Don Nalimison amelenga uchaguzi October, angeendelea na jina lake asingekuwa na kigezo cha kugombea nafasi yoyote ya kisiasa hivyo ujaja wa Don Nalimison akaona kubadili jina ili asiwekee kikwazo/vikwazo na hata akiwekewa kikwazo aweze kupinga kisheria.
Hakimu : Mlalamikaji una ushahidi kuwa mlalamikiwa hana sifa za kugombea nafasi yoyote ya kichama ?
Mlalamikaji : ndio, ndugu Hakimu Don Nalimison alitumikia kifungo hivyo hana sifa.
Hakimu : Mlalamikiwa una chochote cha kuieleza hii Mahakama tukufu
Don : Ndio, Kipindi nasajiliwa kuingia kwenye gereza la Butimba waliniandikisha kwa jina gani ?
Mlalamikaji : Deogratius Kisandu
Don : Kwenye hii kesi imesajiliwa kwa jina lipi ?
Mlalamikaji : Don Nalimison
Don : Nenda ukamtafute Deogratius Kisandu, Don Nalimison hajawahi kutiwa hatiani na Mahakama yoyote ndani hata nje ya nchi.
Hakimu : Kesi imehairishwa hadi ushahidi wa kesi hii utakapokamilika, Mlalamikiwa ana sifa ya kugombea nafasi yoyote pasipo pingamizi.