Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa

Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hebu Isome mwenyewe halafu tueleweshe na sisi;

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi lingependa kujulisha kuwa, Disemba 1,2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es Salaam kuna mtu mmoja mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Landcruiser rangi nyeupe.

Ilielezwa na mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baaadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo.

Ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mara tu baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

Pia soma: Kuelekea 2025 - News Alert: - Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

1733049532296.png

Lakini Je Majibu ya ufuatiliaji wa Wengine waliotekwa akiwemo Soka na Bonge wa Kiluvya yako wapi?

Iko siku hata Msemaji wa Polisi aweza kutekwa na bado Jeshi la Polisi litaendelea kusema tunafuatilia
 
Hebu Isome mwenyewe halafu tueleweshe na sisi

View attachment 3166514

Lakini Je Majibu ya ufuatiliaji wa Wengine waliotekwa akiwemo Soka na Bonge wa Kiluvya yako wapi?

Iko siku hata Msemaji wa Polisi aweza kutekwa na bado Jeshi la Polisi litaendelea kusema tunafuatilia
Hapa ndio huwa sielewi vyama vya upinzani huwa vinapinga ñini?
Yaani mtu àmbae ni mwanachama wao anatekwa, anauawa, wao wanaenda kuhudhuria mazishi tuu.
RIP wagombea wa serikali za mitaa.
 
Kila nikikumbuka kuhusu yule kada wa CDM nabaki nacheka huku nikiumia
Yaani mwanzo walikanusha hawamshikirii baadaye wakakubali wanamshikiria Mwisho wakamwachia kwa faini ya Elfu 85
Je,ni nani huyo Mwenye land cruiser nyeupe anayeweza kumteka mtanzania mwenzetu tena katikati yetu akiwa na pingu ambazo ni nyara/Mali za serikali?
Kwanini viongozi wetu na Wanasiasa wetu kutoka chama tawala hawakemei masuala haya ya utekaji?
 
Hapa ndio huwa sielewi vyama vya upinzani huwa vinapinga ñini?
Yaani mtu àmbae ni mwanachama wao anatekwa, anauawa, wao wanaenda kuhudhuria mazishi tuu.
RIP wagombea wa serikali za mitaa.

Punguza ujinga. Ulitaka wafanye Nini? Wapindue serikali, mmeachiwa kila kitu ila bado hamridhiki. Very stupid idiot
 
Hebu Isome mwenyewe halafu tueleweshe na sisi

Lakini Je Majibu ya ufuatiliaji wa Wengine waliotekwa akiwemo Soka na Bonge wa Kiluvya yako wapi?

Iko siku hata Msemaji wa Polisi aweza kutekwa na bado Jeshi la Polisi litaendelea kusema tunafuatilia
Ajabu sana.
Mbona simu ya mmoja wa watekaji haiongelewi iko wapi?

Na kwenye taarifa iliyopo hapa JF namba za gari ziko tofauti na namba hizo zilizoandikwa kwenye taarifa hiyo!
 
Back
Top Bottom