Swali: Ni kitu gani kwenye mwili kikipimwa huwa kinathibitisha mtu kufariki?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Habari wadau,

Mambo ya kifo wakati mwingine huwa yanafanyika haraka haraka sana hadi huwa najiuliza, ili mtu athibitike kuwa kafariki dunia, ni sehemu gani ya mwili hupimwa? Maana huko mochwari wakati mwingine huwa kuna watu wanakohoa au kuzinduka lakini shida ni pale daktari anakuwa tayari kashasaini "Dead body" kumbe mtu anakuwa yupo kwenye koma au kuzimia.

Tena baadhi ya tetesi zinasadikika kwamba ikitokea mtu maiti ikazinduka ili kunusuru skendo inaweza nyongelewa mbali au kupigwa rungu la kichwa ili ifilie mbali. Swali, kipimo gani hutumika kuthibitisha kifo?

Pia je ikitokea maiti imezinduka huko mochwari, wafanyakazi wa mochwari wana elimu yeyote ya kuokoa?

Maana huwa sielewi mfanyakazi wa mochwari anashika rungu mkononi la nini? Maana story za mtaani nasikia mochwari maiti ikikohoa humaliziwa.

Mwenye kujua atuelimishe.

===
Baadhi ya majibu
 
Mtu kufariki kunapimwa kuangalia muitikio wa ubongo, hapa unaangalia mboni za jicho ikiwa hazipungui au kuongezeka kutokana na mwanga basi ubongo wa huyo mtu umeshakufa na hatoamka.

Unaweza sikiliza mapigo ya moyo, pumzi kifuani lakini ubongo ndo uhakika zaidi maana moyo waweza simama pumzi zikasimama ila kama ubongo still u hai basi moyo na kifua hushtuliwa na maisha yanaendelea
 
Kwa kawaida ubongo huwa unachukua dakika 4 mpaka 5 kufa na sio zaidi ya hapo. Moyo unaweza ukasimama ghafla lakini ubongo huwa unakufa taratibu na baada ya dakika tano tokea mapigo ya moyo yanaposimama ubongo huwa umeshakufa na hapo mtu anakuwa marehemu rasmi.

Ikiwa kama moyo uliosimama unaweza kuamshwa tena ndani ya dakika hizo nne, basi mtu huyo anaweza kuendelea kuishi. Wengi wa waliopitia hali hii wamekuwa wakisema kwa kipindi chote ambacho mapigo ya moyo yalipokuwa yamesimama, walikuwa wanaona kitu kama mwanga hivi na wengine wanasema walikuwa wanawaona madaktari jinsi wanavyohangaika kuwaamsha.

Hivyo basi kitaalamu, ubongo unapokufa na mtu naye anakuwa amekufa rasmi.
 
Kifo kinapotokea hospitalini ni lazima Daktari aliyeko zamu aweze kuthibitisha kwa kufanya uchunguzi kabla ya kutangaza kifo kwa ndugu wa karibu. Hata kama wauguzi au ndugu wa karibu wakihisi kwamba mtu kaishafariki, hairuhusiwi kuondoa maiti kuipeleka chumba cha maiti kabla wataalamu hawa wawili kwa maana ya madaktari na manesi hawajamaliza taratibu muhimu kabla ya kutoka amri ya kupelekwa chumba cha maiti.

Taratibu za kuuchunguza mwili kwa makini kama mtu bado anapumua hufanywa na Daktari kwa dakika zisizopungua tano, kwa kuangalia uso,pua na kifua. Hatua inayofuata ni kupapasa mapigo ya moyo kwenye mkono kama yapo, kusikiliza mapigo ya moyo kwa kutumia kifaa cha kusikilizia moyo na mapafu na hatimaye kupiga tochi machoni kujihakikishia kama macho yanatoa dalili za uhai baada ya kupigwa na mwanga mkali.

Baada ya kumaliza uchunguzi wa Daktari zinafuata taratibu za kiuguzi za kumtayarisha marehemu kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti na hapa inatakiwa yapite masaa kati ya manne au sita tangu kutangazwa kifo ndipo maiti ipelekwe chumba cha maiti au wakabidhiwe ndugu wa marehemu.

Kwa kawaida moyo ukisimama kufanya kazi yake kuna dakika tano tu za kujaribu kupambana ili kuokoa maisha ya mtu vinginevyo baada ya dakika tano seli za ubongo hufa. Ukisikia mtu eti ameonyesha dalili za kuwa hai baada ya kufika chumba cha maiti basi ujue taratibu hazikufuatwa ili kujihakikishia kama kweli mtu amekwisha kufa. Isitoshe kuna mashine zinazounganishwa kwenye mwili wa binadamu ili kukusanya taarifa za mwenendo wa mgonjwa, kifo kikitokea zinaonyesha kabisa kuwa baadhi ya viungo havifanyi kazi tena.
 
Mtu kufariki kunapimwa kuangalia muitikio wa ubongo, hapa unaangalia mboni za jicho ikiwa hazipungui au kuongezeka kutokana na mwanga basi ubongo wa huyo mtu umeshakufa na hatoamka
Hebu fafanua mkuu, mboni za jicho hazipungui na kuongezeka kutokana na mwanga ndiyo nini?
 
Ubongo unatabia ya kuendelea kuwa hai na kuProcess vitu kwa muda fulani baada ya mtu kufa.

Ni MOYO pekee ambao unakuwa unahitaji kiasi cha umeme ili uweze kusukuma damu pande zote ktk mwili, kwahiyo ni kupima PULSE ambayo unaweza kuipima manually kwa kushika mishipa ya damu inayoonekana hasa kwenye mkono kwenye kiganja kwa juu au kwenye mishipa iliyopo shingoni na kuhisi kama DAMU inaflow.
 
Kuna criteria mbili kiu za kumtangaza mtu kwamba amekufa
1. Moyo ukisimama hata baada ya jitihada za kuufanya ufanye kazi kufanyika.
2. Irreversible brain death..

Hizo criteria mtu akizifikia basi hapo kitabibu watasema ame expire.

Hapo kikubwa ni brain maana moyo unaweza kuwa unafanya kazi kwa sababu ya mashine za hospitali lakini kama brain imekufa hapo hakuna kitu.
 
Kuna dawa moja yakisunna anapakwa kwenye pua, hiyo dawa kama upo hai baas unapiga chafya na kama umekufa haupigi chafya

Ndio maana waislam tunatakiwa baada ya kupiga chafya tuseme Alhamdulillah (ikiwa na maana ya kumshukuru mungu Kwa uhai) na hats Saydna Adam baada ya kupuliziwa upepo akapiga chafya na gibril akaitikia "yahamkallah"
 
Hatua ya kwanza kabisa huwa tunaangalia pulse rate (mapigo) ya mkononi/ sehemu iliyonganisha kiganja na mkono,
Hatua ya pili tunaangalia maeneo ya shingo kwenye tonsel, pia napo kuna mshipa huwa unapiga.

Hatua ya tatu huwa tunaangalia macho kama rangi imebadilika kutoka kwenye hali ya kawaida kwenda Gray colour,

Njia ya nne mapigo ya moyo, ambayo ni mara chache sana kugundua kupitia mapigo ya moyo, kwa sababu moyo unaweza kuwa unaenda kwa pulse rate ya 10, na ukasema mtu amekufa kumbe bado yupo hai.
 
dmkali,

Google na kujisomea Brain stem reflexes, legal death, vegetative state utapata uelewa mpana. Story za mochwari kupiga maiti Rungu ni chai za kitaa. Kila mmoja husema nilisikia. Issue za maiti kujitingisha sijui kukunja mikono google kitu kinaitwa Lazarus sign au Lazarus reflex. Soma utajipatia maarifa zaidi. Hospital huwa hawapeleki MTU mortuary msobe msobe.

Wakihisi umekata au unataka kukata nurse atapambana huku akiita doctor, efforts zikifail, hawasemi umekufa that very moment. Wanauchuna kidogo wakikusikilizia, wanajaribu Ku activate hizo brain stem reflexes, if non the watadocument kuwa umekata, Ila MTU wa mortuary watabuy time kidogo kumwita, then watafunga mwili na kumwita msela wa mortuary.

Hayo mambo huchukua muda wa kutosha, hivyo hayo ya kupeleka mortuary walio hai au kuzika walio hai ni story za kuchangamsha genge. Ikitokea labda wanaoletwa direct kutoka nje wakisema ni ajali au majambazi na report inasema kwamba washakufa , mazingira hayo kabda labda labda labda yanawezekana. But rare
 
Mboni ya jicho hugeuka na kuelekea juu tofauti na kawaida
 
Swali zuri nami nimejifunza kutokana na kometi hizi
 
Ooooh kumbe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…