Ifike tu muda madereva wakisababisha ajali,mbali na kunyanganywa leseni,na magari yao yachukuliwe na hata kutaifishwa kabisa, maana huku barabarani kuna muda unaona kitu ambacho dereva anafanya,unaona kabisa kakusudia na siyo bahati mbaya, dereva wa gari kubwa anaona magari madogo yote ni takataka mbele yake,anaweza kufanya chochote, dereva wa gari dogo,ana muona bodaboda ni kama kumbikumbi,anaendesha anavyotaka, bodaboda na yeye ni kama vile fahamu huwa zinamtoka saa akiendesha, kuna haja ya hatua kali kabisa kuchukuliwa,faini za hali ya juu ziwepo,uzembe utapungua.