Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa

Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa

Serikali haiwajui watekaji, Wananchi hawawajui watekaji mbaya zaidi Serikali inaonekana haina uwezo wa kupambana na hawa watekaji.

USHAURI: Serikali ianze kuruhusu raia sasa kumiliki na kutembea na silaha ili wajilinde na haya magenge, watu waruhusiwe bila milolongo Sasa kumiliki bunduki maximum mbili kwa kila mtu, Watanzania waruhusiwe kutembea na masime/mapanga/visu mitaani ili wajilinde na kutoa msaada kwa jeshi polisi kila waonapo raia mwenzao yupo matatizoni.
 
S
Nawakumbusha tena hii nchi ya kijamaa.
hatuna cha kufanya tumewapa mamlaka makubwa sana hawa watu. Usitegemee impact ya abuse of such power kua ndogo na kwa jinsi navyojua wanatanzania wenzangu tulivyo waoga acha tutawaliwe tu hivi hivi.
 
Hebu Isome mwenyewe halafu tueleweshe na sisi;

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi lingependa kujulisha kuwa, Disemba 1,2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es Salaam kuna mtu mmoja mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Landcruiser rangi nyeupe.

Ilielezwa na mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baaadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo.

Ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mara tu baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

Pia soma: Kuelekea 2025 - News Alert: - Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli



Lakini Je Majibu ya ufuatiliaji wa Wengine waliotekwa akiwemo Soka na Bonge wa Kiluvya yako wapi?

Iko siku hata Msemaji wa Polisi aweza kutekwa na bado Jeshi la Polisi litaendelea kusema tunafuatilia
Hii si amini kama ni tukio LA kweli, hii ni bongo muvi imetengenezwa kuwatoa wananchi kwenye issue ya wizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa na ccm, pili lengo hapa ni kutengeneza picha kwamba "jamaa ametekwa" Na watu wa chadema, maana imetajwa namba ya gari kuwa inamrikiwa na Deo Ninja(mchaga) kwa akili ndogo za wabongo, hii itausishwa na chadema,
ACT inatumiwa tu na ccm,
 
Aibu ya nini wakati mi-ananchi imekaa na inakenua menu kujadili Simba na Yanga? Tena hii ni vizuri ifanyike mara kwa mara pengine wananchi wataamka.
Kabisa kaka,tena wangeanza na watu wa familia yako ingekuwa poa sana maana naamini utakuwa kiongozi wa wananchi watakaoamka.
 
wAAYu9E.jpg
 
Back
Top Bottom