Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?


Kuna mtu anataka kutubugiza HOJA! Hoja ile ile inarudiwa kwa vichwa mbalimbali na mashambulizi kutoka kona mpya kila leo! Lakini msimamo wetu unabaki wazi:
"JAPO DR.KIKWETE ANA MAPUNGUFU YAKE, HAMKARIBII NYERERE HATA KIDOGO KWA BUSARA NA KUJENGA HOJA, LAKINI KWA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WAHAMIAJI HARAMU 'HATARI', TUTAMUUNGA MKONO MPAKA DAKIKA YA MWISHO! NA TUNAANZA NA WALE WA MAZIWA MAKUU, AMBAO PAMOJA NA HUJUMA ZAO DHIDI YA UCHUMI WETU (KWA MASAFA MAFUPI NA MAREFU), WENGINE NI RAIA WA NCHI ZINAZOLETA 'KILIMILIMI' KANA KWAMBA TANZANIA NI KOLONI LAO!
KWA KIFUPI: HAWA WATU WARUDI KWAO MAPEMA, WAENDE KWENYE NCHI YAO YA 'MAZIWA NA ASALI, IF BLOOD AND PUSS QUALIFY!', WATUACHE NA BONGO YETU YENYE 'BAJETI TEGEMEZI KWA 40%?' (Rafiki yao mmoja kaanza kunya kwa domo lake!)
 


Sasa kama unajua Uhamiaji na wenzao hawakufanya kazi zao unalalamikia kipi? Kwanini walipokuwa wanaingia hawakuelekezwa hayo matakwa ya sheria? So kama wakati wanaingia ilikuwa sawa leo kipi kimejiri?

Halafu Kobello, na hawa wa hapa Dar na Arusha ambao hata siyo Wanyarwanda wanatakiwa waendelee kukaa siyo? Au ni kwa vile wao Marais wao hawajagombana na Rais wetu?

Matakwa ya sheria? hakuna inayosema waongee na nchi jirani! But unajua lolote juu ya kitu kinachoitwa diplomacy na faida zake japo kidogo? Umewahi kufikiria ni kwa nini nchi zinakuwa na mikataba ya kubadilishana wahalifu? Kwa nini hatuwafukuzi tu? Kwa nini tunawakabidhi mipakani au kwenye ofisi za ubalozi? Labda naku overdose kwani wewe umesoma mpaka wapi? Nahisi kama hunielewi hata nilikuwa nasema kipi na kipi sijasema.

Mahusiano ya mipakani? you have no Idea na ni vipi watu wanaishi huko. Nakushauri tafuta watu wa mipakani. Wao watakwambia wanaishije. By the way nilipokuwa mtoto hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako. Lakini kusafiri na kuishi maeneo mengi kunafundisha mengi.

Na kuhusu mifano ya kina Masogange nimeuliza unadhani SA ingeamua kuwabeba na kuwabwaga mpakani kimya kimya ingeleta muonekano upi diplomatically? Sikusema hawaruhusiwi kushitakiwa SA au Walitumia VISA na Passport gani!

Nadhani hata hujaelewa nilikuwa nasema kipi na ni kipi sijasema in the whole post. Nakushauri rudia kusoma, elewa nilichosema, halafu lete hoja upya. Hiyo ya sasa umekoroga mambo too much!
 
ZeMarcopolo,

..nadhani Mzee Mwanakijiji analinganisha apples and oranges hapa.

..kujibu swali la Mwanakijiji ni kwamba Mwalimu aliwapa SILAHA na MAFUNZO YA KIJESHI wakimbizi toka Uganda.

..sasa sijui kama mtoa mada anataka tuchukue hatua kama hizo baada ya Kagame kuanza kufurumusha matusi na kutishia kumdhuru Raisi wetu.

cc Kobello, Nguruvi3, Ogah, Jasusi,
 
Last edited by a moderator:
Kwa hili mbona Kikwete kaweka clear sana ni "WAHAMIAJI WOTE HARAMU WARUDI WALIPOTOKA"
Sasa kama kuna gazeti ama mtu anataka kubadili na kusema ni WARWANDA Pekee hatuwezi kumzuia..Hivi wale watu ambao boti zao huzamishwa wanapozamia Australia mbona hamsemi kuhusu Haki za Binadamu?
Yani mtu aingie ndani kwako kinyemela,Kistarabu kabisa una mpa muda wa kuondoka na Bado alalamike atake kuingia na chumbani? Tena wamshukuru Kikwete kwa uungwana aliouonyesha wa kuwavumulia muda wote huo waliokuwa wakikaa kinyemela...Ningekuwa Mimi hizo ng'ombe ningezitaifisha ili liwe funzo wasirudi tena...
Hatuwezi kuvumilia kuporwa na kuvuliwa nguo tunaposafiri ndani ya nchi yetu....Huruma ikizidi huponza....
Pia hata kama wamewekeza na kumiliki maelfu ya mifugo hilo haliondoi kosa Lao la kuishi nchini kinyume cha taratibu....walitakiwa wajue toka mwanzo kuwa wapo kinyume cha taratibu nchini.
HATUA ZISIPOCHUKULIWA TUNALALAMIKA ZIKICHUKULIWA TUNALALAMIKA..
 
Enyi watanzania mliojaa unafiki miyoni mwenu na kujiita watu wa amani mbona matendo na maneno yenu yanawasuta.

1.Rais kikwete aliwahi kusema anawajua wauza unga kwa majina lakini hakuwataja wala kuwachukulia hatua.matokeo yake tumeona vijana kama kina Langa,Ngwea na Ray C wakiangamia kwa sembe

2.Rais kikwete aliwajua mafisadi walionyakua vitita vya mabilioni ya shilingi lakini aliwasamehe na kuwaomba warejeshe.
3.Serikali ya rais kikwete imeshuhudia matukio ya kikatili kama kuteswa kwa Dr Ulimboka,Kibanda.kupigwa mabomu kwenye mikutano ya kidini na mauaji kadhaa bila kuchukua hatua stahiki za udhibiti.
4.Serikali hiyo hiyo ya JK imeshindwa kutimiza ahadi ilizoahidi kwa wananchi na badala yake kuyafanya maisha kuwa magumu zaidi.

Leo hii ukiniambia kuondoa wahamiaji haramu walioko kagera ndio priority hasa baada ya msigano kati yake na kagame nitakuona u-mnafiki wa kutupwa.

Jambo hili halitasukuma maendeleo ya kiuchumi ukilinganisha na mambo niliyoyataja hapo juu,sanasana litazorotesha uchumi na uhusiano wetu wa kidiplomasia.

TUSIWE WANAFIKI!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naomba ufafanuzi, hivi wahamiaji haramu Tanzania ni wanyarwanda tu?
Mbona sijasikia wakenya kule Namanga wakikemewa?, Kule mtwara wahamiaji toka msumbiji je?, Wazambia waliojazana tunduma mbona hawaambiwi kurudi makwao?
Na, kwa nini wakati huu tu baada ya kukosana na Kagame?
 
Nimeuelewa upotoshaji wako sana!

On top of that, nimeelewa kutoelewa kwako. Hivi wew umeniona nikilalamika katika uzi huu?? Nimelalamika wapi?

Jamani, kwa akili yako unafikiri asilimia ngapi ya border crossings btn neighbors ipo recorded? Mbona kuna magulio mengi tu mipakani na watu wanafanya biashara kama kawaida?

Ila ukileta ming'ombe yako na kuanza kumiliki ardhi kinguvu, hapo utakuwa unachochea kuchinjwa. Yaani uingie kwa watu na kuanza kufuga ming'ombe yako mpaka kwenye mapori yaliyohifadhiwa?? m... thats too much pushing!!!

Unaweza ukasema watutsi wamekuwa targeted, thats okay kwa sababu, life style ya wafugaji inahitaji, na ina degrade ardhi, na unfortunately kwenye hili, watusi ni wafugaji na style yao ya ufugaji ni ya kizamani na inabidi ibadilishwe. Otherwise their survival will be affected.

Usitetee uharamia!!!

NB:Wewe sidhani kama unaweza kunioverdose kwenye infos zozote, nilisoma na kumaliza "Ant-duhring" by Friedrich Engels nikiwa form two. Na hapa nilipo karibu namalizia page kumi za mwisho za "Consciescism" by Kwame Nkrumah. Hiyo ni hobby tu.
Credentials zangu, siyo kivile ila ni above normal na sizungumzii population ya Tanzania .... so please don't go there.
 
Kikwete ameliingiza taifa kwenye machafuko na chuki ya kibaguzi kwa majirani bila sababu za msingi.
Heshima ya Tanzania imezikwa na Kikwete.
You have a troubled mind probably originating from a troubled past!

Mtu anakutukana kotaifa, halafu bado unamchekea chekea.
Heshima yako unayoiongelea must be from standards of your own troubled up bringing.
 

Kumuunga mkono tu hata pale anapochemka hakumsaidii yeye kubadilika,haiwasaidii kitu washauri wake ambao walikaa kimya mpaka anajitumbukiza humo, haiwasaidii wanaosaidia uvunjaji wa sheria zetu za uhamiaji (wakiwemo askari uhamiaji), wala haiwasaidii Wananchi wa Nchi zote mbili ambapo kesho na keshokutwa watakutana na matokeo ya uhusiano mbovu baina ya nchi hizi! Na kumkosoa hakumaanishi hawa wahamiaji waendelee kukaa bila uhalali. Tunachosema ni kuwa kusiwe na upendeleo wa hukumu na kusiwe na hukumu za jumlajulma. Haki za wote zizingatiwe kikatiba. Wakati unasema "wahamiaji haramu" kumbuka unaweza kuwa unamwambia Mtanzania mwezio ana "mama haramu" au "mkewe haramu" au "mjomba haramu" Au hujui kama watu wa mipakani wameoleana, wana ndugu wengine nchi jirani, au huenda hata huduma za kijamii kama hospitali na shule wanapata nchi nyingine? Fuatilia hilo na utajua kuwa it is really a complex matter.Huu ni mgawanyiko utakaoanza kututafuna wenyewe. Trust me on that. Kushughulikia mambo ya mipaka kunataka busara ya hali ya juu sana!

Lakini ni vema ufahamu na kukumbuka kuwa "HATA BAADA YA KAGAME NA KIKWETE KUPITA, TANZANIA NA RWANDA ZITAENDELEA KUWEPO" So ni vizuri kila kitu kikachukuliwa kwa busara zake kwa faida ya Tanzania na Rwanda ya leo na kesho!
 
wewe ni kichekesho halafu ni msahaulifu sana!hujawahi kusikia wamachinga wa Dar wakilalamikia 'wamachinga' kutoka china?Hawa nao wako kwenye mkondo wa siku 14?au tumewasahau kwa kuwa jingping ni best wa JK?
Au unataka mpaka waue mbongo ndio uone hawahitajiki nchini.

NASHUKURU UMERUDI ILI UENDELEE KUPATA DOSE!
 
meningitis,

..kwanza, ktk mijadala yoyote ile usiwe mkali sana kama hapo unaposema "..watanzania mliojaa unafiki mioyoni mwenu..."

..tukirudi kwenye hoja yako, hata mimi sikubaliani na jinsi JK alivyoshughulika na kashfa luluki ktk nchi hii kwa mfano, EPA, madawa ya kulevya, mauaji ya Mwangosi, mabomu ya Arusha, etc etc

..lakini kwa haya maamuzi aliyochukua kurudisha RULE OF LAW ktk mkoa wa Kagera namuunga mkono. Zaidi namsisitiza Raisi na serikali yake wa-enforce the law ktk maeneo hayo mengine uliyoyataja, mfano EPA, madawa ya kulevya etc etc.

..RULE OF LAW ni moja ya vichocheo muhimu kabisa ktk ukuzaji uchumi na kuendeleza mahusiano mema ya kidiplomasia.
 
Last edited by a moderator:

Hivi hukuona siku lazaro Nyarandu alipotembelea Kariakoo na kutoa amri ya wahamiaji haramu wa kichina waondoke?

Au unafikiri serikali ni Kikwete tu?
 
Ahaa, hivi kumbe Wanyarwanda ni adui zetu? Now I get it.

Mkuu you are letting down your intellectual might.
Jirani yako anamshambulia jirani yenu-common- kwa jeshi lake analoliita M23
Jirani yako anaonyesha hostile maneuvres kwa ku- infiltrate nchi yako
Jirani ysko anakutukania mkuu ea nchi yako na kuahidi "kukufanyizia"

Halafu wewe unaamua kumchekea chekea kama zuzu
Better find a better class of neighbours!!
 
pole kwa kuhisi nimekuwa mkali.
Naona unakubaliana na MMM kwamba tusiwe na 'selective justice' yaani hiyo rule of law isiwe kwa kagera tu bali kwa maeneo yote na nyanja zote na pia iwe sustainable na halafu isije wakati tunapotukanwa au kukosana na watu flani!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu JokaKuu,

Wadau wanaomtetea Kagame na matusi aliyotoa kuna kitu wanashindwa kuelewa.

Iwapo jamii yetu itachanganyika na wahamiaji haramu wenye silaha kutoka kwenye nchi ambazo zina chuki na sisi, wahamiaji hawa wanaweza kutumiwa kama njiti ya kibiriti kwenye mafuta ya taa.

Vilevile hawa mashabiki wa Kagame wanashindwa kuelewa kuwa unapokuwa na wahamiajo haramu, adui yako anaweza kuleta wanajeshi wake nchini kwako washambulie huku wakijifanya kuwa wao ni wahamiaji haramu. Hili analifanya Kagame huko Congo kwa kupeleka wanajeshi wake na kuwavisha uniform za waasi.

Wahamiaji haramu maeneo za Kagera, Geita na Kigoma wana silaha kali sana kiasi kwamba wanakuwa tishio hata kwa askari wetu. Je, hizi silaha hawapewi na mtu mwenye chuki na sisi?

Tatizo ni kwamba kuna watu hawajali maisha ya watanzani wanaosumbuliwa na wahamiaji haramu, tamaa zao za kisiasa wanazipa nafasi kubwa kuliko ustawi wa maisha ya watanzania wenzao. Mfano wa watu wa namna hiyo ni Mwanakijiji...
 
Hivi hukuona siku lazaro Nyarandu alipotembelea Kariakoo na kutoa amri ya wahamiaji haramu wa kichina waondoke?

Au unafikiri serikali ni Kikwete tu?
hizo mbwembwe za nyalandu ziliishia wapi?alitoa siku ngapi vile?wachina walioondoka ni wangapi?
Kama serikali sio kikwete kwa nini hili la kagera hakuachiwa waziri husika....hapo ndipo unapozodi kudhihirisha kuwa jambo hili ni la kukurupuka na kisasi.
 

Mkuu kwa heshima kubwa uliyonayo humu JF na nje ya hapa, basi kuna haja ukaweka hiyo historia ya Mwalimu Nyerere kuhusu wakati wa matatizo na Uganda kabla hujahitimisha lawama zako kwa Serikali chini ya JK.Zaidi ya hapo hisia ya utendaji mbovu wa Serikali na mambo mengine unaweza kuwa sababu za huu mtazamo uliokuwa nao.

(selective justice)
Ebu tuangalie hapa tu ! Kwa hiyo kuanza kufanyia kazi sheria huko Kagera na Kigoma kunatosha kuitwa selective?


 

Way too out again. Hakuna anayesema waendelee kukaa Tanzania. Tunasema busara na diplomacy ni better than bifu!
 

Kwnai mbwembwe za Kikwete zimeishia wapi mpaka unazifananisha na za Nyarandu?
 

Unajua kutongoza! I GIVE YOU THAT! Hoja zako zinakwenda sambamba na jicho lako zuri (You must be very beautifull!), yaani unawezamlegeza chui mwenye njaa! Lakini hoja hapa sio Kikwete na Kagame, tatizo letu ni la muda mrefu la wahamiaji haramu ambao pamoja na kuharibu mazingira yetu na kutuletea biashara ya zana za kivita haramu na kujihusisha na vitendo vya ujambazi bado wengine wanaongozwa na vichaa wanaofikiri jumuia ya Africa mashariki inawapa nchi yetu kama koloni lao na Rais wetu kama mkuu wa mkoa!
NDUGU, MAAMUZI YA KIKWETE NI SAHIHI HATA DUNIA NZIMA IKIPINGA!
ANYATHING SHORT OF THAT IS "UTTER NONSENSE! AND IF IT IS AN IDEOLOGICAL PROBLEM THEN WE BETTER LEAVE IT WITH THOSE WHO HAVE IT, AND...,MAYBE, DEAL WITH IT LATER!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…