meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,425
- 4,768
naona taratibu unaanza kulielewa somo.Ni maamuzi ya kisiasa kwasababu siasa intawala maisha yako. Kama Kgame alivyotukana hakuhitaji ushauri wa Daktari au Engineer. Haya ni maamuzi ya utawala unaowekwa kwa njia za siasa. FYI kurudisha wahamiaji haramu ni agenda katika kampeni za Marekani na kwingineko, je si maamuzi ya kisiasa?
Hivi unahitaji mtaalam wa madini, daktari au Engineer kuamua kuwa mhamiaji haramu aburuzwe kwenda kwao.
Maamuzi yamepangiliwa ndio maana hakuna Mtanzania anayepelekwa Rwanda kwa bahati mbaya, na kuwa wamezingirwa na wanvuka mpaka wenyewe. Bila mpangilio huwezi kukabaliana na M23 Tanzania branch ya Kagame
Hakuna ubaguzi wa kumshughulikia mhalifu. Serikali ya Tanzania haihitaji ridhaa ya Kagame katika kutekeleza majukumu yake.
Ni endelevu kwasababu wakirudi itatufutwa mbinu nyingine. Kwa kiasi fulani nakubaliana nawe kwasababu walipaswa wafikishwe mahakamani waadhibiwe, wakimaliza adhabu zao warudi kwa Kagame kwa amani.
Umetoa mfano mzuri sana wa jinsi USA ilivyoshughulikia/inavyoshughulikia suala la wahamiaji haramu.Nieleze sera ya ccm juu ya suala wahamiaji.
Ni ubaguzi kwa kuwa wahamiaji haramu hawako kagera tu na wala si wanyarwanda tu(usiseme hawa ni wahalifu kwani uhalifu umetapakaa nchi nzima).
Sio endelevu kwa kuwa uamuzi huu haukuangalia chanzo halisi cha uwepo wa wahamiaji haramu badala yake chanzo kimekuwa ni matusi ya kagame.
Sote tunaipenda nchi yetu
Sote tunawapenda wana kagera
Sote tumechukizwa na matusi ya kagame dhidi ya taasisi ya urais
Kamwe tusilipe ubaya kwa mabaya bali tulipe ubaya kwa wema ikiwa kweli Tanzania ni kitovu cha amani.