Halikuwepo hilo Taifa, ila ilikuwepo Uzayuni ambao ilikuwa ni harakati la kutengeneza au kulirudisha Taifa la Israel ikiwa ni maandalizi ya kurudi kwa masihi wao wanaomsubiri kwa mujibu wa maandiko ya kitabu cha Talmud.
Uzayuni ulikuwepo na umeendelea kuwepo katika mataifa makubwa yaliyo na yanayotawala Ulimwengu. Ndio maana mataifa haya ni damudamu na Israel. Kupitia uchumi, usomi na mipango yao wao ndio wanayatawala haya mataifa na hata baadhi ya viongozi unakuta wana asili ya Uyahudi.
Lakini Uzauyuni au Zionism , wapo wayahudi wanaopinga harakati hizo. Kajiongeze ukasome aina za wayahudi itakusaidia pia kukua kwa nini wakina Netanyahu wanaonekana kama Wazungu (caucasians).
Pitia mchango wa myahudi mwingereza na zionist Rothschild katika uundwaji wa Taifa la Israel na influence yake katika siasa za Uingereza.
Mengi sana ya kujifunza, soma vitabu, soma makala, pitia habari huko mashirika makubwa BBC, CNN na n.k utajua hata kwanini kuna aina ya wayahudi walikuwa wamepata ruhusua maalum ya kutojiinga na jeshi lao la IDF wakisema ni kinyume na imani yao.
Katika kujiunza, jielemishe kutofautisha katika ya Zionism, Jew na Israelites.