Ndugu wakazi wa Wilaya ya Kigamboni;
Ninapenda kuwajulisha kuwa kuanzia Jumapili tarehe 9 mwezi wa nane,2020 hadi Jummane tarehe 11 Mwezi wa 8,2020 kutafanyika shughuli ya ukusanyaji wa taarifa na maoni ya wananchi wakazi wa wilaya ya Kigamboni Juu ya matamanio yao maoni, na matarajioi yao kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.
Zoezi hili litahusisha kata zote za wilaya ya Kigamboni na linalenga kuwafikia wakazi wapatao 4000 kwa ajili ya kukusanya maoni yao juu ya maeneo ambayo wangependa yapewe kipaumbele na uongozi utakaochaguliwa na matarajio yao kwa miaka mitano ijayo
Maoni yote na ushauri wa mambo ambayo ungependa yawe kipaumbele katika uchaguzi huu yatapokelewa kwa njia ya Email:
mbungekigamboni20@gmail.com. au kwa kuzungumza na wakusanya taarifa ambao watapita katika maeneo mbalimbali katika wilaya yetu kupata taarifa za wananchi.
Kumbuka zoezi hili ni muhimu katika katika maendele.
Zoezi halina uhusiano na chama chochote cha siasa wala taasisi yoyote bali ni jitihada za Wana Kigamboni katika kutaka kuweka malengo ya pamoja kwa miaka mitano na kujua vipaumbele katika kila kata
Zoezi hili ni muhimu kwani litasaidia kuwawezesha wanakigamboni kushiriki katika kupanga sera na mipango ya maendeleo kwa kata zao na mitaa yao.Ripoti kamili ya zoezi hili itatolewa Ijumaa Tarehe 21 August 2020
Maoni yatumwe kwenda kwa
EMAIL.mbungekigamboni20@gmail.com
Kumbuka kutaja mtaa ulipo katika kutoa maoni yako ili kusaidia katika ufuatiliaji.
Asanteni Sana kwa ushiriki wenu.
Taarifa Imetolewa,
Gwakisa M.J
Mdau wa Maendeleo Wilaya ya Kigamboni
RATIBA YA SHUGHULI HII ITAKUWA KAMA IFUATAVYO
Jumapili -9Aug 2020 Wataalamu wetu watakuwa katika kata za Vijibweni,Tungi,Kigamboni na Mjimwema-Iwapo Ungependa kuzungumza nao tafadhali wasiliana nasi kwa email ili tukufikie ila unaweza kutuma maoni yako pia kwa njia ya EMAIL
Jumatatu tarehe 10 Augu 2020 tutakuwa katika Kata za Kibada,Kisarawe 2 na Baadhi ya maeneo ya kata Jirani
Jumanne Tutafika katika kata za Somangila,Kimbiji na Pemba Mnazi.
Iwapo unapenda kuzungumza nasi tafadhali wasiliana nasi kwa email ila unaweza kutuma maoni yako kwa njia ya email.
Nawatakieni Ushiriki mwema