Swali: Ni kitu gani kwenye mwili kikipimwa huwa kinathibitisha mtu kufariki?

Inakuaje kwa mtoto mwenye degedege....naskia hua nao wanakodoa macho mwanzo mwisho na pupil haiwi responsive, je ni kwel? Na unazungumziaje sasa hyo test?
Kukodoa macho ni tofauti na hii ya kiini cha jicho kurespond unapomulika na mwanga.
Ukimmulika na torch pupil zitarespond to light.
Sasa fanya kufuatilia uone hao watt wenye dege dege mkuu wanasemaga ya kuambiwa changanya na yako.
Nadhan umenipata?
 
Na baada ya ajali kutaka kujua damage ya brain ni kuinua miguu. Kama mgonjwa anaweza kuinua mgumu wa kulia according to command na wa kushoto, juchezesha vidole vya mguu akiwa amelala unajua ubongo bado uko alright
Verbal response.
Check out Glasgow coma score
 
mtu kufariki kunapimwa kuangalia muitikio wa ubongo, hapa unaangalia mboni za jicho ikiwa hazipungui au kuongezeka kutokana na mwanga basi ubongo wa huyo mtu umeshakufa na hatoamka,
Hapa sijakuekewa vizuri hasa upande wa macho, kupungua na kuongezeka ndo inakuwaje hasa?
 
Kuna makala nilisoma zamani kidogo inasemekana kuwa katika nchi nyingi za kimaskini watu wengi wanazikwa wakiwa hai. Kutokana na uduni wa vifaa na wakati mwingine uhaba na ezembe wa wataalamu basi mtu anaeeza kuwa kwenye coma ila akatangazwa kuwa kafa. Wahudumu wa afya wanacheki pulses tuu trna manually wasipozipata wanasema mtu kafa kumbe wakati mwingine mtu huyo hajafa bado.. Mnakumbuka yile mchezaji mpira aliyeangukaga uwanjani akazimia (akawa in a state of death) kwa masaa 72? Basi yule angekuwa nchi zetu hizi ageshafukiwa aisee
 
Hiyo dawa inapatikana wap shekh, je inaruhusiwa mahospitalini?
 
GwaB,
Umefafanua Kwa kina lakini, je vipi maiti inapozinduka mochwari hatua gan hufanywa au ndipo rungu hutembea kuondoa ushahidi?
 
Hizo CPR zipo mahosipitali yote?
 
Mshana Jr,
Kuna story ilitokea huko Mwanza mwaka Jana, kuna dogo anadai alipoingizwa kwenye jokovu ule ubaridi ulipompiga akazinduka
 
Kabisa mkuu
 
Hapa sijakuekewa vizuri hasa upande wa macho, kupungua na kuongezeka ndo inakuwaje hasa?

Mboni za mtu hai huwa zinatanuka kunapokuwa na mwanga hafifu na kupungua kunapokuwa na mwanga mkali.

Leo usiku tafuta kioo na tochi. jiangalie ukubwa wa mboni ukiwa sebuleni penye mwanga wa kawaida na rekodi.

Kisha zima taa ya sebuleni kwa sekunde kama kumi, washa tochi na jimulike machoni huku ukijiangalia na kioo. Hapo utaziona live mboni zako jinsi zilivyo kubwa kutokana na mwanga hafifu wa sebuleni na sasa zitapungua haraka kwa sababu mwanga wa tochi umeongezeka. Kitendo hiki utakiona mwenyewe na kitachukukua sekunde moja au pungufu.
 
Sio kweli...hizo propaganda za nchi za magharibi za kufanya tujione inferior..

Lakini ki ukweli kuna vifo vinatokea ambavyo vinaweza kuzuilika lakini kutokana na ukosefu wa vifaa na uhaba wa wafanyakazi watu wanakufa..
Lakini sio kuwa watu wanazikwa wazima
 
inawezekana watu wengi wamezikwa wakiwa wazima, maana sisi huku vijijini tunapima mapigo ya moyo kwa kuweka kiganja kifuani tusiposikia mapigo yoyote basi wewe umeshazima - ni kuchimba kaburi sanda fastaa ili usilale ndani.
 
Niamini mimi Watanzania(Africa) wengi wanafia mochwari.
 
Daktari wetu wazembe ilikuwaje haraka haraka hivyo wakifunike badala wakipatie o2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…