Taarifa ya Sheikh kutoa muda kwa aliyemuibia Simu infinix yake ya kisasa airejeshe vinginevyo!

Taarifa ya Sheikh kutoa muda kwa aliyemuibia Simu infinix yake ya kisasa airejeshe vinginevyo!

Wapi Simu...

Watu wanaina mpaka misikitini, Mahekaluni na Makanisani...., na wanapeta tu..., Hata kwenye hizo nyumba za ibada wamegundua cha kufanya ni kuweka mlinzi au kufunga milango na makufuri, ingekuwa raisi hivi wangeacha milango wazi
 
Mambo ya kawaida hayo, hatuna muda wa kwenda sijui polisi au Cyber crime, ambako tunajua usumbufu wake so hii ni clear and faster kupata mali yako.
Alafu mtu kama huyu anayedai simu yake iliyoibiwa kwa nguvu na mikwara yote, utakuta anatembea na mke wa mtu!!
Yaani hii dunia hii, Ufarisayo hautakwisha abadani!
 
Ha ha hao jamaa wahuni tu, kuna msikiti huku mtaan waliibiwa pikipiki basi wakawa wanapiga bit usiku wa manane eti piki piki irudi. Mpka leo kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna muhuni aliiba amplifier ya msikitini, sijui kilimkuta nini ila baada siku 3 asubuhi amplifier imetelekwezwa kwenye mlango wa msikiti halafu juu kuna kikaratasi cha kuomba radhi kimeandikwa "nisamehe mimi, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapo chini, Umeuaaaa
 
Back
Top Bottom