Taarifa kutoka TRA kuhusu kubadilisha umiliki wa chombo cha moto

Taarifa kutoka TRA kuhusu kubadilisha umiliki wa chombo cha moto

Wakuu Someni Hii Taarifa Kutoka Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA)View attachment 1968871

=====

October 8, 2021 by Global Publishers

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi ya watu wanakuwa wamesajili vyombo vya moto lakini usajili wao ni batili, hawajasajiliwa na TRA ambapo magari yao yanakuwa yameliingiza nchini kimagendo, jambo linalopelekea magari zaidi ya moja yote yanakuwa na namba moja ya gari.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Oktoba 8, 2021 na Mercy Macha ambaye ni Afisa Msimamizi wa Kodi TRA wakati akitolea ufafanuzi katika kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio huku akiwahimiza wananchi kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo kubadili umiliki wa vyombo vya moto ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kuwakumba.

“Jukumu la TRA sio kukusanya kodi tu, hata kuelimisha pia. Kabla hujanunua gari lazima au chombo chochote cha moto, fika TRA ujue kama chombo hicho ni cha halali, hakidaiwi kodi, fuata taratibu wa kubadilisha umiliki kuja kwako.

“TRA tumekuja na utaratibu mpya, unapokuja kubadilisha umiliki wa chombo lazima mmiliki wa mwanzo awepo, mmiliki mpya (aliyeuziwa) awepo na atuonyeshe kitambulisho chake, chombo lazima kiwepo maofisa wetu wakikague kuanzia Chassis Number. Unapobadilisha umiliki wa chombo lazima zile kodi za uhamishaji wa chombo zichukuliwe, TRA tukusanye mapato.

“Gharama ya kuhamisha umiliki wa chombo cha moto ni Tsh 100,000 jumlisha asilimia 1 ya gharama ya ununuzi iliyoandikwa kwenye kwenye mkataba, na huu mkataba lazima uwe legal, usainiwe na mwanasheria na aweke risiti ya huduma aliyotoa.

“Kuna wanaopewa bajaji za mkataba, anaendesha akimaliza mkataba anakabidhiwa inakuwa ya kwake lakini hawaji kubadilisha umiliki, hawa nao tunawahimiza kuja TRA kubadilisha umiliki wa vyombo vyao.

“Kwa magari ambayo yameingizwa nchini yakiwa na msamaha wa kodi, wakati yanauzwa kuna utaratibu wa kufuatwa kuhakikisha msamaha hauhami kwenda kwa mtu mwingine, mhusika arudi TRA kufuata taratibu hizo. Usiuze chombo chako cha moto bila kuhakikisha umebadilisha umiliki, unayenunua hakikisha nawe unakuwa mmiliki halali wa chombo chako,” Mercy Macha, Afisa Msimamizi wa Kodi TRA.
View attachment 1969147
View attachment 1969149

Kwani kila umiliki unapobadilika huwa lazima mali iwe imeuzwa?

Zawadi, takrima, bakshish ni kwa vigogo tu?

Mzee Mwinyi kapewa lake 500m+ kutoka mifukoni mwetu. Yeye kodi haimhusu.

Sisi wengine tukiwapa au kupewa hiyo ni batili?

Harufu ya ubaguzi ule ule ambao katiba mpya ni muhimu ikauangazia.
 
Juzi nimemgumia demu anataka kuniandikia ile kaingiza T722 paaap!

Nikamshika bega,,, wewe unafanya nini hapo hebu usiniingize bana mie naondoka sasa hivi nimekuja kufanya delivery ya mzigo mda si mrefu! Huyo nikaingia ndani ya chombo na kusepa.

Kwa style ile unaweza kuandikiwa charges hata ukiwa umepaki bar bila wewe kujua aisee!
Hiv kuna menu ya kuingia kwa cm ya mkononi ili kuchek kama una deni la tochi?
 
Hahaa!
Ngoja nikamfufue baba angu aje tubadilishe umiliki wa haka ka gari ka urithi alikoniachia...
Happy birth day dad. Six years now since you departed from planet Earth to be reborn in the kingdom of Heaven!
 
Nahisi tu! Kama yupo mbali aje, kama amefariki unapeleka cheti cha kifo.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Hati ya kifo, hati ya chanjo ya Corona.

Si wote katika jamii hii wanazihitaji hati hizo hata kama chanjo wamechanjwa au kufa hata kama wamefiwa.

Mengine haya ni kutafutana uchawi tu.
 
Hence: watu hawatauziana na tra Watakosa mapato

Hawa majamaa wamesomea wapi!?

Udsm ndio inaleta majitu kama haya au degree za chupli chupli?

Yaani jitu linaongea kiurahisi tu halijali yaani
UDSM imekufanya nini? una 'lnferiority Complex'
 
Sasa Kama Mmiliki Wa Awali Yuko Mbali au amefariki Ts means Hawawezi Kufanya Transfer?
Yaani serikali inaweka masharti magumu sana ya kufanya uhamisho wa vyombo vya moto. Hii ya face to face itafeli sana, kama muuzaji yuko Pemba na anayetumia gari yuko Mpanda, inamaana Mpemba analazimika kusafiri hadi Katavi kwenda kuonekana TRA na kuhakiisha umiliki na uhamisho unakamilika. Sasa hapa TRA wanakaribisha rushwa, maana taratibu za uhamisho zitapindishwa na magari yataendelea kuhamishwa na watumishi na pesa itaingia mifukoni mwao badala ya kuingia kwenye mfuko mkuu wa serikali.
 
Huu utaratibu ni kuongeza usumbufu tu.
Hao ma afisa wa TRA wenyewe watakagua wanao huo muda?
Kama kuwainua tu kwenye kiti wanadai hela.
 
Back
Top Bottom