Taarifa ya bunge: Kuhusu wabunge wa CHADEMA walioko nje

Taarifa ya bunge: Kuhusu wabunge wa CHADEMA walioko nje

Kwani lazima waingie bungeni,waachwe tu huko walipo kama ni adhabu tutawapa sisi saaa ya kuwapigia kura.
 
Mbona jina la mheshimiwa Mnyika silioni?
au yeye ameisharudi bungeni?
 
Kufanya kazi kwa kutekeleza maagizo ya muhimili mwingine kunaondoa fahamu za kujitambua kuwa wewe nawe ni kiongozi wa muhimili ambapo kiongozi wa muhimili mwingine anatakiwa aufyate kwako anaposogea kwenye anga zako.
 
Spika wa Bunge ameagiza kitengo cha usalama cha Bunge kutowaruhusu wabunge 15 wa CHADEMA kuingia katika maeneo ya Bunge kuanzia leo 13 Mei 2020 mpaka pale watakaporudisha posho ya kujikimu ya kuanzia tarehe 1-17 Mei 2020 waliyolipwa na Bunge. Pia wabunge hao wametakiwa kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya virusi vya Corona.


1589377488357.png

1589377461899.png
 
Kuna aina ya maneno ukiyasoma toka mwanzo kurudi nyuma huleta maana fulani ya kificho ama huwa ni yenye ukakasi kwa namna fulani, kwa mfano neno "live" ukilisoma hivyo huwa "evil" Hili sasa la "ndugai" husomeka kama "iagudn" ama wengine wangeweza kulisoma kama "igandu".

Kwa kauli zake tata za hivi karibuni na uvunjaji wa wazi wa katiba na kanuni za bunge, labda ndiyo kusema kati ya hayo maneno mawili, moja ama yote husadifu kauli na matendo ya kiongozi asijielewa na mwenye kupelekeshwa na mhimili uliojichimbia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amevizia wakati wamemaliza muda wao waliojiwekea ndio anatoa tamko, ili ionekane wamemtii
 
Eti leo Ndugai analazimisha wabunge wa Chedema kurejea Bungeni.

Si ndiyo alikuwa anawafukuza bungeni na vikamati vyake uchwara.
 
Eti leo Ndugai analazimisha wabunge wa Chedema kurejea Bungeni.

Si ndiyo alikuwa anawafukuza bungeni na vikamati vyake uchwara.
Mambo si yanaenda yakirudi mkuu, shati bovu la jana leo linaweza kuwa tambara la deki jipya.
 
Back
Top Bottom