Wewe jamaa una kichwa kigumu hatari.
Unajua kwanini nilikuuliza nani anachunguza federal crimes huko Marekani? Sio kwamba nilikuwa sijui jibu lake. Ungekuwa unajua mfumo wa law enforcement ulivyo US ungeelewa kuna Federal na State crimes.
Sasa turudi kwenye ABC.
US hakuna Polisi wa Taifa kama huku kwetu i.e Marekani hakuna IGP Sirro. Kule miji ina polisi wake wanaohusika na mambo ya miji yao. Sasa swali linakuja kama hakuna polisi wa taifa, nani anafanya kazi kwenye maswala ya kitaifa? Ndio linapokuja swala la majukumu. Kuna taasisi zinadeal na mambo ya Federal tu, na premier agency ni FBI. Ndio wanaofanya kazi "kama" polisi wa taifa. Ndio maana nikakumbia wanafanya majukumu ya polisi. Sasa wewe unadhani FBI kazi yake ni maswala yanayohatarisha usalama wa Marekani; wakati FBI inadeal mpaka na Child Pornography.