Taarifa kutoka TRA kuhusu kubadilisha umiliki wa chombo cha moto

Kazi yao ni kukaza ili raia aumie. Ila sio kutazama changamoto ya sheria zilizopo ambazo zinafanya raia waone kodi ni mzigo na kuzikwepa.

Tatizo hapa sio raia kukwepa kufuata taratibu za kisheria bali tatizo ni hizo taratibu za kisheria zinabinya masilahi ya raia na kumnyima haki zake.

Pumbavu sana.
 
Naomba niseme tu mnaoona hili zoezi n baya acheni upumbavu na uvivu wa kufikiri, kila kitu kulalamika tu.

Kwaiyo mnataka muuziane kinyemela tu mtaani huko na wewe unayenunua unamiliki Mali kinyume na taratibu unaona fresh tu akati kiuharisia wewe sio mmiliki halali kwa sababu hujafata taratibu.

Kama mmiliki kafariki si kuna vielelezo kama mtu kafariki? Acheni kujifanya mnataka maendeleo akati bado mna akili za kizamani kila siku mtaona maendeleo ni kero kwenu.

Waafrika tulivyo wajinga tunaamini mtu asiyefata utaratibu halali na akafanikisha jambo lake uyo ndo mjanja sasa na kila mtu atamsifia. Ujanja ni kufata taratibu
 
Mambo mengine huleta ugumu wa maisha tu bila sababu. Let's agree that there are issues can work better in Europe or America but not in Africa, at least in some decades to come. Otherwise watajikuta wanakosa hata hicho kidogo.
Tatizo msisitizo wao ni nini, kuwa watu wafuate taratibu na sheria au kuwafanyia raia extortion kupitia mfumo wa sheria za kikanjanja......?!
 
Magari yanalipiwa yaingiapo inchini.sasa Kama mmiliki wa kwanza anamuuzia mtu Kodi ya Nini tena?,wakati gari ilisha lipiwa?.Au TRA Wana anzisha double taxiation?aghhhhhhh!!!!!
TRA thinking tank yao ni zero. Ubunifu hakuna kabisa.....
 
Na mahari watataka wapate percentage yao......
 
Wewe nae basi kuwa na uelewa. Unadhani kwamba wanaopinga hawapendi kufuata sheria?!

Tatizo hizi taratibu zinakuwa na makando makando ya upigaji ndani yake. Mamlaka zinakuwa zinabana sana raia kuwa huru na maisha kulingana mifumo ya kiuchumi ilivyo kwa sasa ambapo hela zinatoka sana kuliko zinavyoingia.
 
Haiwezekani na itafeli maana si kila mwenye gari anaendesha yeye. Kuna magari ya mizigo, daladala, tax, magari ya kukodi, kuazima. Usumbufu utakuwa mkubwa. Kila siku itakuwa watu wanaitwa polisi kuthibitisha umiliki.
 
Mnapoweka conditions wekeni pia options in case condition A haiwezekani basi X itakubalika, kwa mfano mmiliki yupo hoi hospitali, anauza gari lake ili atibiwe, je atafikaje TRA?
 
Unaelewa kubadili umiliki maana yake ni nini? Au umeendika ugolo wako kisa una ITEL na upo kwa kochi la shemeji yako? Kabla hujaandika kitu kwenye hoja za msingi anza kwanza kujiuliza maswali muhimu. Ujuaji kama huu ndio unafanya tuwe nyuma kimaendelo. Ngoja nikupe maelezo, unapobadili umiliki wa chombo utahitaji
1. TIN ya mmiliki wa chombo kitu ambacho ni rahisi tu kupata ambapo kwenye kadi ya gari inaonekana wazi kabisa.
2. passport ya mmiliki ambapo nayo ni rahisi kupata kupitia TIN yake.
3. barua ya kuomba kubadili umiliki nayo ni rahisi maana hakuna uthibitisho kuwa huo ndio mwandiko wa mmiliki halali.
4. Mkataba wa mauziano baina ya mnunuzi na mnunuaji, hapa pia ni rahisi maana unajiandikia tu unapitisha kwa wakili/mwanasheria.
5. Hati ya kiapo cha Umiliki wa chombo ambayo utaipata kwa mwanasheria/mahakamani ambayo nako wala hawajui kama ww ndio mmiliki hivyo ni rahisi sana kufoji.
6. Kadi OG ya chombo cha moto ambayo pia unaiweza ipata ikiwa gari imeibiwa na mwenye gari alikuwa anatunza hiyo kadi ndani ya gari.
NB haikuwa lazima mmiliki afike ofisini na hapo ndipo inafanya iwe rahis hata gari ya wizi iweze badilika umiliki.
Hivyo basi MABORESHO HAYA YATALETA UFANISI NA KUPUNGUZA WIZI, LKN PIA ITAMPUNGUZIA GHARAMA MMILIKI MPYA kuhangaika na TRA. YANAPOTOKEA MABORESHO TUWE POSITIVITY KATIKA KUHOJI NA KUCHAMBUA BADALA YA KUJIFANYA TUNA AKILI ZAIDI YA WATU WENYE UZOEFU NA HIZO IDARA MIAKA NA MIAKA.
 
SIKU UKIUZA GARI NA ULIYEMUUZIA AKAENDA KUFANYA TUKIO LA UJAMBAZI, AU KUBEBA WAHAMIAJI HARAMU AKATELEKEZA GARI NDIO UTAJUA UMUHIMU WA KUBADILI UMILIKI WA GARI MAPEMA SANA. MARA NYINGI HATUJUI KAZI ZA WAL TUNAOWAUZIA.
 
mmiliki awepo na mnunuzi awepo, kuna tatizo. mtu kanunua gari kwenye mnada uliohusisha magari yaliyo kamatwa kwa wadaiwa sugu, wamiliki utawapata wapi?
 
Hivi Wamefanya risechi ya Kutosha kweli? Na Kama Leo Ardhi Wamesitisha Kutoa hati za makaratasi eti wanatoa hati za Electronic ambazo Toka Mwezi Wa 3 hakuna hati iliyotoka
mambo mengi Tanzania ni mwendo wa zimamoto, hakuna maandalizi, wala utafiti.
 
Niliuziwa gari na mzungu 2013 alisharudi kwao. Nampataje Leo hii 2021?
Muda wote huo ulikuwa hujabadirisha umiliki?
Mimi cha kwanza kabisa ni kubadirisha umiliki ,ili niwe na uhakika na mali yangu hapo hata barabarani unatembea kwa kujiamini
 
Mlolongo mrefu sana aisee ,mara police,mara viapo,mara hati , yaani ni mwendo wa tozo tu ndani ya nchi ya TOZONIA
 
Naona TRA wametoa ufafanuzi namna ya kubadili umiliki wa vyombo vya moto du kumbe unaweza baadaye shindwa liuza kama ulinunu bila libadili jina au jamaa akakupiga famba

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…