Sweden yapunguza misaada kwa Tanzania kuwa 75% kwa miaka mitano ijayo

Sweden yapunguza misaada kwa Tanzania kuwa 75% kwa miaka mitano ijayo

Nafikiri kuna kitu nje kabisa ya haki za binadamu na demokrasi kwenye sakata hili; time will tell. Ukilinganisha Tanzania na Rwanda kuhusu demokrasia na haki za binadamu, utaona kuwa serikali ya Rwanda ni katiri sana kwa wapinzani; mwulize mama Victoire, General Nyamwasa, au yule mwanamuziki na wengine wengi waliotoweka lakini jamaa hao hao hawajatoa tamko. Kulikuwa na tamko la kupinga Kagame kubadili katiba ili atawale maisha lakini wakaishia kunyamaza kimya kimya.
 
Tusifurahie jamani, kwa sisi watu wa chini maisha yanaenda kusimama!

Sent using Jamii Forums mobile app
HATUNA HASARA WW. Hii serikali TAJIRI ikiminywa kila sehemu itakosa jeuri ya kutawala ndio tutapata sababu ya KUITIMUA. Vikwazo ni kwa SERIKALI sio Watanzania. Sisi ndio mabosi wao, mambo yakiwa mabaya kwa kunyimwa misaada kunakosababishwa na KIBURI na UJEURI wa watawala TUNAWATIMUA wakafie mbali. SIO NCHI YA CCM HII. Inaweza kuongozwa hata na VICOBA ili mradi katiba iheshimiwe tu.
 
ksk,
SIASA ZA UPINZANI HAPA TANZANIA ZIMEKOSA DIRA NA MWELEKEO. JAPO WANASEMA SABABU NI MAGUFULI KUZUIA MIKUTANO BINAFSI NADHANI HATA KAMA MAGUFULI ASINGEZUIA MIKUTANO BADO HAWA WAPINZANI WETU WACHUMIA TUMBO HAWANA HOJA YA MAANA YA KUSHAWISHI WATU KUIONA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWAMBA HAIFAI.

WAMEKOSA HOJA WELEDI BAADA YA KUBADILISHA GIA ANGANI SASA WAMEBAKI WANATANGATANGA TU KAMA WAZURURAJI.
 
Huko Sweden si ndiyo yupo Nguli wetu Dr. Slaa? Kwanini ameshindwa kushawishi kinyume chake?
Hilo nililitarajia sana, huwa Marekani akianza kutoa taarifa za ki CIA basi tutarajie nchi washirika nyingi kuja na misimamo yenye aina moja kiuelekeo.

Taarifa za CIA huwa rasmi kwa nchi nyingi washirika kwani wao pia huhusika kwa namna moja au nyingine katika kupatikana kwa taarifa hizo
Nakufatilia kwa karibu upo vzr kaka
 
Huko Sweden si ndiyo yupo Nguli wetu Dr. Slaa? Kwanini ameshindwa kushawishi kinyume chake?
Hilo nililitarajia sana, huwa Marekani akianza kutoa taarifa za ki CIA basi tutarajie nchi washirika nyingi kuja na misimamo yenye aina moja kiuelekeo.

Taarifa za CIA huwa rasmi kwa nchi nyingi washirika kwani wao pia huhusika kwa namna moja au nyingine katika kupatikana kwa taarifa hizo
Siii walisema hii inchi tajiri, mbona mwaanza kulalama tena!!! Swalamaaa huko! Inchi hii tajiri bwana,Nyerere Hydroelectric power bado, standard Gauge bado uwiiiii!! Tafadhali jamen huu ut tusijejetukauana buree
 
Enyi kizazi cha Dr. Shika, ni nani aliwaambia kuwa Mzungu ni rafiki wa Mwafrika? Nimeona anasema "development zinaenda wrong direction".

Ni nani hakushuhudia jinsi Ujarumani walivyotupinga mradi wetu wa umeme pale mto rufiji kwa madai tutaharibu mazingira, yaani wao kwao wamejaza miradi mpaka chini ya ardhi halafu kwetu ndio tulinde mazingira tena kwa kuhurumiwa na wao!

Sweden anasema Mipango ya maendeleo haiendi ilivyopangwa, unaweza kuona jinsi jenzi mbalimbali zinavyoendelea, hapa sio kwamba maendeleo hayapigi hatua.

Hawa walizoea kutoa pesa za miradi zinaliwa bila miradi kutekelezwa hivyo kuilazimu serikali kuendelea kukuza deni hali inayowapa fursa wao kuendelea kutunyonya maliasili zetu, sasa wanaona pesa inatumika katika miradi wanajua soon tutapunguza au kuacha kabisa kuwategemea na hapo watakosa kutunyonya.
 
Huko Sweden si ndiyo yupo Nguli wetu Dr. Slaa? Kwanini ameshindwa kushawishi kinyume chake?
Hilo nililitarajia sana, huwa Marekani akianza kutoa taarifa za ki CIA basi tutarajie nchi washirika nyingi kuja na misimamo yenye aina moja kiuelekeo.

Taarifa za CIA huwa rasmi kwa nchi nyingi washirika kwani wao pia huhusika kwa namna moja au nyingine katika kupatikana kwa taarifa hizo
Not only that ,,,,bila shaka ttaanza kutegmea mapato ya ndani na uwekezaji,,,ttegemee kodi kupanda ,hakutakua na nyongeza ya biashara due to budget deficit...pia utakua mbinde kuajiliwa ,,,,nazan vilimo vinavyotegemea vyama vya ushirika kuuza mazao vitabanza zaid maana huko ni rahis tra kujipangia kodi nazungumzia korosho na tumbaku,,,,,
 
Uledi,
Kaka , "Sweden" si mtu hivyo usiite "huyo". Ni nchi.
halafu beberu ni "imperialist", sivyo? (bado naamini maneno yana maana maalumu). "Imperialist" ni yule anayetafuta "empire" juu ya watu wengine, nchi nyingine. Sweden sasa?

Ni nchi ndogo yenye wakazi milioni 10 hivi. Haikupigania vita tangu miaka 200. Ninavyosikia ni nchi tajiri kwa sababu hawakupiga vita na kuchapa kazi.

Sweden kuonea wivu Tanzania ? Unaiamini kweli? Wivu kuhusu nini ?
Cjui inasaidia kurudia slogans bila kutafakari.

Labda ni watu tu walioamua kutoa msaada kwa sababu wanaona si vizuri kama pengo baina matajiri na maskini inaongezeka mno. Na kwa sababu waliona Tanzania si tajiri (maana hawatoi msaada kwa Kuwait au Saudia) bali maskini.

Halafu walipenda Tanzania kwa s ababu walitawaliwa na Masocial democrates waliomwona Mwalimu Nyerere alifanana na itikadi yao (si ubepari tupu, si ukomunisti) hivyo walisaidia miradi mingi sana tangu siku za Mwalimu.

Na pia ni watu ambao hawapendi kufanya na kutoa pesa dhidi ya imani yao - kwa hiyo wakipata picha haki za binadamu (jinsi wanavyoelewa hao) hayao sawa TZ, basi wanapunguza kutoa.

Sasa hii ni ubeberu? Haya.
 
Mwanamkiwi,
Asante kwa darsa ila hayo nayajua yote na ziada. Bado nawaita Sweden mabeberu kwa maana ndivyo ccm inavyotaka tuamini. Ccm wanaamini kila anayewanyima msaada ni beberu. Subiri uone jinsi watakavyo itukana Sweden kisa wamepunguza msaada. Watawaita kila jina baya ikiwemo "mabeberu"
 
Wengi wetu tulitarajia haya, na tunaona kama yanachelewa kutokea vile!!! Na tusipoangalia tutakuwa kama Zimbabwe. Enyi washauri wa mzee baba, mwambieni kuwa "liishalo ni dogo kuliko linalokuja!".
 
Conclusively hiyo deficit ni kubwa na ulikua inachangia kubalance budget ....mataifa meng yatapunguza msaada and its going to be worst ,,,advice serikali irudishe cost sharing in education kubalance budget.

Mfano shule ya kata yenye wanafunz 1000 itapokea kusanyo la ada la Tsh 20,000,000 inatosha kulipa hata walimu wanne wenye degree kwa mwaka it will help.

Pia serikali itapunguza garama kama za rimu na nyinginezo ....ila tnaowategmea wamejikataa wallah ttakimbia vitu tulivyochonga
 
Back
Top Bottom