macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Hivi ni Mawua au Maua seminary?Majimbo katoliki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ni Mawua au Maua seminary?Majimbo katoliki
MauaHivi ni Mawua au Maua seminary?
Tumsifu Yesu Kristo. Taarifa hii inatolewa na Idara ya Elimu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2024 kwa shule za Kanisa Katoliki.
Lengo la kutolewa kwa taarifa hii ni kutoa tathmini ya ufaulu wa shule hizo ili kubaini maendeleo ya kitaaluma, maeneo yanayohitaji maboresho, na mwelekeo wa jumla wa elimu katika taasisi hizo.
Kwa mujibu wa takwimu, jumla ya watahiniwa wote nchini Tanzania walikuwa 516,695. Kati yao, wanafunzi wa shule za Kanisa Katoliki walikuwa 19,182, sawa na asilimia 3.6 ya watahiniwa wote.
Kwa upande wa ufaulu, wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi la tatu walifikia 18,745, sawa na asilimia 97.72 ya watahiniwa wa shule za Kanisa. Wanafunzi waliopata daraja la nne walikuwa 128 (asilimia 2.23), huku waliopata daraja la sifuri wakiwa watu 9 tu, sawa na asilimia 0.04.
Ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2023, ufaulu wa shule za Kanisa umeendelea kuimarika. Mwaka huu, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 1.66, tofauti na ongezeko la asilimia 0.15 mwaka uliotangulia.
TAKWIMU ZA UFAULU KWA KILA DARAJA
Daraja la Kwanza: Wanafunzi 12,308 (64.16%)
Daraja la Pili: Wanafunzi 4,991 (26.01%)
Daraja la Tatu: Wanafunzi 1,146 (7.53%)
Daraja la Nne: Wanafunzi 128 (2.23%)
Daraja la Sifuri: Wanafunzi 9 (0.04%)
TAKWIMU ZA UFAULU KWA SHULE
Katika shule za Kanisa, jumla ya shule 65 zilipata ufaulu wa A, shule 160 ufaulu wa B, shule 47 ufaulu wa C, huku shule 2 zikipata ufaulu wa D. Hakuna shule hata moja iliyopata ufaulu wa E.
SHULE KUMI ZILIZOONGOZA KWA UFAULU
1. St. Francis Girls, Mbeya
2. Cardosa Girls, Dar es Salaam
3. Tengeru Boys, Arusha
4. Precious Blood Girls, Arusha
5. Bethel Girls, Mafinga
6. Mawua Seminary, Moshi
7. Anuarite Girls, Moshi
8. St. Mary's Mazinde Juu, Tanga
9. Marian Boys, Morogoro
10. St. Aloysius Girls, Dar es Salaam
PONGEZI NA MAPENDEKEZO
Tunaipongeza jamii nzima ya shule za Kanisa, ikiwemo walimu, viongozi wa shule, wafanyakazi, na wanafunzi kwa kazi kubwa iliyofanikisha matokeo haya. Pia, shukrani kwa wazazi ambao wamewajibika katika malezi na elimu ya watoto wao.
Tunawashukuru maaskofu kwa kusimamia shule hizi, kuhakikisha zinazingatia maadili ya Kanisa, na kuimarisha huduma za kiroho kwa wanafunzi. Huduma hizo zimechangia mafanikio haya makubwa.
Hadi kufikia mwaka 2025, lengo ni kupunguza kabisa wanafunzi wanaopata daraja la sifuri na kuboresha zaidi kiwango cha ufaulu. Idara ya Elimu inahimiza waalimu na wakuu wa shule kuendelea kuweka juhudi kubwa zaidi ili kuhakikisha elimu inayotolewa inaleta mabadiliko chanya kwa jamii.
Tunaendelea kuwaombea baraka za Mungu katika kutekeleza jukumu la elimu na malezi ya wanafunzi wetu.
View: https://youtu.be/BDXmTW0SIZ8
She gani ya kanisa warming wamechangishwa kujenga?Shule zimejengwa na waumini kwa kukabwa koo ya michango halafu ada inayowekwa waumini hawawezi kumudu kulipia watoto wao kwa shule waliyojenga wao wenyewe.
The same na hospitali, waumini wanachangishwa kujenga hospitali lakini wakiugua hawawezi kutibiwa bure kwenye hospitali walizojenga wenyewe. Huu ni wizi kama wizi mwingine kwa mgongo wa dini.
Dini ni utapeli kama utapeli mwingine Mungu hayupo.
Zaidi ya hayo shule nyingi za kanisa zinaendeshwa na mashirika mbalimbali,labda Seminary ndio waamini wanachangia huendeshaji wake tena sio kwa asilimia zoteWala sijawahi kusikia makubaliano yakifanyika kanisani kuwa tunajenga ili tusomeshe wanetu hivyo tuweke gharama ambazo ni affordable kwa kila mmoja.
Shule hizo zinatoa huduma bora na huduma bora zinahitaji gharama, zikiwekwa gharama za Kayumba matokeo yakawa ya Kayumba mtakuja hapa kushangilia.
Hivyo ni vitegauchumi vya kanisa ndio maana lipo imara, sasa ninyi endeleeni kusalia kwenye maturubai na shule za kuhesabu huku mkitoa malalamiko ambayo waumini wa RC hata hawayatoi.
Sahihi kabisa mkuuShe gani ya kanisa warming wamechangishwa kujenga?
Zaidi ya hayo shule nyingi za kanisa zinaendeshwa na mashirika mbalimbali,labda Seminary ndio waamini wanachangia huendeshaji wake tena sio kwa asilimia zote
Atakua msabato uyoKuna watu wakiona mambo ya RC hata yawe mazuri kiasi gani watatafuta namna ya kukosoa tu hata kama haieleweki
Hao wadau chuki yao dhidi ya RC ni ya viwango vya kipekee, sijui sababu yao huwa ni nini.Atakua msabato uyo
Na Sisi bakwata tutatoa data zetu za ufaulu Kwa shule zetu ndani ya wiki hii......
Wabillah tawfiq!!!!