Taarifa ya kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya mikoa Nchini

Taarifa ya kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya mikoa Nchini

Ushaona watu ambao hatujivunii kabisa nchi yetu??? Ndo sisi sasa Watanzania sometimes mtu una-wish ni heri ungezaliwa nchi za Somalia uamue moja kuwa unashika mtutu au ufe kikondoo.... written from bottom of my heart nachukia ufanyaji kazi wa viongozi wetu.

Uende somalia ukaungane nao masaa machache yaliyopita wametangaziwa ushindi na Naibu Rais wa Kenya kwamba hazina ni mufilisi.
 
Lisu anashangilia na kufurahi sana huko chumbani kwa Amsterdam
Haya matusi unayomtukana Lissu kila mara yanakusaidia nini?

Ni siasa tu zinakufanya kumtukana mtu mzima kama Lissu matusi makubwa hivi?

Katika maisha yako ulishawahi kumwona baba yako mzazi yuko na mwanamme chumbani,?
Lissu ana familia, ndugu, na marafiki wanakwazika na matusi yako, kama ambavyo ungekwazika ukitukaniwa wazazi wako,
 
Haya matusi unayomtukana Lissu kila mara yanakusaidia nini?

Ni siasa tu zinakufanya kumtukana mtu mzima kama Lissu matusi makubwa hivi?

Katika maisha yako ulishawahi kumwona baba yako mzazi yuko na mwanamme chumbani,?
Lissu ana familia, ndugu, na marafiki wanakwazika na matusi yako, kama ambavyo ungekwazika ukitukaniwa wazazi wako,
Alieneza chuki sana kwenye taifa letu
 
Alieneza chuki sana kwenye taifa letu
Chuki kama zipi? Ukiona anaeneza chuki, wewe hubiri amani.
Sio kumtukana matusi ya nguooni, na umekuwa na tabia hiyo kwa kutumia I'd tofauti,
Siasa zisitutoe utu, tunatofautiana lakini bado sisi ni binadamu tu,
 
Hizi hitilafu za kila siku zitaisha lini Tanzania hii?

Hii nchi kwenye suala la kusimamia nishati ya umeme wakiri tu kuwa WAMESHINDWA na wabinafsishe tu.
 
Tanesco waone aibu sasa, tatizo ni kina cha maji au hitilafu kwenye mitambo yao?

Hawa jamaa wanatuchezea sana siku hizi.
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kukosekana kwa huduma ya umeme kulikosababishwa na upungufu wa kina cha maji kwenye vyanzo vyetu vya Kihansi na Pangani pamoja na hitilafu iliyotokea kwenye vituo vya Kinyerezi I na Songas leo, Jumanne, Septemba 13, 2022.

Hitilafu hii imesababisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar Es Salaam, Morogoro, Singida, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Njombe, Ruvuma, Songwe, Iringa, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Geita, Mara, Manyara, na Simiyu kukosa huduma ya umeme.

Jitihada za kiufundi zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha hitilafu iliyojitokeza inatatuliwa haraka iwezekanavyo. Aidha, tutatoa taarifa mara huduma ya umeme itakaporejea.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

IMETOLEWA NA KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA, TANESCO MAKAO MAKUU.

SIMU
: +255 748 550 000

View attachment 2355492
TUTAKUKUMBUKA CHUMA JPM! #R.I.P CHUMA JPM#
 
Back
Top Bottom