Taarifa: waandamana kupinga ujio waBUSH

wasomi vyuo vikuu na walimu wao wameandamana nimeiskia kwenye BBC kwa kupinga ujio wa buSH VIPI wao tuwaiteje?

kuandamana na kupinga kile ambacho unahisi si sawa bila ya kuvunja sheria za nchi mie sioni kuwa ni tatizo.

wao wametumia haki yao ya kidemokrasia.


na kama kuna watu wanataka kuandamana kumpongeza buSH WAFANYE HIVYO NA NNATEGEMEA WATAFANYA SAWA


na wanaotaka kuandamana kuwapinga waislam kwa hili na wafate taratibu


hakuna mijadala mibaya ambayo daima hutufikisha pahala pagumu kuliko mijadala inayohusu dini.

tujitahidini mijadala kama hii kuidhibiti kabla madhara yake hayajawa makubwa.

maombi kwa maadmin mada kama hizi zikianzishwa tu ziwahini kudhidhibiti kabla ya watu kuanza kutukana imani za wengine. Maana mie nilivyokasirika huyo Tzpride angekuwa karibu ningemsweka mangumi au hata kumuwasha risasi na niitwe niitwavyo.


uungwana ni kuheshimu imani ya wengine na kama kuna hoja kujadiliana kwa hekima na busara
 
Bwana Kikwete kanyaga mafuta twende . Nimepata tetesi muda mfupi kwamba next visitor to Tanzania is his Hollines Pope Benedict .Ponda and the co get ready maana naye aliwahi kustema cheche watu wakaandamana Duniani he shortly he will flying to Tanzania kwa safari ya Kiserikali na kichungaji .
 
Wasomi UDSM wapinga ujio wa Rais Bush wa Marekani
Na Kizitto Noya

UMOJA wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), kwa kushirikiano na taasisi mbalimbali za kijamii na za Kutetea Haki za Binadamu, umepinga ziara ya Rais George Bush wa Marekani aliyewasili jana nchini.


Umoja huo ulieleza kutoridhika kwake na ziara ya rais huyo jana katika mdahalo wao ulioandaliwa kwa kushirikiana na wanaharakati hao kwenye Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.


Akisoma tamko la pamoja, Mwenyekiti wa UDASA, Datmas Nyaoro, alisema Umoja wa Wanataaluma chuoni hapo unaamini kuwa kidemokrasia Tanzania haina jambo lolote jema la kujifunza kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa rais huyo wa Marekani.


"Hii inatokana na ukweli kwamba, chini ya utawala wa Rais Bush, haki za Wamarekani weusi zimeendelea kuvunjwa, idadi ya wafungwa kutoka katika jamii za Wamarekani weusi imeongezeka huku huduma za kijamii hasa afya na elimu zikidorora," alisema.


Kwa mujibu wa UDASA, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ufadhili kutoka nchi zinazotoa misaada yenye masharti kandamizi kama Marekani, hivyo mkataba wa dola za Marekani 608 milioni unaotarajiwa kusainiwa kati ya Rais Bush na Tanzania akiwa nchini, hauna maana yoyote zaidi ya kuendeleza ukandamizaji huo.


"Tunaamini pia katika kujitegemea na kujitawala wenyewe. Kuongezeka kwa kiwango cha misaada kutoka Marekani katika kipindi hiki ambacho uchumi wake umedhoofika na upinzani dhidi ya ubabe wake umeongezeka, kunatufanya tuamini kwamba ufadhili huu una agenda ya siri ambayo ni Africom," aliendelea kusema Nyaoro.


UDASA ilitoa wito kwa Watanzania kulinda misingi ya uhuru na utaifa, kulinda na kutetea utu, haki, usawa, amani na umoja wa Afrika badala ya kuendelea kuikumbatia Marekani na kupoteza misingi iliyojengwa tangu enzi za mababu.


Awali wakizungumza katika mdahalo huo, baadhi ya wanaharakati na wawakilishi wa taasisi za kijamii walisema kuwa ziara ya Rais Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania isipokuwa kwake binafsi na taifa lake la Marekani.


Kwa upande wake, Amiri wa Shura ya Maimam, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema ziara ya Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania zaidi ya taifa kujitengenezea maadui kwa kuunga mkono sera ya ugaidi.


Alisema sheria ya ugaidi nchini inapaswa kuangaliwa upya kwani inapingana na sheria za nchi na ndiyo inayosababisha mapigano katika mataifa mengi duniani.


Hussein Mmasi wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema Bush hana utaratibu wa kufanya ziara zenye manufaa kwa nchi wenyeji na kuwa ziara hii ni mwendelezo wa utaratibu huo wenye misingi ya kuzinyonya nchi maskini.


Profesa Azaveli Lwaitama, Mhadhiri wa UDSM, aliitaka serikali kuchagua marafiki wa kweli wanaoweza kutoa ushauri wa haki kuhusu maendeleo yake badala ya marafiki wanafiki kama taifa la Marekani.


Alisema Rais Bush amekuja nchini kwa kivuli cha misaada, lakini ukweli ni kwamba ana agenda kubwa yenye masilahi binafsi na taifa lake.


Ndani ya ukumbi kulikofanyika mdahalo huo kulikuwa na mabango kadhaa yaliyoelezea hisia za wanaharakati hao juu ya ziara ya kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani.


Baadhi ya mabango hayo yalisomeka 'Mfumo tulionao wa demokrasia wakilishi haufai, tunadai demokrasia shirikishi... Bush sitisha vita Iraq, Amani na Haki siyo vita'.
 

Mwanakijiji una matatizo makubwa sana mie sina dawa labda Mbowe anaweza kukutibu matatizo yako, napata shaka na wasi wasi kama kweli uko Marekani.

watu hawaichukii Marekani wanamchukia Bush kama mwenda wazimu ktk dunia hii, anayeshughulika na Ukimwi ni Bill Clinton kipenzi cha wamarekani na duniani kwa ujumla ana mfuko wake unaitwa Bill Clinton Aids Foundation, amekuja nchini na hakuna aliyemzomea bali alishangiliwa na watu wote kuwa ni mtu mwema amekuja kuona na kusaidia janga hili.

Clinton amefanya kazi kwa karibu sana na mzee Mandela kwenye suala la Ukimwi south Africa.

ungekuwa unatumia akili kidogo tu ungepata jibu.nchi zinazoongoza kwa janga la UKIMWI ni south Africa, Botswana, Zimbabwe,Lesotho,Zambia, Namibia, kenya n.k katika msafara wake bwana bush hakuna hata nchi moja ya hizo atapita, umeona hali ya South Africa ilivyo?

jana kama umefuatilia wakati anapanda ndege wachambuzi wote wa Marekani sio Jenerali Ulimwengu walisema anakwenda Africa sababu kuna cold war baina ya Marekani na China kugombea Africa na rasilimali zake, na lingine base ya kijeshi. hakuna aliyesema kuwa kuna barabara au Ukimwi.

Bush si mtu wa huruma aje kuona wagonjwa wa Ukimwi kwetu wakati mafuriko ya Harricune yalipotokea Marekani mwana jana hakuenda kuwaona raia wake sababu ni watu weusi ndio wanaishi eneo lile, misaada ikatoka nchi za kiarabu kuwasiadia wamarekani aibu kubwa, wengi walikufa na kupoteza maisha yao vipi leo awe na huruma na sisi? wakati hana huruma na raia wake wala wanajeshi wake wanaokufa bila sababu ya msingi.

Mwanakjj huwezi kumbeza Jenerali Ulimwengu kisa tu hoja yako ikubalike, Jenerali ni maneno mengine usifananishe kijalida chenu cha Tanzania Daima na kazi za Ulimwengu unatia aibu sana,

any way asiyekujua hakuthamini wewe utamjulia wapi Ulimwengu?
www.raiamwema.co.tz

wewe unajitia uko Marekani naomba uulize Maracois ni nani? au tembelea website ya Jennifer Diaz.

huyu bwana alikuwa anaishi Chicago siku Bush alipovamia Iraq yeye na wenzake zaidi ya elfu kumi waliandamana kupinga uvamizi wa mabavu.hatimaye watu mia tano wakawekwa ndani.

baada ya Mwaka mmoja wa kuvamia Iraq wakandaa maandamano makubwa zaidi ya kumpinga bush akakamatwa na wenzake na kuwekwa Ndani. hivi karibuni ameamua kujiua kutokana na kilio chake kutosikilizwa na Bush.

huyu si muislam ila ni mtu muadilifu.sasa kama kwao watu wamejiua unashangaa nini watu kuandamana Tz? na waliondamana si waislam ila ni wapenda haki na amani.

Inapotokea muislam akahoji kama alivyohoji Professor Kighoma Malima tenda mbovu ya MV BUKOBA anaandamwa na kuambiwa mdini.

nyinyi mmejua kuhoji juzi, Malima na waislam toka mia ya 70.na hata kina bibi Titti Mohamed walihoji mengi na kuambiwa wachochezi na kutiwa ndani.

nakuuliza wewe niambie japo kwa fununu tu Malima amekufa ana mali gani? Magufuri angekuwa muislam na akauza nyumba zile alizouza humu ndani ingekuwa kelele tu kinyume chake anapigiwa chapuo humu kuwa anavaa uwaziri aliteleza mara moja wazungu wanasema ONCE A CHEAT, ALWAYS CHEAT. mnasema kapuya hafai kafanya nini baya? jibu hamna ni udini tu.

unauliza nchi za UAE hazifanya kitu jee chuo kikuu cha Dodoma kitakachokuchukua watu elfu arobain 2009 anajenga PAPA BENEDICT? ni mtoto wa mfalme wa Saudia na wanasoma watu wa dini zote na wakristu ndio wengi hakuna anayelalamika.

KUWAIT imejenga daraja la Rufiji ambalo limebatizwa kuwa la MKAPA huku aliyeomba msaada ni mzee Ruksa cha ajabu hata siku ufunguzi hakualikwa.

leo hii uwanja wa Taifa mnapinga usiitwe JK kisa alyeomba pesa MKAPA.

Mwanakijiji muulize Museveni ananufaika vipi na Middle East baada ya kujiunga na OIC? waulize Msumbiji, tungepata mengi lakini udini umetutawala,mmezuia OIC halafu mnauliza mbona misaada mingi haitoki Middle East? kaulize kilimo cha mpunga bonde la RUFIJI. hivi sasa Aljeria inatoka scholarships mia moja kila mwaka za udaktari kwa serikali yetu.

Chuma.

huyu bwana asikumbue ni Mkatoliki namba moja hana hoja toka aanze kutuma vimakala uchwara kwenye gazeti la Chadema anajiona amekuwa Mwandishi na kuwakebehi magwiji wa fani kama Jenerali Ulimwengu.

kisa alinyimwa nafasi ya kupeleka upuuzi wake kwenye Raiamwema gazeti makni bwana Mwanakjjj hoja za Ulimwengu hata bosi wako makengeza hawezi kujibu.

Mwisho.

Wakoloni walipovamia Africa kuna watu waliwapinga na kupigana nao kama chifu Mkwawa-(Muislam, Abushir,Kinjekitile-muislam lakini wengine wakawakebehi na kuwaona wajinga hawa wazee.

baadaye ndio wakajua athari za mkoloni. kuna watu walipewa gololi na wazungu kuchukua dhahabu kwa kipindi kile hawalaumiwi kwa wakati ule, lakini leo hii Mwanakijiji na expose yako ya nje unashindwa kujua Bush anafuata nini? unadanganywa na mradi wa Malaria ambapo kwa miaka nenda rudi waJapan wanatusaidia? Elimu yetu hatusaidii kujua vision ya Africa. mwambie BUSH ameona waCHINA wamejenga viwanja vinne vya mpira Ghana kabla ya mazungumzo.
 
Uislam wameleta Waarabu na Ukiristo wamelata wazungu- yet leo Waafrika tunagombana wenyewe kwa wenyewe na dini walioleta wageni!
 
MH.
Hatugombani najaribu kumpa somo jamaa yangu Mwanakijiji.
ameshindwa kujua kuwa Marekani hana line nzuri middle East ya mafuta kwani anagomvi sehemu Nyingi. sehemu pekee ya kuyawinda mafuta ni Africa.

DRC ilikuwa nchi iliyotulia Wamarekani walipotaka Dhahabu wakaanzisha vita ili mikataba itoke kwa wafaransa wachukuwe wao. wakamuweka Kabila.
 
kama kuna marafiki wa kweli kwetu baina ya waarabu na wazungu bila ya kuficha nitakwambia ni waarabu.

wao wametusaidia sana tena bila ya masharti.


kule kwetu zanzibar tuliutanua uwanja wa ndege kwa fedhwa za mwarabu.

tumekarabati mahospitali na mashule yetu kwa fedhwa za waarabu.

mabara bara hata stop light za barabarani tumeletewa na waarabu.

ndugu zetu ktk kuhakikisha kuwa tuna vyuo vikuu walitusaidia sana zanzibar sasa ina vyuo vikuu vitatu

zanzibar colledge, zanzibar university tunguu na SUZA na karibu vyote ndugu zetu hawa wametusaidia.

lami na mengine wametusaidia ndugu zetu wa libya mafuta iran na wako njiani kutujengea chuo kikuu.

wataalamu wengi wa zanzibar wamesomeshwa na waarabu kuliko hata ulaya.


kwa hio mkjj waarabu wametusaidia tena bila ya kuunyonya uchumi wetu.

sijasikia kama unazo hadithi za hawa ndugu zetu kutunyonya kiuchumi


na nimesahau BARAZA LETU la Wakilishi linatarajiwa kuhama kutoka Mnazimmoja na kuelekea mbweni ambapo kunjengwa Baraza jengine na waarabu.

kuhusu misaada ya kijamii ndio usiseme ni visima vinggi vimechimbwa kuwasaidia wananchi na mayatima kusaidiwa kielimu, kifedha, kimavazi na mengineo.


kuwa fair mkjj usisukumwe na matashi yako
 
Mie nakwenda kusaka kwenye web wamerekani na watu wengine ambao si wa happa Tanzania wanasemaje kuhusu ujio wa kichaka Tanzania na Afrika. Nikizipata habari ntakuja zibandika hapa, naomba na wengine wasaidie tujuwe the other side wanasemaje?
 
Mie nakwenda kusaka kwenye web wamerekani na watu wengine ambao si wa happa Tanzania wanasemaje kuhusu ujio wa kichaka Tanzania na Afrika. Nikizipata habari ntakuja zibandika hapa, naomba na wengine wasaidie tujuwe the other side wanasemaje?

Kama nilivyoahidi hapo juu, naanza na hii, zingine zitafata:


Bush Africa visit seen more about strategy
By Barry Moody
Reuters
Friday, February 15, 2008
DAR ES SALAAM: President George W. Bush's coming African tour will emphasise the caring side of U.S. policy but it is widely seen as being more about military interests, oil supplies and combating Chinese influence.
Bush is scheduled to start a tour of five nations with a brief stop in Benin on Saturday, although he has threatened to delay the trip because of a legislative battle with Congress.
The five countries -- Tanzania, Ghana, Liberia and Rwanda, as well as Benin -- have been chosen for what are viewed as strong democratic credentials and successful U.S. aid projects.
The centrepiece and longest stop of the tour will be Tanzania, whose leader, President Jakaya Kikwete, is seen by Washington as a poster boy for progressive African government.
Bush, accompanied by his wife Laura, will visit hospitals, schools, AIDS and malaria projects. In Tanzania he will sign the biggest ever grant, of $698 million, under his Millenium Challenge Corp, to fund water, energy and infrastructure.
The MCC is intended to reward good governance and sound economic policies.
Kikwete named a new cabinet this week after the previous prime minister resigned over a corruption probe but Washington sees this as confirmation of the president's anti-graft credentials rather than an embarrassment.
Bush's attempt to anoint some of his more successful policies in Africa in the dying months of his presidency risks being derailed by cynicism over U.S. motives and the same issues, led by Iraq, that have made him unpopular elsewhere.
About 2,000 Muslims marched peacefully through Dar es Salaam on Friday to protest against Bush and his war on terror.
One of the march organisers, Sheikh Mussa Kundecha, told Reuters: "Bush will be here for his own benefit instead of caring about the people of the country."
Student Emmanuel Dickson said earlier: "America and Bush have one policy, to look after their own interests. If he is going to give us money for infrastructure and health ... what does he want in return? He wants to bring forces to Africa and he wants to stop the Chinese from getting a greater hold."
Beijing is now Africa's third biggest trading partner, behind the European Union and the United States, after a huge 30 percent jump in the first 10 months of 2007.
AFRICOM
Analysts say confused U.S. policy on Africa and bad handling of its new Africa command (Africom), particularly premature discussion of basing it on the continent, have alienated regional powers like South Africa and made Washington unpopular.
Bush approved Africom, a new command for Africa to offer both training to African armies and humanitarian work, a year ago. But African opposition has forced it for the moment to shelve plans to base the headquarters on the continent.
Africom has added to Africa's unhappiness over other elements of Bush's post 9/11 campaign against Islamist militants.
U.S. backing for the Ethiopian invasion of Somalia a year ago to prop up a weak transitional government against Islamist insurgents and the subsequent "rendition" of Muslim suspects, including Kenyan nationals, to Ethiopia has caused widespread anger.
Patrick Smith of the Africa Confidential newsletter said U.S. policy "appears to be at sea ... what is the foundation of the policy? Is it a security nexus based on militarisation or is it a much more development-oriented policy?"
"There is a sense that Africa has got the fag end of the war on terror and that it has been very badly handled and if anything has diminished the U.S.'s standing in the region with no great benefit in terms of military effect."
There is also a widely held belief around the continent that Bush is trying to counteract growing Asian, especially Chinese, influence and investment and that Washington is only really interested in oil resources in the Gulf of Guinea -- expected to provide 25 percent of its needs by 2015.
"What is on top of Bush's mind is the Chinese. China is worrying to the U.S. It is not only taking markets and alternative trade partnerships ...African countries will no longer need American aid to survive," said Ugandan student Joseph Mwaka.
Houcine Akkari, a retired man in Tunis told Reuters: "The U.S. says it wants to help Africa to boost democracy, reduce poverty and improve governance. But the truth is so different. Bush wants to exploit Africa which is rich in natural resources, without giving anything to Africa." (Additional reporting by Wangui Kanina, Francis Kwera in Kampala, and Sonia Ounissi in Tunis)
 
Mtalii umempa ujiko mkubwa Mkjj kuwa ni Bishop...Bishop wanakuwa na Elimu ya DINI yao, Huyu Mwanakjj hana elimu ya U-bishop..kafundishwa chuki...Ila Muombee AONGOKE aione Haki.

Mtalii Kwa nondo ulizoweka...labda avae miwani ya Mbao...inatosha kuhitimisha Mjadala huu.
 

Kweli kabisa kwa postings zake nilizoziona na mada zake anazoshindwa kuzitetea, mnhhh, sijuwi hata elimu yake ni ipi, au ndio wasomi wa Tanzania? waliofundwa na nyerere?
 
Nadhani rais J.Kikwete alipata fununu za maandamano na akamtuma Sheikh wa BAKWATA kuwaonya waandamaji. Sheikh Simba alitoa taarifa yake kuhusu habari hizi na kuwaambia kwamba USA inasaidia miradi mingi Tanzania na waislaamu pia ndio wanaofadhilika na misaada hii.Kwa hiyo wamkaribishe President Bush kwa ukarimu mkubwa kwani amealikwa na rais Kikwete.
Sisi watanzania kwa ujumla hatuna milahizi za kishenzi za kuchoma bendera za mataifa mengine. Lazima itakuwa ni hao waaarabu ndio waliowatuma kufanya hivi.

Tungojee ujumbe wao ni nini? Kama hiyo miradi ya kuenga babarara ambayo President Bush anatia sign hawaitaki basi watuambie. Kama hiyo barabara ya kutoka Horohoro mpakani wa Kenya mpaka Tanga haitaki itakuwa ni ajabu sana. Rais J.Kikwete aliahidi katika pirika pirika za uchaguzi kwamba atafanya juhudi hiyo barabara itengenezwe.

Wasituvurugie hawa!
 


Wape wape eeeh vidonge vyao, wakimeza wakitema ni shauri yao!
 

Moja kubwa walilotuleteya waarabu ni "ustaarabu", hii mijitu mingine isiyojuwa ustaarabu ni nini haielewi hilo.
 
Islam is crap, I wonder why you guys are wasting your time discussing about bombers! JF wanna be bombed now..I'm quiting...

F U do not ever abuse Islam! who are you? come out in the open and say that and see what I'll do to you, again F U.
 

Sawa kabisa ni la kidini, kwa sababu uIslam unatufundisha kutetea haki za wanyonge na wenye kudhulumiwa. Jee, wewe dini yako inakufundisha nini? Au anayoyafanya bush Iraq wewe unaona ni sawa?
 

Sijuwi dini ki-kwenu maana yake ni nini, lakini nakuomba ujuwe kuwa dini ni neno la kiswahili linalotokan ana neno la kiarabu "Din"na maana yake ni mfumo wa maisha. Kama uIslam ni dini, basi ndiyo mfumo wa maisha wa waIslam wote na si vinginevyo. Upo hapo ulipo?

Jee, ki-kwenu dini maana yake ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…