Taarifa ya ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule za kanisa katoliki Tanzania

Tujenge VETA nyingi zaidi na kujikita kwenye special education kuanzia primary hadi chuo. Kanisa halipaswi kuendelea kujikita kufanya mambo ambayo watu wengine wanaweza kuyafanya vizuri.
 
Kwa kweli umenena mkuu
 
Wale wa upande wa Munyazi Mungu wana cha kujifunza hapa!
 
Hawa wapuuzi wanatangaza biashara kwa upande moja na kuleta mgawanyiko kwa msingi wa dini
 
Toka lini Marian boys ikawa Morogoro na St.Aloysius ikawa Dsm?
Marian boys ipo Bagamoyo jimbo katoliki la Morogoro na st. Aloysius ipo kibaha jimbo Kuu katoliki Dar es salaam. kwa hiyo sista alikuwa anataja shule kutokana na majimbo katoliki zilipo hizo shule
 
Ngoja niwahii masifu ya asubuhii sasa!

Atukuzwe Baba mwana na Roho Mtakatifu kama mwanzo na sasa na siku zote milele Amina 🙏

Eh Mungu uliye nguvu yetu na makimbilio ya wanadamu

Kwa wema usikilize sala za watu wako wanaokulilia.... Amen
 
Ni wapi ulikabwa koo wakati wa ujenzi wa hizo shule? Nitajie na mfano hata wa shule moja tu uliyokabwa koo kwa michango wakati wa kujengwa kwake! Halafu unataka hizo shule zisitoze ada, halafu wale walimu mahiri watalipwa na nani mishahara mizuri ya kuwafanya wawe na ari ya kufundisha kwa bidii zaidi?

Kwenye dunia ya leo ya survival of the fittest, bado unawaza kupewa huduma za afya za bure kwenye hospitali za Kanisa! Na wale wahudumu nao watakuhudumia bure? Je, wewe hapo ulipo unafanya kazi bure pasipo na malipo?
 
Mbinu ya kibiashara.

B.T.W! hongereni Sana RC kwa kuchukua jukumu la NECTA na kulifanyia kazi ninyi kama ninyi kwa Shule zenu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…