Taarifa za Heche za Benki ya CRDB zaonyeshwa hadharani Mahakamani na Wakili wa Serikali bila idhini ya mwenye Akaunti

Taarifa za Heche za Benki ya CRDB zaonyeshwa hadharani Mahakamani na Wakili wa Serikali bila idhini ya mwenye Akaunti

Ni feki na huko Instagram, FB, X na mitandao mingine risiti mbili zinazagaa Moja ya ni ya ingizo la TZS 10,000,000/= na nyingine ni ya ingizo la TZS 20,000,000/=

Lakini za kule mitandaoni, waungwana walishathibutisha pasipo shaka kuwa ni feki, sio halisi..

Na kama ndizo ambazo Katuga kuzitumia mahakamani, basi iko shida mahali kwa Jamhuri

Na kuwa sasa ni wazi kabisa hii kesi imewalemea kiasi kwamba wako so desperate kutafuta hata milango isiyo rasmi kwa kuvunja sheria ili tu ku - justify kuwa bado wamo wamo..
We nae, yaani mwenye account mwenyewe hajakanusha kuwekewa mzigo na Salman, we nani ukatae!?
 
Binafsi nilitegemea Heche "alianzishe" pale pale mahakamani kwa kuhoji uhalali wa wakili kuwa na nyaraka ya bank inayomuhusu na hata kama wakili alipewa nyaraka hiyo na mtu aliye deposit pesa kwa akaunti ya Heche, ningekuwa mimi (hata kama mahakamani kuna mambo mengi) ningeshikilia pale pale kuwa "simjui huyo mtu na kama unataka kujua hiyo akaunti ni ya nani na aliweka hela za nini kamuulize hilo swali aliyekupa hiyo risiti". Kamwe nisingekubali kukubali huo upuuzi
 
Kuchunguza namba ya simu ya mtu inahitaji court order .

Walipoanza kumfuatilia Erick Kabendera wala hawakuchukua court order policcm walienda moja kwa moja Vodacom na kuwatumia vidampa wao wa pale wakapewa taarifa zote za mteja wao , ghafla Kabendera anaona SIM card zake zimefungiwa kupokea wala kutoa pesa na ghafla hawezi kupiga wala kupokea simu kumbe walishamuweka kwenye target akawa located akakamtwa.

Hawajaanza leo kuvunja sheria , Kabendera ana kesi na Vodacom na Lissu ana kesi na Tigo kwa sababu hizi hizi za kuvamia faragha.
 
Toa neno pumbavu jadili mada, hujawahi kusikia serikali imeshindwa kesi au hujawahi kusikia benki imemlipa mteja mabilioni ya pesa.
Siyo katika Mazingira ya kutoa ushirikiano kwa mamlaka za serikali fuatilia vizuri Polisi TAKUKURU TRA wanaomba bank statement za mtu yoyote
 
Kama ilikua Part of Evidence haina shida Mahakamani hakunaga Siri ni sehemu ambayo mambo huelezwa bayana Heche is notorious Criminal anasema 30m kwenye account yake hajui aliyeweka?😁

Kama Heche ni "criminal " hawa tuwaiteje chawa?

HRIbj__aEAAWDsl.jpg
 
Na Martin Maranja Masese

Taarifa za kibenki za mteja zina ulinzi mkali wa siri za wateja, kuzingatia kanuni ya Usiri wa Kibenki (Bank Secrecy and Confidentiality Principle). Nguzo kuu inayojenga uaminifu kati ya benki na wateja.

Kisheria, taarifa za kibenki za mteja zina ulinzi mkali wa siri za wateja unaotokana na mkataba kati ya mteja na benki, Sheria ya Taasisi za Benki na Fedha, na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa za Binafsi.

Benki inatakiwa kulinda taarifa za mteja isipokuwa katika mazingira manne pekee: (i) Compulsion of Law), (ii) Duty to the Public, (iii) Interests of the Bank, (iv) Consent of the Customer.

Wakati John Heche anatoa ushahidi wake katika kesi ya uhaini ya Jamhuri Vs. Tundu Lissu, Wakili Mkuu wa Serikali, Katuga ametoa nyaraka zake za ‘photocopy’ kuonyesha akaunti ya benki ya John Heche.

Nyaraka hizo za ‘photocopy’ zimetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali ili kuonyesha taarifa za miamala ya John Heche mbele ya Mahakama kutoka katika akaunti yake ya Benki Na. 01522005XXX.

Nyaraka za kibenki kama zikihitajika na Mahakama, zinatakiwa kuwasilishwa Mahakamani zikiwa unauthenticated au uthibitisho wa kisheria (Bankers’ Books Evidence Act/Certified Copies).

Soma Pia: Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Anyways, kama kuna kuvunja mkataba wa usiri wa mteja (Breach of Duty of Confidentiality), John Heche akimaliza kutoa ushahidi wake Mahakamani, ataona nini anatakiwa kufanya katika jambo hilo.
Taarifa yeyote ikihitajika mahakamani inatolewa,
elewa hilo
 
Siyo katika Mazingira ya kutoa ushirikiano kwa mamlaka za serikali fuatilia vizuri Polisi TAKUKURU TRA wanaomba bank statement za mtu yoyote
Itajulikana kesi ikifunguliwa unaweza kuta benki ikamkana Katunga ili isipoteze brand yake na uaminifu kwa wateja, serikali ikajitenga Katunga akabaki peke yake.
 
Kuna kitu watu hawajakiona...

Hiyo risiti ya muamala ni ya mwaka 2024, kabla Heche hajawa makamu mwenyekiti...

Katuga ameileta...anajua itatumika na CCM kumshambulia Heche kwamba anakula michango ya tone tone..

Kauliza gari Prado...Heche aliagiza November 2024, lakini swali linalenga kuonyesha amenunua mwaka huu baada ya michango..

Lengo la Katuga ni kuuliza vitu personal..ili watu wajue kwamba ana neemeka na michango

Watu hawajui Heche anafuga mifugo mingi..analima... Ana kampuni..
 
CRDB WATAMLIPA MABILIONI. Wala asiwachekee
Hawawezi kumlipia kwa sababu Hana ushahidi kama zimetolewa na Benk au nawakala,au mtu aliye ziingiza ma je ni Risiti halisi au copy. Mnivigumu sana kuwashitaki.sema kikubwa Bank inaweza kupoteza wateja kwa kuhisi kuwa Siri za account zao zinaweza kufikiwa kirahisi. Ila Huwa ni jambo la kawaida taasisi za serikali kukagua account za watu na kuchukua atua pale mtu anapoonekana amevunja Sheria za nchi na mara nyingi TRA Huwa wanafunga account za wafanya Biashara nakuchukua fedha zilizopo kwenye Account zako kama wanakudai hata bila kukutaarifu.unakwenda beki kutoa pesa unakuta wazee wakazi wamekomba pesa zote.
 
Back
Top Bottom