Kuna tofauti ipi kati ya tamthilia hii 'Kosem Sultan'
na hii 'Sultan' inayorushwa Azam tv
Nimeangalia Kosem Sultan binti mrembo Anastasia anatekwa kutoka ugiriki mpk jengo la kifalme instambul kipindi hicho mtawala wa taifa ni sultan ahmed aliye apishwa na Saphia Sultan(grand queen),baadae mwishoni akaja mtawala Osman (mtoto wa Ahmed na Anastasia) yakatokea mapinduzi ya kijeshi Osman anauliwa na Mustapha (mdogo wa Ahmed/mtoto wa Halima)anakosa vigezo vya kuwa mfalme kutokana na matatizo ya akili ,
Anastasia (mother queen) anaua wasaliti wote walioshiriki kupindua nchi ikiwemo Dilhuba na mama yake yani (Halima), kisha tamthilia inaishilia ep 100 mahali Anastasia (kosem) anaelekea kumuapisha mwanae mmoja kati ya watoto 4 kuwa mtawala wa taifa.
NAOMBA: Mwenye kufahamu, je hiyo Sultan inayorushwa Azam ni mwendelezo huu au ni series nyingine, na kama ni mwendelezo zipo series ngapi za hii tamthilia matata ya kifalme (Ottoman empire) ndani ya viunga vya instambùl -TURKEY.?
Natanguliza shukrani za dhati kabisa... Asante!
Sent using
Jamii Forums mobile app