Acha zako wewe,we funga kilokole🤣🤣🤣kwaresma haiwahusu nyie walokole.Mnaumizwa Sana na wakatoliki,ilhal wakatoliki hatuna time na nyie watoto wa kambo,mlojitenga,kina ishmael
shida ni kwamba, tunawaonea huruma,mmepotea, tunajaribu kuwarudisha, kwasababu kanisa hilo mlilonalo silo lile la mitume, kanisa la mitume mfano wake ni vile ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume, nakupa homework kasome kitabu icho mwanzo hadi mwisho. utagundua yafuatayo:
1. Kanisa la kwanza lilisimama kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu, na lazima ujazwe Roho baada ya kuamini.
Matendo 19: 2 aka wauliza, “Mlipoamini mlipokea Roho Mtakatifu?” Wakajibu, “Hapana. Hatujawahi hata kusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” 3 Ndipo Paulo akawauliza, “Mlibatizwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Ubatizo wa Yohana.” 4 Paulo akasema, “Yohana alipobatiza, aliwaambia watu watubu dhambi na kumwamini atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” 5 Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Yesu. 6 Na Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia , wakasema kwa lugha mpya na kutabiri. 7 Walikuwepo kama watu kumi na wawili.
2. Kanisa la Mitume hawajawahi kuomba kwa kupitia Maria wala kumwinua kwa namna yeyote, ni mtu wa kwaida tu. soma Matendo yote hutakuta icho kitu.
3. Kanisa la kwanza, waliamini katika kuokoka, lazima umkiri Yesu na uokoke, la kwenu linafukuza wanaookoka.
4. Kanisa la kwanza liliamini watu wanene kwa lugha, lakwenu mnasema ni mapepo.
5. kanisa la kwanza haliamini katika kuombewa ukifa ili usamehewe, unasamehewa kama ukitubu ukiwa hai, baada ya kifo ni hukumu. ninyi mnaombea wafu, mnaomba kwa kupitia wafu, mnaamini wafu wapo sehemu fulani watapeleka maombi yenu kwa Mungu.
6. Kanisa la kwanza, kama Yesu mwenyewe alivyosema, Ombeni kwa Jina langu, nanyi mtapokea, ninyi mnaomba kwa maria, na wafu wengine hadi ndugu zenu. hakuna njia nyingine ya kumfikia Mungu iwe katika maombi au chochote ila kwa njia ya Yesu Kristo pekee.
7. Maria mwenyewe, kwasababu aliuwepo miongoni mwa wale 120 waliompokea Roho Mtakatifu pale upper room siku ya pentecoste, aliamini watu wanatakiwa waokoke na alishirikiana na mitume kuhubiri ili watu waokoke, ninyi mnapinga wokovu na hata wale wanaookokea kwenu mnafukuza (karismatic).
sasa mnafunga nini? wakati hamjaokoka? hamna Mungu? imani yenu imeshikiliwa na vatican ambaye ni ishara mojawapo ya mpinga Kristo tangu zamani, na kwa sasa imeanza kuchipua kuonyesha makucha yote kwa kuruhusu ushoga. Mungu awasaidie. siku ukiondoka huko, utaona kwanini umepoteza muda miaka yote hiyo. kama neema ya Mungu utafanikiwa kabla hujafa, nakuombea kwa Mungu upate neema.
watu wengi mnapinga wokovu na njia iliyo sahihi, ila kwa mtu mwenye akili timamu, ukiona watu wanaokoka na maisha yanabadilika, jiulize kuna nini huko hadi watu wabadilike? jaribu kuokoka, ukiona wokovu mbaya acha. Biblia inasema Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema, heri mtu yule anayemtumaini Bwana. Mjaribu Mungu kwa kuokoka uone kama kuna tofauti au walokole waongo. ila sio lazima, usipookoka ni hasara yako, ila kabla hujaondoka hapa duniani jaribu hata mara moja tu usije enda uendako ukaenda kukuta ulikuwa umepotea tulikushauri uje kwenye njia sahihi ukagoma na muda umepita hakuna kurudi nyuma.