Taarifa za habari kutoka kwenye media zetu zinaboa sana

Habari zao kubwa ni makongamano, warsha, ziara ya fulani, uzinduzi, fulani kawataka wakina fulani wafanye hivi. . . , zinachosha sana. Nadhani waandishi hupewa posho kwenda kurekodi hayo matukio hivyo wanaona kama wana deni la kuyarusha.
 
Yaani miaka nenda Rudi ukitazama ITV, TBC, ZBC, clouds, wasafi
Habari ni zile zile za matatizo.
1. Video
2. Watu kutekwa
3. Mafuriko.
4 Matatizo ya maji
5. Mlipuko wa magonjwa, kipindupindu, suala
6. Upungufu wadawa
7. Ugomvi wa wakulima na wafugaji
8. Ufisadi.
9. Ubakaji
10 Njaa n.k
11. Kukatika madaraja

Yani ukiwa Tanzania huwezi kuwasha TV ukatazama habari chanya za

1. Mambo ya technology
2. Mapinduzi katika kilimo
3. Biashara za Kimataifa
4. Tafiti mbalimbali
5. Masuala ya viwanda, kukuza uchumi n.k

Sasa hapa tutatokaje hapo
Shida aliziacha Nyerere hadi Leo zipo
"Black people are good for nothing apart from indulging in sex and having so many wives."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the apartheid era.
 
Nadhani Utv ambayo ni channel ya Azam Tv wanajitahidi wapo tofauti kidogo, kwenye siku 5 za wiki yaani Jumatatu hadi Ijumaa, kuna siku moja kwenye taarifa ya habari kuna segment ya makala ya kilimo, elimu, teknolojia, afya hizo zote huwa ni makala mpya kila wiki.

Kueleweka zaidi ni kwamba Jumatatu wanaweka makala ya elimu hiyo segment wao wanaita ufunguo, Jumanne wanaweka Kilimo ambapo wanaita shambani, jumatano wanaweka Teknolojia, alhamisi wanaweka Afya wanaita Siha yako, ikimbukwe kwamba hizo makala huwa zinaruka kwa kupishana siku japo naweza kua nimekosea kutaja siku ila huwa ndani ya Jumatatu hadi ijumaa.
Kwa Tanzania hii UTV ndo kituo chenye taarifa ya habari bora kabisa ukilinganisha na hao wengine, kinachonisikitisha nikuona jamii ya watu wengi huwa hawaielewi taarifa ya habari ya UTV, Unakuta watu wanaangalia taarifa ya habari kwenye mabanda yetu ya mpira, ikiwa UTV watapiga kelele kuwa toa hapo tupeleke ITV or Star TV, huwa nawashangaa sana ukizingatia nina kataaluma kangu ka Mass Com, hawa media kongwe wanapaswa kubadilika sana katika hizo taarifa zao za habari aiseee.
 
Hakika kabisa mkuu
 
Hapo kwenye watu kutoielewa Utv ni jambo hata mimi linanishangaza, mimi huu unaenda mwaka wa 6 kama sio wa 7 toka taarifa ya habari wanarusha Azam Two hadi baadae Utv naangalia Azam news pekee nikikuta inaangaliwa taarifa ya channel nyingine naondoka naendelea na shughuli nyingine.

Utv wapewe maua yao, quality ya picha HD, package ya habari waliyo nayo ni top, mtiririko wa habari zao, uchambuzi na sasa hivi wameongeza nusu saa ya uchanganuzi kwa sasa hawa ndio bora.
 
Azam wanajitahidi
 
Anzisha tv yako uwe unaangazia habari unazotaka...
Njoo na mapinduzi yako
 
Sio Tanzania tu ni AFRICA na katika Mabara yote kwa ujumla katika maeneo wanaoishi Wabantu hata South Africa penye Wabantu ndio kuna mlipuko wa magonjwa na watu kuuana

The same to Nigeria na USA, Lakini ukija kusini mwa jangwa la Sahara ndio kabisaa ni Uozo mtupu

Shida, Ujinga, Laana na Umasikini ni vitu vibaya sana

Unakaa mahali na Mgeni Spain, Sweden, Norway au German then mkiangalia Taarifa ya habari kila siku anakuuliza

"Why are you always live like this?"

Wanaona kama hatuwezi kujiongoza na hatupendani kabisa, Pia wanatuona hatuna Uzalendo na nchi yetu
 
Back
Top Bottom