Swali: Serikali kushindwa kuwadhibiti wakopeshaji wa online ni ishara kuwa hii nchi wenye pesa wana nguvu kuliko serikali?

Swali: Serikali kushindwa kuwadhibiti wakopeshaji wa online ni ishara kuwa hii nchi wenye pesa wana nguvu kuliko serikali?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!
Suala la kero za wakopeshaji wa mitandaoni limekuwa kero kubwa. Kila ukiperuzi mtandao wowote Tanzania usipotumia VPN matangazo ya mikopo yatajazana mbele yako mpaka kero.

Kwa wakopaji kero wanazokutana nazo ni pamoja na kudaiwa pesa kabla ya siku ya makubaliano, kudhalilishwa, watu wanadhalilishwa na kutukanwa na wahudumu kabla siku halali ya malipo.

Kuuza taarifa sehemu B.
Yaani ukikopa sehemu A, na ukawa mlipaji mzuri wanauza taarifa sehemu B, unaanza kypigiwa simu kila siku ya kukutaka ukope kwenye app yao.

Kero nyingine ni kubadilishiwa kiwango cha pesa ya mkopo huku tayari ushakubali na huwezi ku deny maana hakuna option ya ku cancel.

Ndugu, marafiki na wengine kusumbuliwa bila sababu za msingi na wengine wanatishwa.
Nimewahi kuwa mkopaji huko ila sasa sikopi tena. Nasumbuliwa sana wakipiga simu wakitaka nikope tena.
Serikali iko kimya, dhuluma kwa Watanzania ni nyingi

Hii inatoa picha kuwa wenye pesa sasa wamekuwa na nguvu kubwa sana. Untouchable.
Ni vigumu sana kumfundisha kijana kuwa mzalendo kwenye nchi ambayo tajiri ana nguvu kuliko serikali.
Hata haya mabenki yanatunyonya sana.

Nimekopa juzi ml. 17 miaka 9 nitalipa mil. 35, hapo ningekopa microfinance kama finca, Bank ABC ningelipa hata millioni 40.
 
Mil 17 miaka 9 unakaa na pesa ya watu ulitaka urudishe Tsh ngapi? Kuhusu hawa wakopeshaji uchwara watu wote wakope wasilipe ili wakianza kutafuta mdhamini wanakuta naye kakopa hajalipa. Akipatikana kiongozi akaanzisha hii kampeni ya kopa usilipe hizo kampuni zitajifia.
 
Hao jamaa wananidai hadi 1.5 saizi napigiwa simu kama vichaa vielfu 70 vingi mpaka vimefika M na kitu, kumbe niwakazie tu 😄
 
Hao jamaa wananidai hadi 1.5 saizi napigiwa simu kama vichaa vielfu 70 vingi mpaka vimefika M na kitu, kumbe niwakazie tu 😄
Duh. Si nasikia app zishafungiwa na BOT?
 
Back
Top Bottom