Taarifa: Nimekwisha kula Kiapo (DEED POLI) na kwa msajili wa Viapo na Nyaraka (Mahakama ya Ardhi) kuanzia sasa nitakuwa naitwa DON NALIMISON

Taarifa: Nimekwisha kula Kiapo (DEED POLI) na kwa msajili wa Viapo na Nyaraka (Mahakama ya Ardhi) kuanzia sasa nitakuwa naitwa DON NALIMISON

Don Nalimison amelenga uchaguzi October, angeendelea na jina lake asingekuwa na kigezo cha kugombea nafasi yoyote ya kisiasa hivyo ujaja wa Don Nalimison akaona kubadili jina ili asiwekee kikwazo/vikwazo na hata akiwekewa kikwazo aweze kupinga kisheria.

Hakimu : Mlalamikaji una ushahidi kuwa mlalamikiwa hana sifa za kugombea nafasi yoyote ya kichama ?

Mlalamikaji : ndio, ndugu Hakimu Don Nalimison alitumikia kifungo hivyo hana sifa.

Hakimu : Mlalamikiwa una chochote cha kuieleza hii Mahakama tukufu

Don : Ndio, Kipindi nasajiliwa kuingia kwenye gereza la Butimba waliniandikisha kwa jina gani ?

Mlalamikaji : Deogratius Kisandu

Don : Kwenye hii kesi imesajiliwa kwa jina lipi ?

Mlalamikaji : Don Nalimison

Don : Nenda ukamtafute Deogratius Kisandu, Don Nalimison hajawahi kutiwa hatiani na Mahakama yoyote ndani hata nje ya nchi.

Hakimu : Kesi imehairishwa hadi ushahidi wa kesi hii utakapokamilika, Mlalamikiwa ana sifa ya kugombea nafasi yoyote pasipo pingamizi.


Hakuna kitu kama hicho, deed pool haiwezi kukuweka mbali na makosa yeyote uliyoyafanya nyuma vinginevyo tungekua tunafanya makosa na kubadilisha majina.
 
Mkuu Deogratius Nalimi Kisandu sipping uamuzi wako,lakini hili jina jipya limekaa ki-ujana zaidi/kisanii. Alafu bado vyeti vyako vya elimu vinatumia jina lako la zamani,huoni litakuletea shida huko mbeleni?


Haiwezi kumletea shida popote atakapotakiwa kuwasilisha vyeti vyake lazima aambatanishe na deed pool kuonyesha mabadiliko ya majina.
 
Kuna systems nyingi za Tanzania zinahitaji majina matatu, usije ukalazimika kupachika jina lingine kukamilisha hilo hivyo kuvuruga tena majina yako.
 
Mtemi kisandu jukwaa lilikumiss sana, karibu tena blaza tulimiss sana burudani yako...usipotee sana Don
 
Wewe tumia JF tu achana na Facebook na YouTube na Instagram hapa Jf utakuwa safe huwezi kudondokea police maana ukiandika matusi yanafutwa ..

Pia tupe namba za Familiya yako ili tukutafutie msaada wa matibabu ya akili. Ili usije kurudi jela.
Sory mkuu huyu ni aliekuwa akiitwa deo kisandu au?
Nimeogopa kumuuliza yeye moja kwa moja
 
Kuna gharama zinazohusiana na kuapa kwa maana ya kutengeneza hyo deed poll inategemea na anaesimamia kiapo lakini kwa ukienda kuapia mahakamani haziwezi kuzidi 10,000. Ukishamaliza unaenda kwa msajili wa nyaraka na deed poll yako ikishapitishwa unalipia 32000 . Kwa hyo haiwezi kuzidi 50000.
hv gharama ya kubadili jna n sh ngapi na n office zipi wanashughulika na hili zoez
 
Back
Top Bottom