Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?


Kikwete ameliingiza taifa kwenye machafuko na chuki ya kibaguzi kwa majirani bila sababu za msingi.
Heshima ya Tanzania imezikwa na Kikwete.
 
 
jibu ni kwamba hakukua na wahamiaji haramu kipindi hicho,kama walikuwepo hawakufika hata kumi so hawangeweza kuwa tishio.wapinzani wa idd amini wengi walikuwa wamekimbilia Tanzania akiwamo obote,hao hawakuwa tishio kwa usalama.

Wanyaru wa sasa wanatishia amani huko mikoa ya pembezoni.
 
Mpaka sasa iko tofauti ya tafsiri ktk tamko la JK; tafsiri moja kubwa na maarufu ni kuwafukuza "Wanyarandwa" na sio "Wageni waishio nchini isivyo halali".

Kuna uwezekano wa hisia (hasira nk) ktk hilo tangazo, au kilicho nyuma ya pazia ndicho kinachotekelzwa. Ila kwa namna nilivyosoma lile tamko la Rais Kikwete lilikuwa "too general" kuliko "application" ninayoiona. Na hapa ndipo napojikita kwa maswali ili nipate majibu.

Ningependa kuona tafsiri na utendaji mpana wa sheria kila siku/mahali (na sio kusubiri tamko la Rais); lile tamko lilipaswa tu kuwapa watendaji some moral support etc
 


  1. Mimi nadhani hujamwelewa MMM, mleta hoja. Alichokileta Mwanakijiji ni HOJA FIKIRISHI na kwa kweli kwa watu wanaofikiri vizuri, akiaamua kujielekeza kujibu hoja,basi ataijibu kwa HOJA!!
  2. Hapo katika BOLD GREEN, unachobishia ni nini Mkuu??...Si amri ya JK imetoka baada ya hawa wakuu wawili wa mataifa huru kuanza kurushiana maneno??...Na hivi ni kweli kabisa kuwa kila palipo na uhalifu ni kwa sababu ya wahamiaji haramu?...Watanzania sisi wenyewe miongoni mwetu hakuna wahalifu??
  3. Sidhani kama MMM anataka kujustify lolote lenye chuki kama ulivyomaliza hoja yako kwa kuwalinganisha JMK na JKN zaidi tu ya kwamba Nyerere aliwahi kuwa kiongozi wa taifa hili (Rais) kwa takribani miaka 25 na huyu Kikwete ndiye Rais wetu wa sasa. Aidha wakati wa Nyerere kulitokea mfarakano uliosababisha vita kati yetu na majirani zetu Uganda. Na sasa kwa namna huyu Rais wetu JK anavyoshughulikia mgogoro wake na mwenzie wa Rwanda PK kuna kila dalili kuwa anaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi tofauti na kinyume kabisa na namna ambavyo yeye mwenyewe binafsi na washauri wake pale Magogoni wanavyofikiri!!....Kwa hiyo ni haki na ni lazima wajadiliwe kwa sasa na walinganishwe kwa namna wanavyotenda kama viongozi wetu

Mwisho hakuna anayekubaliana na tatizo la watu wa mataifa mengine kuingia nchini kwetu pasipo kufuata sheria hata kama tunawaita WAHAMIAJI HARAMU. Ishu ni moja, kwamba, tunatumia njia gani kushughulika na mtu/watu wa namna hii mara tunampowatambua wamo nchini mwetu isivyo halali hata kama pia watakuwa wametumia udhaifu wa mifumo yetu ya utendaji?? Je ni hivi inavyofanya serikali yetu? Na je, watanzania wenzetu walioko katika mataifa mengine kwa njia hizihizi nao watendewe hivihivi au??......Hebu Rejea tena kwenye Katiba yetu inasemaje juu UTU na UBINADAMU na angalia pia maisha ya watu wa mipakani jinsi yalivyo.....hapa naamanisha muingiliano kwa sbb nchi hazina mipaka ya ukuta na idara zetu za uhamiaji haziwezi kuweka ofisi ktk kila njia ya mpakani. Hapa Rais na serikali imechemka si ktk nia yake tu bali pia ktk mfumo wa utekelezaji wenyewe wa agizo la Rais!!

Let us think deeply kwa kuweka itikadi zetu za vyama pembeni na kila mtu atoe mchango wake bila kumuonea mtu. Binafsi nampongeza MMM ameleta hoja hii kwa wakati mwafaka na serikali wakifikiri vizuri inaweza kuwasaidia kutenda vizuri zaidi katika kushughulikia tatizo la "wahamiaji haramu" na bado ikawa na heshima yake ileile nzuri mbele ya uso wa kimataifa!!
 
Ni vyema wachangiaji wakalinganisha mifumo mbalimbali ilivyokabiliana na swala la wahamiaji haramu....ili kutanua uwigo wa kujadili hoja hii.
Case studies:
David Cameron vs wahamiaji haramu
USA/Obama na sera za uhamiaji haramu
South Afrika na sekeseke la vipigo dhidi ya wahamiaji kutoka zimbabwe n.k

Tusimshambulie mleta hoja bali tujadili hoja.
 
naamini mwanakijiji anaishi marekani kama mhamiaji haramu na hana any legal documents zakumfanya aishi huko!! kwa maana kama anaelewa athari za wahamiaji haramu asingeongea huu utumbo aliouandika, ulaya nzima kwa sasa kampeni za kisiasa hutawaliwa na ishu ya kuhandle wahamiaji haramu, uingereza, ufaransa,italy,spain,sweden nakadhalika kote huku wahamiaji haramu wanawekwa maeneo maalum wanachunguzwa sababu za uhamiaji wao na kama hawakidhi vigezo wanakuwa deported back to their countries!!

tuseme haya mwanakijiji hayafahamu? au kujitia hamnazo tu ili apate sababu ya kupinga serikali? hana tofauti na Dr Slaa kwamba yeye kila kitu cha serikali basi ni kupinga tuuu, hizi ni akili za kawaida au akili za kukariri? wana tofauti gani basi hawa na wabunge wa CCM ambao hupinga kila mchango wa mbunge wa upinzani?

unafiki ni janga kubwa tulilonalo Tanzania, na kama hakuna uzalendo wa dhati basi hatuna chetu tena
 
Hivi kwa nini mtu ukipinga huu mgogoro unaitwa Mnyarwanda? Jana mie Mnyamwezi nimeitwa MTUSI na mjinga fulani.

Wewe leo unamwita Mwanakijiji Mnyarwanda wakati wengi tunafahamu Baba yake alikuwa nani na Mama yake ni Msukuma.

Kama huna la kuandika si ukae kimya kuliko kuropoka? Mzee Mwanakijiji anafahamika kabisa kuwa Mtanzania na sehemu anayotoka, ungelionekana walau una akili kidogoo ukamwita Mmalawi au Mzambia. Sasa utamwita hata Mbowe kuwa Mnyarwanda. Mchaga na Mtusi wapi na wapi?
Mwanakijiji na unyarwanda wako pamoja na pasi ya Tanzania unayo2mia haukufanyi kudhihaki maamuzi ya nchi ye2
 
ukishasema wahamiaji haramu hauna haja ya kuuliza kama mi halali kuwachukulia hatua au la. Jk angekuwa amewafukuza waamiaji halali hapo tungehoji.
 

Unasema mwenyewe "Ni kweli malalamiko ya wenyeji yalianza siku nyingi."

Bila shaka tumepata sababu nzuri ya kuanza kuyashughulikia wakati huu. Ilikuwa ni lazima ifike muda fulani hatua zichukuliwe. Kama wanavyosema - sooner or later.

Wala haijasemwa wasije Tanzania. Wafuate taratibu zilizowekwa. Rwanda wapo Wa Tanzania wengi mpaka kwenye vyuo vayo wanategemewa. Hao wote wamefuata taratibu za kwenda huko.

Inaniuma sana kuwahangaisha jamaa zetu wamasai na wasukuma na mifugo. Wamefukuzwa Kilombero. Badala ya Wanyarwanda kuchunga mifugo yao Bongo, bora ndugu zetu waende huko. Mwisho wa siku mifugo hiyo inanifaisha uchumi wa Tanzania. Wanyarwanda hapa kwetu wanalisha tu, hatimaye wanaenda nayo kwao.
 


If it takes a decade for a government to find what to do then to hell with it. Na kwa nini siyo wahamiaji wote waliojazana nchini? Why ni Kagera tu? Hao wanaobaki wana uhalali gani? Na bado huajibu swali: Walipkuwa wanaingia Serikali ilikuwa wapi?

Hakuna alipendekeza waendelee kukaa siyo Mwanakijiji wala mimi sijasema hivyo. Nilichosema ni utaratibu unaotumika unawanyanyasa utu wao na ni uvunjaji wa haki ya kuthaminiwa utu wao na usawa kisheria.

Jaribu kurudia kusoma posti ya Mwanakijiji , rudia na yangu...then karibu tena.
 
Dar es salaam hakuna wahamiaji haramu ambao ni wahalifu pia ? arusha je? Au Mwanza hakuna wahamiaji haramu ? Kwanini agizo hili linahusu Kagera tu? Isn't that selective justice?
 
Mwanakijiji angeongeza kuwa ethnic cleansing anayoifanya Kikwete ni crime against humanity. Pia ku-destroy uchumi wa watu na kuwabakiza wakiwa masikini. Mhamiaji ana mifugi yake, ndo kila kitu, hana elimu, hajui bishara, hajui kulima, then unakuja unampa wiki mbili eti arudishe mifugo alikoitoa. Hajui kuwa hawa wafugaji hawajatoka kokote, ila wana asili tu ya Rwanda na Uganda, ila ni wa hapahapa. Unawafanya wauze ngome 1 kwa shs 20,00, ubinadamu huo? Hivi Kikwete si mwislamu?
 
Apology not accepted.

Sheria za uhamiaji zipo wazi, askari uhamiaji wameshindwa kulinda mpaka ipasavyo.

Kuhusu relationships mipakani, hebu acha kutupotosha, hata geitra nako??, mpaka mwanajeshi wa JWTZ auliwe ziwa tanganyika? .. usitake kutuongopea, you know this is a very peculiar case of border crossing and need to be handled as soon as possible.


Hakuna sheria inayosemaa eti tuongee na nchi wanakotoka kwanza. Wamepewa ultimatum, which is a very diplomatic way of deportation.

Usitumie mfano wa Masongange, that is stupid!! Tanzanians have automatic visas in SA, and when you break the law, you have the right to a due process/fair trial.

They should be arrested after the deadline. Tats just the law!!

But they should not be treated violently.
 
adolay,

..naomba kutofautiana kidogo na wewe.

..Kagera kuna tatizo la ujambazi. Raisi ametoa wiki 2 kwa MAJAMBAZI kusalimisha silaha zao.

..Kagera kuna tatizo la walioingiza mifugo ktk maeneo yasiyostahili kama hifadhi za taifa. Hao pia wamepewa wiki 2 watoe mifugo yao.

..Kagera kuna tatizo la wahamiaji toka nchi jirani. Raisi kawapa wiki 2 waweke mambo yao sawa, au warudi nchi walikotoka.

..hivi Raisi anayebembeleza mpaka majambazi anapaswa kuitwa dikteta kweli? kuwapa muda watu waliovunja sheria waziwazi ni udikteta?

..Raisi amechukua maamuzi hayo baada ya kusikia malalamiko toka kwa wananchi wa Kagera. Nakushauri usome au usikilize hotuba ya Raisi.

..In 2010, Kikwete akiwa ndiyo Raisi wetu, Tanzania iliwapa uraia wakimbizi 160,000 toka Burundi. Sasa madai kwamba Kikwete ni mkatili na dikteta yanatoka wapi?

..Mwisho, natofautiana na Raisi Kikwete ktk masuala chungu nzima, lakini katika hili nakubaliana na hatua alizochukua.

cc Sikonge, Ogah
 
Last edited by a moderator:
Dar es salaam hakuna wahamiaji haramu ambao ni wahalifu pia ? arusha je? Au Mwanza hakuna wahamiaji haramu ? Kwanini agizo hili linahusu Kagera tu? Isn't that selective justice?
baada ya siku 14 kuna msako utaanza,bila shaka utahusisha maeneo ya Upanga kwa wahindi na kinondoni kwa wakongo!
 
Dar es salaam hakuna wahamiaji haramu ambao ni wahalifu pia ? arusha je? Au Mwanza hakuna wahamiaji haramu ? Kwanini agizo hili linahusu Kagera tu? Isn't that selective justice?

We nawe akili zako kama kichwa cha panzi.

Swali lako hili ni sawa na mtu aulize kwanini mradi wa maji uko Karatu kwani Dodoma hakuna shida ya maji.

Au mtu aulize kwanini barabara inajengwa Songea kwani Singida hakuna shida ya barabara.

Umeshawahi kusikia Dar es Salaam kuna mtu kashindwa kufanya shughuli zake kwa sababu ya wahamiaji haramu? Hujui Tanzania ilivyo, kazi yako kusambaza chuki tu...

Chuki inakupeleka kubaya sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…