Nilikuwa na mwanaume ambaye anataka Mimi ndiyo niwe kichwa cha familia, just imagine familia iongozwe na mtu ambaye anatumia hisia badala ya akili, kuna kutoboa hapo kweli..??
Yeye kila kitu ajibu Ndiyo, ukimpa ideas hana challenges zozote zile, Ilikuwa ni mahusiano ambayo Mimi ndiyo natakiwa niwe na ultimatum, kwenye kila wazo yeye anataka kujua unawaza nini, utakachojibu ndicho atakachosema 'Sawa'..!
Wakati tukio hilo la kusikitisha likiendelea, Mimi nilikuwa nataka mwanaume ambaye ni KIONGOZI, ambaye ana akili kuniliko, mwanaume ambaye nitaweza Kumuheshimu na Kumsikiliza without second guessing, mwanaume ambaye sitakuwa natoa maelekezo bali tutakuwa tunajadiliana kwa kina, nikaona nitakuja msumbua bure kijana wa watu, akili za kaskazini hazitaki akili iliyolala..!!
Nikatembea mbele na Bwana, sahii niko na hekaheka moja matata sana, mnafanya mazungumzo mpaka hoja zinakuishia unanyanyua mikono juu mwendo wa mateka, and daaaaang', that is my thing..!!