SWAT, FBI na CIA nini tofauti ya hizi taasisi?

SWAT, FBI na CIA nini tofauti ya hizi taasisi?

Sasa unahisi Child pornography sio hatari kwa usalama wa marekani au unahisi hatari ipo kwenye issue nyingine tu au??
Ukisema hivyo hata Kukata Miti itakuwa inashughulikiwa na FBI, maana nayo inaweza kuwa hatari kwa usalama wa nchi.
 
Wanakuonyesha tu watu wako kwenye vyumba vya giza. Pitia bookshop, tafuta vitabu vya Nigel West; ana madini mengi sana.
Siwezi kukukatalia kuhusu hilo kutokana na uwezo wako unavyoelewa mambo....

Polisi hawawezi kuwa Kama FBI hata siku moja....

Polisi wanafanya kazi kijamii kwa hiyo makosa ya jinai yanachunguzwa kwa uwazi tu...
 
Siwezi kukukatalia kuhusu hilo kutokana na uwezo wako unavyoelewa mambo....

Polisi hawawezi kuwa Kama FBI hata siku moja....

Polisi wanafanya kazi kijamii kwa hiyo makosa ya jinai yanachunguzwa kwa uwazi tu...
Mpaka sasa hivi unazunguka tu au nikuulize swali jepesi, ni idara gani inachunguza makosa ya jinai Marekani?
 
maneno jasusi na upelelezi unayatumia vibaya.

FBI siyo shirika la ujasusi bali ni ofisi inayoshughulika na upelelezi wa makosa ya jinai ndani ya Marekani; ni kama CID hauku kwetu. Wako mbele kidogo zaid ya CID, kwani wanafanya upelelezi wa makosa yaliyokwisha fanyika, na vile vile kufanya upepelezi wa kuzuia makosa yasifanyike. Huwa hawafanyi ujasusi wa ki-James-Bond kama wa CIA bali wanapeleleza na kukusanya ushahidi pamoja na mashahidi. Ushahdi wanaokusanya lazima uwe sahihi kwa sababu baadaye utapimwa na mahakama.

CIA siyo shrika la upelelezi bali ni ofisi ya ujasusi inayoshughulika na mambo yote ya ujasusi nchi za nje ikiwa ni kupata habazi za usalama kijasusi, kufanya sabotage kwa maadui kijasusi na kadhalika. CIA haifanyi kazi ndani ya Marekani. Huwa hawapelelezi bali hufuatilia na kukusanya taarifa wanazoona ni za muhimu kwa usalama na malengo ya Marekani. Habari hizo zinaweza zisiwe sahihi kwani hakuna kipimo cha kuzithibistiha.
Unamkosoa mwenzio badala ya wewe kusema ukweli ila ndo umekuja kuharibu, maelezo ya mleta mada yapo sahihi kwa 100%.
 
Unamkosoa mwenzio badala ya wewe kusema ukweli ila ndo umekuja kuharibu, maelezo ya mleta mada yapo sahihi kwa 100%.
Mada yake iko sahihi ila ametumia maneneo hayo vibaya; hata ukiwauliza wataalum wa kiswahili watakafufafanunia. Ujasusi ni zaidi ya kupeleleza; ujasusi hufanyika kisiri sana wakati upelelezi hufanyika hadharani tu. Ni vivyo hivyo, CIA hufanya kazi zake gizani wakati FBI hufanya hadharani tu.
 
Yote uliyosema ni kweli ila unayatafsiri vibaya hasa unapotaka kutenganisha function ya security na ya intelligence ambazo naturally ziko intertwinned.

Nikurudisha nyuma tena kuwa CIA hawana jurisdiction ndani ya nchi, hawaruhusiwi kabisa kufanya ujasusi ndani ya nchi. Mambo yote ambayo CIA wangependa kuyajua yanapotokea ndani ya mipaka, yanakuwa ni crimes inayoshughulikiwa na FBI ambao wana kitengo kinaitwa Intelligence Branch (IB). Iwapo uhalifu huo unafanyika ndani ya mipaka ukiwa unahusisha na watu walioko nje ya nchi, basi NSA ndiyo inayoshulikia. Electronic surveilance ni sehemu moja tu ya kazi za NSA lakini zipo nyingine. It happens tu kuwa mtu anayefanya mambo yanayodhaniwa kuwa ya ughaidi akiwa anashirikian na watu wa nje atatumia mawasiliano electronic, kwa hiyo ndiyo maana electronic surveillance inaonekana kuwa ni kubwa sana, lakini elewa pia kuwa CIA nao wana electronic surveilance yao. Kwa hiyo ni kweli kuwa NSA ina juridiscation ndani na nje ya nchi hivyo ni kubwa zaidi ya CIA, lakini kuna majukumu ambayo yamepewa CIA tu nje ya mipaka ambayo NSA hawawezi kuyafanya . Hiyo ni pamoja na kuwa CIA inaweza kufanya sabotages mbalimbali pamoja na assasination ya magaidi ambao ni hatari kwa usalama wa Marekani, vitu ambavyo NSA haiwezi kuvifanya.

Siyo kweli kuwa security agencies zote ni za ujasusi kama wa CIA wala hazina malengo yanayofanana. Agencies hizo nyingi ni za ujasusi wa kijeshi kulingana na branches za jeshi la marekani. Agency za kiraia, zaidi ya CIA, FBI, na NSI (hii iko pande zote za kiraia na kijeshi) nyingine ni pamoja na ONSI (ujasusi wa kutafuta taarifa za vyanzo vya madawa ya kulevya), OICI (Ujasusi wa kutafuta habari zinazohatarisha nishati ndani ya nchi pamoja na ujasusi wa kutafuta habari kuhusu matumuizi mabaya ya nishati ya nyuklia) na INR ( kwa ajili ya ujasui kutafuta habari zinazohusu usalama wa mabalozi). Agencies nyingine huwa hazifanyi ujasusi bali zinafanya analysis ya habari za kijasusi zinazopatikana kutoka kwenye agencies nyingine kwa malengo maalumu. Hizi ni pamoja na OIA (kuchambua taarifa mbalimbali za kijsausi kuangalia kama zinahusisha utakatishaji wa pesa) na I&A ( hii inakusanya taarifa mbalimbali za kijasusi na kuchambua namna ya kuzifikisha kwenye idara zinazaozhitaji habari hizo zaidi). Agency nyingine zote za kijasusi zilizobaki ni kwa sababu ya branches mbalilmbali za kijeshi tu, sasa hivi imeongezwa moja ya Space Delta 7 kwa ajili ya ujasusi unaohusiana na usalama wa satellites tu
Wote hao wapo chini ya Homeland Security...Director wa hii taasisi ndio ana organise reports zote za mashirika mengine kwa ajili ya briefing kwa Rais daily
 
Kwani nani ambaye amebisha kwamba FBI ni domestically nianzie hapo kwanza......

Ila uelewa wako ndo umeishia hapo mm niliielezea hiyo Tv show ili kuleta logic....

Na wewe pia kwa nn usiwe mjuaji pia kwani inakatazwa....
Bahati mbaya sana huwa sifanyi argument na Idiots ka nyie,
 
Back
Top Bottom