Taa yoyote nyekundu kwenye dashboard ya gari yako siyo ya kuipuuza

Taa yoyote nyekundu kwenye dashboard ya gari yako siyo ya kuipuuza

Na mbaya zaidi tatizo moja husababisha matatizo mengine kutokea.

Niliwahi kuwa na hilo tatizo la taa ya check engine. Nikaidharau.

Gari ikaanza kunywa mafuta kuliko kawaida, gari ikaanza kuoverheat, radiator top cover ikapasuka, silencer ikapanda juu na gari ikakosa nguvu kabisa.

Hizo taa usizichukulie poa, tatizo la kutibu kwa 100k unakuja tibu matatizo 6 kwa 800K. Ndo yalonikuta mimi.

Sema mkuu inategemea check engine imewaka kwa sababu ya nini. Kuna vitu huwa ni vidogo kama airfilter tu. Ila kama hiyo case yako inaonekana majanga yalianzia kwenye ECT sensor.
 
Safety features ni expensive kuziweka.

Gari ya mjapan inayoenda EU au US ni gharama sana kuliko hata za huyo mzungu kwasababu ya kuweka features kama za huyo mzungu.

Sema wenzetu wanajali sana maisha yao. Siyo kama ilivo huku kwetu. Mtu ilimradi gari linatembea tu inatosha. Mambo mengine yatajisort.
 
Mkuu mimi gari yangu inawaka taa ya abs muda sana zaidi ya mwaka.ina maana siku yyt tairi zinaweza kujilock?na nauliza tu spea za volvo zinapatikana uko nyumbani?
Maana nina wazo la kuja nalo uko .nishachoka na maisha ya stress ya south africa

Kama kuna siku utaendesha gari yako katika mazingira ambayo matumizi ya brake yatakuwa makubwa basi tairi zinaweza kulock up.

Pia kama gari yako ina features kama Traction Control basi hazitafanya kazi.
 
Waswahili Wana msemo "wasiwasi ndiyo akili"
Kama Mimi nikiona sign yeyote Kwenye gari lazima niende Kwa fundi immediately kwasabb sijui mambo ya ufundi kiundani zaidi pia Kwa mtu ambaye Hana uzoefu wa kutosha wa Magari ni Bora akimbilie Kwa fundi baada ya kugundua hitilafu

Ni kweli mkuu. Ila ndio maana nimejaribu kuhighlight rangi za hizo lights ili kuonesha urgency ya hilo tatizo.
 
Capture.JPG
Yangu kama miti ya krismass lakini naishi nayo tu
 
Kwangu nikiwasha gari inawaka taa ya coolant ya kijani na kuzima dakika nne au tano ninapokuwa kwenye mwendo, na hapo haiwaki tena mpaka nitakapo washa gari tena.
 
Kwangu nikiwasha gari inawaka taa ya coolant ya kijani na kuzima dakika nne au tano ninapokuwa kwenye mwendo, na hapo haiwaki tena mpaka nitakapo washa gari tena.
Taa ya kijanj au bluu ni taarifa tu.
 
Back
Top Bottom