KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Unafanyeje Mkuu?
 
watoto wakishua hamuwezi kuelewa huu mtiti kuna wengine kwenye circle zetu sisi ndio wenye nafuu
Sina maana kwamba mimi ni bora sana mkuu ila kwenye mazingira ya uhitaji kuna umuhimu wa kuwa na watu wawili au watatu mnapaswa muwe mna-share shida ndogo ndogo.

Sizungumzii shida za laki+ hapana ni hizi hizi za 20K 10K so kwa situation ya jamaa hapa angekuwa na hao watu akawagusa wawili au wote asingeikosa hiyo 40K.

Nisieleweke vibaya tafadhali.
 
shida si mikopo shida ni sheria, kuruhusu access ya contacts haimaanishi umeruhusu wazitumie unless kuna kipengele kimesema hivyo. kunauliza allow .... to access contacts nikajibu yes, haimaanishi nmekuruhusu uzitumie pia
Sasa usilipe ndani ya siku hizo ulizopewa halafu uone Moto unavyowaka utakavyotangazika mpaka makaburini
 
mmi binafsi phone book yangu ina majina zaid ya buku ila nikiwa na changamoto nikiwakosa watu watatu maana yake nimekwisha
 
Kampuni zote unazozijua wewe zinazokopesha hela ni lazma utangazike
Ni vile watanzania tunaogopa kwenda mahakamani ndio maana wachache wanaoenda wanaishia kuvuna mahela kama akina AY na tigo.... Hicho kitu wanachofanya hakiwezi kuwa sawa kabisa.
Note, si kwamba nasema watu wasilipe, ukikopa lazima ulipe na watanzania hatupendi kulipa.
 
Yajayo yanafurahisha zaidi 🤣🤣🤣
 
Aisee, hao waduanzi kwani wangapi wanakopa. Ningekuwa mimi nisingewalipa maana wameshatumia silaha yao ya mwisho.

Alafu haina haja ya wewe kujisikia vibaya kwani sms katumiwa mtu mmoja mmoja kwahiyo kila mtu ataielewa kwa anavyo kufahamu ni rahisi kumjibu kuwa hao ni matapeli
 
Hiki ndo nilichowafanyia PESA X mbwa wale, nimepita na 80000 yao, na kunishika hawawezi, shenzi kabisa yani mtu ukikaa tu siku tatu bila kuwalipa wanaaza usumbufu wa kingese.

Mpaka waje kudevelop hizo applications zao tutakuwa tumewaliza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…