Taarifa ya ajali ya Tanga vifo 17 naiona Aljazeera, TV za bongo zinaonesha miziki tu

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Posts
2,507
Reaction score
2,412
Nimeikuta ALJAZEERA wanaionyesha muda wote kwenye kimstari kinachopita chini, scrolling ticker. Yani wameipa umuhimu.

nikaenda kutafuta details kwenye TV za bongo, zote zinaonyesha vipindi vya miziki...

Ndio aina ya media ambayo inaruhusiwa. Serikali kwa makusudi inalea taifa la watu wasio na taarifa wala mijadala muhimu, kwa hiyo hatuwezi kutafuta majawabu ya matatizo yetu, deaf dumb and blind. Kwa ajili hiyo tunaendelea kufa.
 
Hata ajali ya ndege ya Precision ilikuwa ni hivyo hivyo.

Watu walilalamika lakini hakuna cha maana cha kujifunza kwa matukio.

Hii ndiyo Tz yetu.

Pole sana kwa wote waliofikwa na dhahama hii pamoja na ndugu na marafiki zao wote pia, Mungu awarehemu.
 
Najiuliza huyo dereva wa fuso angesubiri dakika moja tu ku overtake,

Angeokoa maisha ya watu 17,
Ifike tu muda madereva wakisababisha ajali,mbali na kunyanganywa leseni,na magari yao yachukuliwe na hata kutaifishwa kabisa, maana huku barabarani kuna muda unaona kitu ambacho dereva anafanya,unaona kabisa kakusudia na siyo bahati mbaya, dereva wa gari kubwa anaona magari madogo yote ni takataka mbele yake,anaweza kufanya chochote, dereva wa gari dogo,ana muona bodaboda ni kama kumbikumbi,anaendesha anavyotaka, bodaboda na yeye ni kama vile fahamu huwa zinamtoka saa akiendesha, kuna haja ya hatua kali kabisa kuchukuliwa,faini za hali ya juu ziwepo,uzembe utapungua.
 
Wangeamua kulivalia njuga ajali zingepungua sana
 
Nimeikuta ALJAZEERA wanaionyesha muda wote kwenye kimstari kinachopita chini, scrolling ticker. Yani wameipa umuhimu.

nikaenda kutafuta details kwenye TV za bongo, zote zinaonyesha vipindi vya miziki...

Ndio aina ya media ambayo inaruhusiwa. Serikali kwa makusudi inalea taifa la watu wasio na taarifa wala mijadala muhimu, kwa hiyo hatuwezi kutafuta majawabu ya matatizo yetu, deaf dumb and blind. Kwa ajili hiyo tunaendelea kufa.
Waziri wa mambo ya ndani ana ramba asali tu wala ashtushwi na vifo vya ndugu zetu

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ajali ya precision = yale yale

Ajali ya MV Spice islander = yale yale tena TBC walieka Taarabu mwanzo mwisho.

Muda huu 2:17 PM star tv wanaona bora waweke mkutano wa sherehe za CCM, wanaona bora washerehekee msiba aisee.. kweli kufa kufaana. Sasa hao waliokufa hawakuwa wanachama wa CCM? aisee.
 
Gari ya msiba ndio ili overtake

Wakiokufa 14 ni Ukoo mmoja wa Mrema

Watoto wa Marehemu wamekufa, Watoto wa Kaka yake, Mashemeji zake na wengine

Waliibiwa pesa zote na vitu vyao

Wanaomba msaada wakazike Uchagani

Mmoja wa wahusika wa Msiba akiongea na waandishi wa Habari
 
Back
Top Bottom