KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya Mikopo inayojiita Credit Land imenifanyia udhalilishaji

KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya Mikopo inayojiita Credit Land imenifanyia udhalilishaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna huyu kaniweka mimi kama mdhamini, sasa wajomba toka juzi wananitumia sms ninachokifanya ni kumfowadia jamaa, halafu yeye anakataa kata kata na credential zake ni hizo zote.
 
Attachments

  • Screenshot_20240407-201507.png
    Screenshot_20240407-201507.png
    121.3 KB · Views: 20
Hivi hili swala mbona hazipiti siku mbili watu mnakuja kulia humu achaneni na mikopo hiyo mkope haya mshikaji sio unakopa kopa tu.Pia wabongo kulipa maden bibwagum sana acha mzalilishwe akili iwakae sawa
 
Mimi ukinidhalilisha hivyo ujue ndio tumemalizana hapo, hutopata hata senti yangu tena. Sasa utapima mwenyewe faida na hasara za maamuzi yako ya hovyo.
 
Mkuu laki mbili tu ndio unaleta malalamiko huku?
Ulipokua unakopa ulituomba ushauri?
Hebu lipa halafu utuletee changamoto ulizopitia.
Walah ukishalipa halafu wakaendelea kukubughudhi tutawapeleka mbele.
Kukopa harusi kulipa ......,
 
Hivi ulipokopa lengo lako lilikua kula Bata Sana halafu usamehewe Deni?
It does not work like that.
 
Wewe kaza tu, usipokee simu zao kabisa. Ukifanikiwa kuvumilia vitisho vyao tu, tayari umetoboa. Pesa za Mama hizo
 
Mnapo allow zle permission jitahidi unachagua "While using the app" hii itapunguza uwezekano wa wao ku access simu yako kama hujafungua app.
 
nenda ofisini kwao kawalipe lakini na wewe kusanya ushahidi wa defamation mtafute peter kibatala kama utaweza kumlipa
yani wao tu hujawalipa ndo utaweza kumlipa kibatala mbona kama najitesa kutoa ushauri
lakini navyokuona utawaweza kwa njia moja tafuta uchawi waloge sababu ukienda kwa mganga wa kienyeji hutaweza kumlipa
Umetoa solution na madongo juu😆😆😆🙌
 
Mimi ninadhani upambane tu ulipe maana hakuna namna. Wabongo wengi hadi wanazitupa line zao baada ya kukopa songesha na mikopo mingine ya mitandaoni. Yaani tabia za kipuuzi mno za kutotaka kulipa mikopo. Pia jitahidi sana kuishi na watu vizuri. Kudhalilika kisa 240k inatia sana mashaka kuhusu mahusiano yako na watu. Au wewe ni wale wanaosema mwaka huu ana-cut fake friends wakati yeye mwenyewe ndo fake friend?
 
Hao watu unatakiwa uwa face sio hujifiche.
Wakituma message unawajibu wakitaka ujue upo wapi unawaambia. Kama wanahisi wanatapeliwa basi kwanini wasiripoti polisi?

Haimaanishi ukidaiwa basi udharirishwe?
Wangapi wana mikopo na taasisi mbalimbali na wameshindwa kuilipa kwa wakati? Wangekuwa wanafanyiwa hivyo kama wewe si mjini yangejaa mabango na mitandaoni zingejaa jumbe za madeni ya watu na taasisi walizokopa...
 
Hujifiche ❌ ujifiche✔️, udharirishwe ❌ udhalilishwe✔️
 
Hizo zilikuwepo sana US ila sasa zimepigwa marufuku, ulikuwa unakopa dola 100$ wahuni wanataka title ya gari, na kwa njaa zako utawapa tuu, ukija kushtukia deni limefika 500$ 🤣 🤣 , wanajua ukienda kwao uko desperate au hujui shark loans, target ya mikopo hii ni watu maskini na Elimu duni, regulations ni muhimu la sivyo itaumiza wengi
 
Back
Top Bottom