Zanzibar 2020 Taarifa ya ACT Wazalendo yasema watu watatu wamefariki kwa kupigwa risasi na Polisi huku tisa wakijeruhiwa Zanzibar

Zanzibar 2020 Taarifa ya ACT Wazalendo yasema watu watatu wamefariki kwa kupigwa risasi na Polisi huku tisa wakijeruhiwa Zanzibar

Kama tumeandikiwa kufa tukipambana na mkoloni Mweusi na iwe hivyo!

Walio tangulia wapumzike kwa amani nasi tuko nyuma yao.
 
Ndo waweke masanduku ya kura feki!?
Mtaji wa wanasiasa ni ujinga wa wafuasi wao. Huko Pemba hai waliojeruhiwa ukipata mmoja anajua kusoma na kuandika una bahati. Hai wanafanya kila wanachoambiwa na Maalim hata Kama hakina ukweli wowote. Jiulize Maalim alikuwa wapi akaona makaratasi yamewekewa kura Hadi akaenda kuwaambia wafuasi wayachukue kwa nguvu toka kwa polisi kwa kuwapiga na mawe?
Acheni kupotosha watoto.
 
Hao watoto wa miaka13 na 16 usiku walikuwa wanafanya Nini ktk vituo vya kura mpaka kujeruhiwa kwa risasi
 
Acha ujinga wewe Sasa hao ambao hata kura hawapigi unawaingizaje barabarani watoto?
Maalim achukuliwe hatua kwa alichokifanya.
Ndio maana mnaonekana punguani. Unajibu bila kuchunguza, kisa mahaba kukujaa tuu.
Screenshot_20201027-055224.jpg
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa ya yanayoendelea Pemba, taarifa hiyo imeandaliwa na Maalim Seif na kutolewa kwa Umma

=======
Taarifa zilizothibitishwa kutoka Pemba zinasema wananchi watatu wameuawa kwa silaha za moto na Jeshi la Polisi kuelekea mwanzo wa upigaji kura siku ya kesho, wengine tisa wamejeruhiwa.

Usiku huu Jeshi limekuwa likigawa masanduku ya kupigia kura kwenye vituo kwa ajili ya upigaji kura wa awali. Wananchi wanaozunguka maeneo hayo wamedai kwamba masunduku hayo tayari yana kura zenye alama. Wananchi hao walizuia masunduku hayo kwenda kwenye vituo vya kupigia kura, polisi walianza kurusha mabumu ya machozi kwenye jaribio la kutawanya mkusanyiko. Baada ya kushindikana, wakatumia silaha za moto. Bahati mbaya, imepelekea vifo vya Wazanzibari watatu na tisa kujeruhiwa.

Waliofariki katika kijiji cha Kangani
  1. Asha Haji Hassan(33)
  2. Yussuf Shaame Muhiddin(27)
  3. Kombo Hamad Salum(30)
Waliojeruhiwa kwa sialaha za moto
  1. Abbas Haji Nyange(27)
  2. Bakari Khamis Bakari(50)
  3. Mukhtar Yahya Hassan(16)
  4. Khamis Mohammed Mmanga(40)
  5. Hassan Kombo Ali(13)
  6. Abbas Mgau(22)
  7. Mgau Omar Mgau(35)
  8. Hamad Omar Hamad(20)
  9. Ali Hamad Seif(16)
Kulingana na vyanzo eneo hilo, imekuwa kuwachukua waliojeruhiwa kwenda hospitali kutoka Kangani kwa sababu barabara zote kuelekea Chake Chake, Vitongoji na Wete zinasimamiwa na vyombo vya usalama.


View attachment 1613146

View attachment 1613147
Sijawahi kuwaamini ACT wazalendo, kwani ni wa kukurupuka.
 
Ngoja akatusemee kwa
Lissu aseme neno.
amstedamuu.....HV kweli unazuia askari mwenye silaha. na mawe unategemea nn...mnashindwa sahau jeshi duniani kwote limepewa ruhusa kujilinda......
 
Back
Top Bottom