Mzee Mwanakijiji,
..kwani sheria za Tz zinasemaje kuhusu suala la "illegals"?
..mimi nadhani Mwalimu angefuata sheria za Tz jinsi ya ku-deal na "illegals."
..kwa mfano, hivi mlitegemea Mwalimu angecheka na mtu yeyote yule, raia ,au "illegals," ambaye ameingiza mifugo kwenye misitu ya hifadhi?
..je, Mwalimu angetoa siku 14 kwa majambazi, raia au "illegals," wasalimishe silaha zao?
Jasusi atakumbuka jinsi Mwalimu alivyopeleka askari wa JWTZ kushughulikia wale wahuni waliojitangazia uhuru na jamhuri yao kule Mara.
..Kwa hiyo jibu langu ni kwamba Mwalimu angezingatia sheria za Tanzania. Hawa tunaoshughulika nao sasa hivi siyo wakimbizi, ni wahamiaji haramu.
..Kwa mtizamo wangu, tusimkatishe tamaa Raisi Kikwete. Badala yake tum-challenge ashughulike na wahamiaji haramu popote pale ktk Jamhuri yetu.