Taarifa ya ajali: Mwana JF mwenzetu Ushimen kapata ajali mbaya na sasa yuko Muhimbili hospital

Taarifa ya ajali: Mwana JF mwenzetu Ushimen kapata ajali mbaya na sasa yuko Muhimbili hospital

Wakuu.

Nimepata wasaa wa kupita MNH jioni hii na nimefika alipo ndugu yetu Ushimen

Kwanza sikuwa namfahamu kwa sura/hatukuwahi kuonana ana kwa ana. Yeye pia hivyo kama mimi.

Mwaka 2020 nilibadilishana naye contact hapa hapa JF tukaweza kuwasiliana nje ya hapa, since then, sikuwahi kupoteza namba yake.

Pamoja na kutaniana humu kama kawaida yetu ila nje ya JF haikuwa haba pia kwa mawasiliano.

Leo hii nimefika kumuona kwa mara ya kwanza na yeye kuniona kwa mara ya kwanza, cha kusikitisha yeye akiwa kitandani, ni mipango ya Muumba wetu.

Nimefurahi na yeye kafurahi pia kuonana naye hasa akiwa kwenye hali yake hii.

Kama Mshana Jr alivyoeleza hapo kwenye uzi, jamaa kaumia sehemu za bega(kwa ndani, hamna mchubuko kwa nje), Pafu( hapa ndio ilipo shida kubwa kwani liliathirika na kutiririsha damu na kujaa) ambapo kwa sasa kawekewa mpira wa kutoa hiyo Damu na maji maji.

Kwenye kuwezesha hayo maji yatoke analazimika kupush kwa kupuliza Pulizo(yaani anakaza/bana mbavu) ili mapafu yabane na kufanya maji yasukumwe yatoke kupitia mpira uliounganishwa. Tumuombee.

Wale ambao mtaweza na kupenda kwenda kumjulia hali, yupo Sewahaji 17, room/kitanda 12.
Mbarikiwe sana wapendwa 🙏
 
Back
Top Bottom