Taa nyekundu ikikuwakia, simama, kuendelea na safari ni kujitakia kifo

Taa nyekundu ikikuwakia, simama, kuendelea na safari ni kujitakia kifo

Mimi ubishi na wivu wa kipumbavu nilitoka 🏃🏽‍♀️Baada ya kupata story yake huko kwao kigoma aliwahi kumkata mpenzi wake mkono nikasema toba roho yangu.
Wii hii sikuiona wee 😹😹
Jamani kukatana mikono tena??! Wohiii Wohiii
 
Tilipendana ila mm nikafall Zaidi nikapata story ana mwanamke nikawa nalia na kumbembeleza asiniache wakat huo anakana kuwa sio mwanamke wake
Kipindi hiko Hana kazi anafatilia mipango aingie jeshini

Sikuwa na ujasiri wa kumuaccha had akanitamkia wazi siwez muacha nilionyesha rangi zote had za njano still nikakomaa 😃😃
Nikawa nashindwa kuonana nae Kam zamni nikawaa naandik barua za mapenz na kubembeleza 😃
Rafikizangu wakaanza kunichukia nilikuwa sishauriki kwa yule jamaa Yani watasema hadi walie akinibembelelza kidogo tu bas

Sikumoja tukakutana tukakosana akasema nifanye lolote yeye ni kma polis na mm ndo mwizi vyovyote vile pale ndo nyumbani 😃😃😃
Theresa49
Lamomy
Nuzulati
Bantu Lady
Wifi na barua ulikuwa unaandika?? 😹
Kweli ulipenda mahi wangu, ndo bwana wako wa kwanza?? 😜
 
Wifi na barua ulikuwa unaandika?? 😹
Kweli ulipenda mahi wangu, ndo bwana wako wa kwanza?? 😜
My Wii nilikuwa nusu mwendawazimu Yani nilipenda niliwashiwa had taa za blue bahari ila wapi fuvu limekaza Tena hizo barua naandika huku nalia sabbu nilikuwa siwez kuongea nilikuwa mkimya so live nilikuwa siwez kumkabili ni Kwa barua au Kwa simu ndio nitatoa la rohoni 😂
 
My Wii nilikuwa nusu mwendawazimu Yani nilipenda niliwashiwa had taa za blue bahari ila wapi fuvu limekaza Tena hizo barua naandika huku nalia sabbu nilikuwa siwez kuongea nilikuwa mkimya so live nilikuwa siwez kumkabili ni Kwa barua au Kwa simu ndio nitatoa la rohoni 😂
Pole sana 🥹😹
Haya endelea ikawaje sasa? Au ndo imeisha?
 
Njooni huku; naona kwenye ule uzi mwingine tumevamiwa na jinsia ya upande wa pili, ngoja tuwaachie.

Mahusiano ni kuvumiliana na kuchukuliana madhaifu yetu, ila kuna wakati unasema hapana, siwezi kuendelea.
Ladies, nini kilikutokea kwenye mahusiano kikafanya red light iwake kichwani na umuache mpenzi / mwenza / mume wako?

*Naanza: *

Mwanaume alikua mvivu, hajishughulishi, akili mgando na mlalamishi.
Kila akipata ajira hadumu anafukuzwa kwa sababu ya kutokujituma na malalamiko yasiyoisha (Ajira 3 tofauti in 2 years). Nilikua nalipa ada za wadogo zake, kodi nyumbani na majukumu mengine yote. Japo alikua na mema yake ila baada ya miaka miwili nilichoka na nikaona hakuna future. Niliomba uhamisho kazini kwenda mji mwingine, nilivyofika tu makao mapya, nikampiga kibuti.

── ⋆⋅☆⋅⋆ ──

CC:
nakwede97Aaliyyah
Sister AbigailBantu Lady
realMamyQashy Lilith
Atoto
Niwaheri
Lamomy
To yeye
Msweet
Chujio
Demi
ledada
Midekoo
Carleen
ABJ

Waiteni na wengine!
Nlimnyamazia bila.sababu
 
Nikachoka nikamwambia tuachane alicheka balaa alijua Sina ujanja nikaondoka kabisa pale nilivorud akawa kashaenda jeshin nikawa na amani kidogo alivorudi akaanza kuomba msamaha nikawa nachomoa hasira akaanza kunifanyia matukio ya ajabu ajabu ubabe na kunitishia maisha 😂😂

Aliwahi kupiga boyfriend wangu akapokea akamjibu hawez kuniacha aniache yeye ndo mumewangu 🤣🤣🤣

Nik akamfata aunt yangu kumuomba amuombee msamaha
Nikabadili namba akawa anazipatab nikiblock anatafuta namba mpya
Tulipofikia ni kuwa sitaolewa na nikiolewa atafanya vurugu siku ya harusi yangu Yani kasema ni lazima aniharibie 😃😃
Hadi hapo wii inaonyesha mtarudiana mnapendana nyie 😹
 
Mimi bhana ni story ndefu ila ni bonge la mwanaume, nikimfikiria nabaki nalia sana.!! 😭

Naweza kusema Mungu alinionyesha mwanaume ninayetakiwa kuwa naye ila kwa kunidolishia…. Unajua ile unapata kazi nzuri ina marupurupu ya kutosha na mshahara mkubwa bado dili za nje km zote?? Basi ndo nilikuwa mimi sasa..!! Niliokota dodo chini ya mnazi..!

Mpaka leo namlaani Mungu, ndiomana kuna muda siamini km yupo..!
Tuishie hapa nikiendelea kuna watu wanaojua kisa changu watanijua..!! 🥹
Pole mkuu, inaonekana umepita mapito sana maishani.
 
Back
Top Bottom