Taa nyekundu ikikuwakia, simama, kuendelea na safari ni kujitakia kifo

Taa nyekundu ikikuwakia, simama, kuendelea na safari ni kujitakia kifo

Njooni huku; naona kwenye ule uzi mwingine tumevamiwa na jinsia ya upande wa pili, ngoja tuwaachie.

Mahusiano ni kuvumiliana na kuchukuliana madhaifu yetu, ila kuna wakati unasema hapana, siwezi kuendelea.
Ladies, nini kilikutokea kwenye mahusiano kikafanya red light iwake kichwani na umuache mpenzi / mwenza / mume wako?

*Naanza: *

Mwanaume alikua mvivu, hajishughulishi, akili mgando na mlalamishi.
Kila akipata ajira hadumu anafukuzwa kwa sababu ya kutokujituma na malalamiko yasiyoisha (Ajira 3 tofauti in 2 years). Nilikua nalipa ada za wadogo zake, kodi nyumbani na majukumu mengine yote. Japo alikua na mema yake ila baada ya miaka miwili nilichoka na nikaona hakuna future. Niliomba uhamisho kazini kwenda mji mwingine, nilivyofika tu makao mapya, nikampiga kibuti.

── ⋆⋅☆⋅⋆ ──

CC:
nakwede97Aaliyyah
Sister AbigailBantu Lady
realMamyQashy Lilith
Atoto
Niwaheri
Lamomy
To yeye
Msweet
Chujio
Demi
ledada
Midekoo
Carleen
ABJ

Waiteni na wengine!
Chai
 
Hilo linaeleweka kitambo huña haja ya kujenga hoja.
Mwanaume ukiwa huna hela mwanamke anakuona tàkataka tuu.
Kabisaaaa. Sawa na sie wanaume mwanamke ambae hana tako ni takataka kabisa 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Haya mambo huwa yanaenda vice versa, ukikuta mume amenyooka, ni husband material haswa, basi mke mara nyingi anakuwa kimeo.

Ukikuta mke amenyooka kama wewe, ni wife material haswa, basi mume anakuwa goigoi kama huyo wako..
Bora hao wanabalance equation. Sasa uwakute wote vimeo, yaani ni vurugu mechi🤣
 
Kuna zile story za kwamba unatoka na mtu chini hamna kitu yaan sijui nikikuambia chini unaelewa? Halafu tunakuja kukaa vizur kiuchumi anakuona wewe so kitu ni story ndefu ila mungu anajibu maombi nilipata hasira mnooo nikawa naomba mungu huyu mtu muadhibu Kwa namna yoyote
Mungu yupo nyie mungu yupo na anajibu yule mtu karud alipotoka ameanza moja Tena Kwa kipigo takatifu Allhamdullilah 🤲
Lakini nimeinuka tena alafu ndio nataka nioe rasmi sasa
 
Sasa hii taa nyekundu yangu ERoni
Niendelee nayo au niishie njiani🙆‍♂️🙆‍♂️
Anyway ngoja nipite tu, ajali haina kinga🤣🤣🤣
 
Mungu yupo nyie mungu yupo na anajibu yule mtu karud alipotoka ameanza moja Tena Kwa kipigo takatifu Allhamdullilah 🤲
Daaah sijui alikutenda nini ila usimuombee mabaya kiasi hicho🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Tusiwe na too much expectations, some relationships are not meant to last. Na wakati mwingine ni sisi tunang'ang'ania pasipofaa, then baadae tunaanza laumu watu.
 
Daaah sijui alikutenda nini ila usimuombee mabaya kiasi hicho🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Tusiwe na too much expectations, some relationships are not meant to last. Na wakati mwingine ni sisi tunang'ang'ania pasipofaa, then baadae tunaanza laumu watu.
Ndio maana nakupenda we mwanamke, yaani mtu anatendwa na kuweka visas na laana juu, ya nini yote hayo? Mimi naamini ni sehemu ya maisha tu, jifute usonge mbele.
 
Hapanaaaa, nyie bwana ni zoa zoa tu, mnatia mimba hadi vichaa. Hambagui hamchagui, ataewazika hamumjui[emoji1787][emoji1787]
Huwa najiuliza akili za baadhi yao sijui zikoje naishia kucheka sijui hawanaga kinyaa [emoji706]
 
Back
Top Bottom