kweli daima, lakini Jee ni Lazima Kuusema Kila Ukweli Unaousikia?. Kwenye Medani za Siasa, Kabla ya Kuusema Ukweli Tunausikia, Jee Tutangulize Mbele Maslahi ya Taifa Kwa Kuupima Kwanza, Ukweli Huo Una Matokeo Gani, au Ukisikia Lolote, Lisema Tuu kwa Sababu ni la Ukweli?. Jee Ili Kupata Manufaa ya Kisiasa, Jee ni Lazima Wanasiasa Wetu, Tupoliticise Kila Kitu?.Sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni ni kweli!.

Wasalaam.

Paskali

Rejea.
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa ...
Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
Kitendo cha kuita nchi majirani zako kuwa ni "vinchi" ni uungwana ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hoja ya Udikiteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi ...
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio ...
"In a time of deceit telling the truth is a revolutionary act" -George Orwell. Mungu atusaidie sana watanzania
 
Ni kweli kaka yangu pascal lakini liko tatizo kubwa la kiukoo ambalo litaigarimu familia nzima ya watanzania (Tabia ya makuzi)hujenga desturi
Kwa zaidi ya miaka 20 ya utawala wa mwalimu tulijengewa huo utamaduni kutobishana na viongozi kila alichosema kiongozi kilikuwa dhahabu hata kama ni jiwe.

Kumi la tatu la Tanzania huru lilishuhudia likianza kuwajengea watanzania kujiamini na kuhoji, sio kila asemacho kiongozi ni dhahabu kwenye jiwe tukafundishwa kusema jiwe darasa hili liliendeshwa na mwalimu Nyerere mwenyewe kumbuka hotuba maarufu ya Mwl may mosi Mbeya na press conf za mwl hapa Dar.
Kumi la nne la makuzi yetu vyama vya upizani vilianzishwa na mwl akaendelea kutujengea kujiamini na vyama vya upinzani hali kadharika huku akiikemea tabia ya CCM kutegemea polisi badala ya ushawishi wa kisiasa kumbuka ishu ya wananchi kusukuma gari la mrema aliitaka serikali iache mara moja kupambana na wananchi wanaotaka kusukuma gari la mrema au hata kumbeba, kama wameridhia na anaebebwa kama amerdhia kubebwa kama maiti sio kazi ya serikali kuzuia. kauli hii bado ni fundisho kubwa hadi leo hasa kwa awamu hii maana kutokana kauli hiyo serikali iliacha kufukuzana na wabebaji, wabebaji wakaona hakuna sababu ya kubeba maiti,mbebabwaji nae akaona yeye sio maiti biashara ikafa kisiasa na sio kibabe kwa kutumia nguvu ya dora,
Kumi la tano tulishuhudia makuzi na kuanza kukomaa kwa vyama vya upinzani vikaacha kukaa ofisini kusubili uchaguzi vikahamia field uhuru wa habari ukashamiri watanzania wakazidi kujiamini na kuhoji kauri za viongozi,ahadi,matendo,uaminifu na uzalendo wa viongozi kwa ujumla demokrasia ilianza kunawili na huenda wazee wa ukoo hawakulipenda hili na kwa kuwa mhenga wa ukoo alishatutoka hawana wa kuwakemea wanataka kumnyonga kijana demokrasia kabla hajapevuka ili asiwapigie kelele tena watawale kwa raha mstarehe.

Mwanzo wa kumi la sita manju mpya ameingia hataki mamanju wenzie nyimbo zao zisikilizwe anao wimbo, wimbo wa matumaini yaliyopotea wimbo wa maendeleo,toka wimbo huu uanze kuimbwa kuna baadhi ya beti za wimbo huo zimeleta ukakasi kwenye ukoo zimewatia simanzi baadhi ya watu na kutumbukia nyongo, maana wakati mwingine manju wetu huwa hachagui maneno ya kidipromasia ya kuweka kwenye wimbo wake na hata yeye husema yeye ni msema kweli, na ukweli wakati mwingine huumiza,aache watu wateme nyongo ili kuleta utulivu kwenye ukoo.

Ushauri wangu manju lazima akubali kukosolewa na ni lazima akubali manju wengine waimbe ili ajue ni wapi anakosea kwenye nyimbo zake arekebishe.

La mwisho sio kazi ya vyombo vya dola kupambana na wapinzani wa manju hatuna sababu ya kutathimini kauli zetu hazijareta madhara huko nyuma zaidi ya faida.
 
Sio kila ukweli lazima usemwe, especially kwa watawala. Mtawala ni mtu ambae anaongoza watu wenye itikadi tofauti, dini tofauti, makabila tofauti, makundi mbalimbali na n.k. Sasa priority no.1 ya mtawala anayeongoza makundi tofauti lazima iwe ni kuwaleta pamoja watu wote, makundi yote yajisikie amani. sasa kunaweza kukawa na ukweli ambao unaleta msuguano baina ya makundi anayoongoza haina haja ya kuusema kama hauleti faida yoyote ni bora ukabaki nao ili unaowatala wafeel kama wewe ni kiongozi wa wote sio mbaguzi.

Mfano, katika kipindi cha Rais Obama akiwa madarakani aliutambua mji wa Tel aviv kama ndio mji mkuu Israel na hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuharmonize mambo ili aonekane hajalalia upande wa Israel wala Palestina. Sasa amekuja mtu wa type ya hao viongozi waropokaji wasiofikiria madhara kabla ya kuongea kabwabwaja kwamba Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel na anahamishia ubalozi wake kule tofauti na tamko la UN, tofauti na EU na Africa hali iliyopelekea machufuko na mimia ya watu kuuawa kwa ajili ya tamko la mtu mmoja tu. Obama sio kwamba alikuwa hajui kwamba mji mkuu wa Israel ni Jerusalem lakini kwa ajili ya kuleta amani ili watu wasiuane alichagua Telaviv

Sasa kipi bora ukweli unaoleta machafuko na mauji au kutumia diplomasia ya mazungumzo inayoleta amani na furaha baina ya pande mbili au zaidi hasimu.

Ushauri wangu, kiongozi huwa anajua mambo mengi sana ya nchi kwa sababu analetewa taarifa xa kijiinterejensia na wanausalama lakini kiongozi hana budi kukaa na ukweli wake moyoni kama hauna faida kwa taifa, hana budi kukaa kimya kama ukweli wake ni wa kibaguzi dhidi ya makundi anayoyaongoza.

Amani na upendo kwanza
Ukweli usio na faida badae

LoveTz
Mkuu Kimbakuli, karibu mtaa huu, hapa nimezungumzia hii hoja yako ya sio lazima kuusema kila ukweli unaousikia.

P.
 
Untill when kama unakiri kuwa Jerusalem ni capital city ya Israel? This has to come to an end, UKWELI usemwe! as long as ni ukweli! watu wauzoee ukweli.
 
Paskali, mwanzoni nilidhani na wewe huwajui "Wasiojulikana" na Wasiojulikana. Lakini nimeacha imani hiyo. Unawajua wote wa aina mbili na ndo maana unakimbilia kukosoa thread yangu badala ya kujikita na maswali niliyouliza.
Mkuu Baija, nchi inaongozwa kama familia, hata wewe ukiwa nyumbani, kama mtoto wa kiume unaejitambua, siku mama yenu amesafiri kwenda kijijini kwao kusalimia, huku nyuma baba akaingiza mgeni, na ukamuona. Kumbe yule mgeni aliacha chumbani kwa baba nguo yeke fulani, bila baba kujua, ama kwa kusahau kwa bahati mbaya ama kwa makusudi ili mwenye nyumba ajue hayuko peke yake.

Mama aliporudi, kukaibuka ugomvi mkubwa kati ya baba na mama kuhusu hiyo nguo imetoka wapi na imeachwa na nani?.

Baba kamwambia mama hamjui mwenye nguo hiyo wala hajui imeingiaje,labda watoto au msichana wa kazi alijichanganya.

Kwa vile wewe uliona picha nzima, jee utamweleza mama ukweli wa ulichoona?.

Hiyo ndio essence ya wasiojulikana hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Kama baba amesema hajui nguo imefikaje, who are you kusema imefikaje?.

Kama yule aliyemshikia Nape bastola naye hajulikani mpaka leo anatafutwa na polisi, what are the chances kuwabaini julikana wa Lissu?.

Wana familia bora, wanamwamini baba mwenye nyumba, hata kama wewe ulimuona mgeni wa baba, lakini hukumshuhudia wakati akiivua hiyo nguo na kuiacha uvunguni mwa kitanda chumbani kwa baba, hivyo kama baba kasema hajui, then it migh be true, baba hajui, na hiyo nguo iliachwa siku nyingi nyuma na mgeni mwingine ambaye hata wewe hukumuona.

Hivyo sio lazima kuusema kila ukweli unaousikia.
P
 
Kanuni ya kimaadili inatutaka kuchagua lililo na madhara kidogo, lesser evil mkuu Paskali. Ukweli hausemwi kila mahali na kila wakati. Ni kanuni hiyo
 
Mkuu Baija, nchi inaongozwa kama familia, hata wewe ukiwa nyumbani, kama mtoto wa kiume unaejitambua, siku mama yenu amesafiri kwenda kijijini kwao kusalimia, huku nyuma baba akaingiza mgeni, na ukamuona. Kumbe yule mgeni aliacha chumbani kwa baba nguo yeke fulani, bila baba kujua, ama kwa kusahau kwa bahati mbaya ama kwa makusudi ili mwenye nyumba ajue hayuko peke yake.

Mama aliporudi, kukaibuka ugomvi mkubwa kati ya baba na mama kuhusu hiyo nguo imetoka wapi na imeachwa na nani?.

Baba kamwambia mama hamjui mwenye nguo hiyo wala hajui imeingiaje,labda watoto au msichana wa kazi alijichanganya.

Kwa vile wewe uliona picha nzima, jee utamweleza mama ukweli wa ulichoona?.

Hiyo ndio essence ya wasiojulikana hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Kama baba amesema hajui nguo imefikaje, who are you kusema imefikaje?.

Kama yule aliyemshikia Nape bastola naye hajulikani mpaka leo anatafutwa na polisi, what are the chances kuwabaini julikana wa Lissu?.

Wana familia bora, wanamwamini baba mwenye nyumba, hata kama wewe ulimuona mgeni wa baba, lakini hukumshuhudia wakati akiivua hiyo nguo na kuiacha uvunguni mwa kitanda chumbani kwa baba, hivyo kama baba kasema hajui, then it migh be true, baba hajui, na hiyo nguo iliachwa siku nyingi nyuma na mgeni mwingine ambaye hata wewe hukumuona.

Hivyo sio lazima kuusema kila ukweli unaousikia.
P
Nimesoma huku nacheka, japo sikuamini sana.
 
Huhitaji kuwaamini binadamu, bali muamini Mungu tuu, kwa sisi binadamu hapa duniani, unachotakiwa sio kuamini bali kuukubali ukweli.
P
 
Mimi Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu ya mwana habari, (cardinal rule ni " tell the truth, no matter what!", hivyo mimi ni mtu mkweli daima, na ni muumini wa ile ahadi ya mwana TANU " Nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko", ila katika kuusema ukweli au kuandika ukweli, nasema na kuandika kwa kutumia responsible journalism kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kujiuliza jee ukweli huu ukisemwa, utajenga, au utabomoa?.
Umeisahau kanuni ya ethical consideration?
 
Kwenye siasa za multipartisim duniani kote, kazi ya the opposition ni kupinga, kuopose kila kitu kinachofanywa na chama tawala hata kiwe ni kitu kizuri namna gani!, that is their right, kupinga, ndio maana wanaitwa wapinzani. Na serikali zote zinazoheshimu demokrasia ya kweli, lazima zikubali kupingwa.
Kwenye hili sio kweli
 
Umeisahau kanuni ya ethical consideration?
Mkuu Zawadini, asante kunikumbusha hili neno, umenirudisha darasani kwenye darasa la journalism, kwamba katika kuusema ukweli, lazima uzingatie ethics za mahali ulipo, huo ukweli utakaousema. lazima uwe ethical, kitu kikiwa unethical, hata kama ni kweli sii lazima ukiseme!.
Asante kunikumbusha.
P
 
Mkuu
Sii kweli kivipi?.
P
Mkuu vyama vya upinzani vipo/vinakuwepo kwa ajili ya kuikumbusha serikali/chama tawala kwa yale serikali ya chama tawala inachokifanya hasa inapokosea. Na kimsingi kinatakiwa/vinatakiwa kupongeza pale inapofanya vyema. Hufanya hivi wakiongojea nao kushika hatamu za serikali. Wenyewe wanaviita government in waiting. sio sahihi kusema vipo kupinga kila kitu. Ikitokea hivyo huenda wakawa wamesahau majukumu yao.
 
Mkuu Baija, nchi inaongozwa kama familia, hata wewe ukiwa nyumbani, kama mtoto wa kiume unaejitambua, siku mama yenu amesafiri kwenda kijijini kwao kusalimia, huku nyuma baba akaingiza mgeni, na ukamuona. Kumbe yule mgeni aliacha chumbani kwa baba nguo yeke fulani, bila baba kujua, ama kwa kusahau kwa bahati mbaya ama kwa makusudi ili mwenye nyumba ajue hayuko peke yake.

Mama aliporudi, kukaibuka ugomvi mkubwa kati ya baba na mama kuhusu hiyo nguo imetoka wapi na imeachwa na nani?.

Baba kamwambia mama hamjui mwenye nguo hiyo wala hajui imeingiaje,labda watoto au msichana wa kazi alijichanganya.

Kwa vile wewe uliona picha nzima, jee utamweleza mama ukweli wa ulichoona?.

Hiyo ndio essence ya wasiojulikana hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Kama baba amesema hajui nguo imefikaje, who are you kusema imefikaje?.

Kama yule aliyemshikia Nape bastola naye hajulikani mpaka leo anatafutwa na polisi, what are the chances kuwabaini julikana wa Lissu?.

Wana familia bora, wanamwamini baba mwenye nyumba, hata kama wewe ulimuona mgeni wa baba, lakini hukumshuhudia wakati akiivua hiyo nguo na kuiacha uvunguni mwa kitanda chumbani kwa baba, hivyo kama baba kasema hajui, then it migh be true, baba hajui, na hiyo nguo iliachwa siku nyingi nyuma na mgeni mwingine ambaye hata wewe hukumuona.

Hivyo sio lazima kuusema kila ukweli unaousikia.
P
We ni kilaza uliebahatika kusoma

I wonder how people can be this stupid !!!!

Mifano ya kitoto haina hata mashiko yani
 
For this thread only umeondoa credibility yako for good

How can people believe in you again kama una advocate uongo ..
 
Mkuu

Mkuu vyama vya upinzani vipo/vinakuwepo kwa ajili ya kuikumbusha serikali/chama tawala kwa yale serikali ya chama tawala inachokifanya hasa inapokosea. Na kimsingi kinatakiwa/vinatakiwa kupongeza pale inapofanya vyema. Hufanya hivi wakiongojea nao kushika hatamu za serikali. Wenyewe wanaviita government in waiting. sio sahihi kusema vipo kupinga kila kitu. Ikitokea hivyo huenda wakawa wamesahau majukumu yao.
Sasa hapa Tanzania hizo waiting govts zinafanya hayo uliyosema au VINASHINIKIZA maoni yao kukubalika?

Na kama ni ivo demokrasia inakuwa wapi sasa. Na je watakuwa tayari na wao kupokea matakwa na mashinikizo ya hyo itayokuwa waiting govt wakati wao??

Na kama ikiwa ivo itakuwa nchi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi au kupinduana kila uchao??
 
Unajipendekeza sana..mkuu..
Kazana tuu utapata udc na ras...
Eti "polisi wanajipendekeza..."....unajipinguza uweledi wako kwa makusudi kabisa.. kujua upana wa mamlaka ya chama tawala na utendaji wa polisi..
 
Back
Top Bottom