Taasisi ya Kidini ya Spirit Word Ministry yafutiwa usajili

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1685381986640.png

Wizara ya Mambo ya Ndani imesitisha usajili wa Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/24.

Masauni amesema katika kudhibiti na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imesitisha shughuli za Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

“Jumuiya hiyo imefutiwa usajili kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kutoa ujumbe wenye kuhafifisha jitihada za kupambana na vitendo vya ushoga nchini,”amesema.

Aidha, Masauni amesema taarifa zimekusanywa zinazohusu idadi ya vituo vya kulea watoto na shule zinazotoa mafundisho ya dini kwa watoto wadogo.

Amesema lengo ni kutambua idadi ya vituo au shule za bweni zinazotoa mafunzo yenye mwelekeo unaokinzana na maadili ya nchi yetu ikiwemo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ambapo katika mwaka 2023/24 wizara imepanga kuandaa mwongozo wa taratibu za kuabudu na ithibati ya taasisi zinazotoa elimu ya dini, kuimarisha ufuatiliaji na utendaji wa Jumuiya za Kidini na zisizokuwa za Kidini.

Pia katika mwaka huo watafanya ukaguzi na tathmini ya vihatarishi vya kiusalama kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Jumuiya yatakayochangia kudumisha amani na utulivu nchini.
 
Jamaa yuko deep vizuri sana kufundisha neno ila ana vitu kadhaa simuungi mkono...
Aliomba msamaha kwa serikali na wananchi kwa maneno kuhusu ushoga etc....kwanini serikali isingempa onyo kuliko kumfungia. Aliomba msamaha.

View attachment 2639633
Wizara ya Mambo ya Ndani imesitisha usajili wa Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/24.

Masauni amesema katika kudhibiti na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imesitisha shughuli za Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

“Jumuiya hiyo imefutiwa usajili kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kutoa ujumbe wenye kuhafifisha jitihada za kupambana na vitendo vya ushoga nchini,”amesema.

Aidha, Masauni amesema taarifa zimekusanywa zinazohusu idadi ya vituo vya kulea watoto na shule zinazotoa mafundisho ya dini kwa watoto wadogo.

Amesema lengo ni kutambua idadi ya vituo au shule za bweni zinazotoa mafunzo yenye mwelekeo unaokinzana na maadili ya nchi yetu ikiwemo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ambapo katika mwaka 2023/24 wizara imepanga kuandaa mwongozo wa taratibu za kuabudu na ithibati ya taasisi zinazotoa elimu ya dini, kuimarisha ufuatiliaji na utendaji wa Jumuiya za Kidini na zisizokuwa za Kidini.

Pia katika mwaka huo watafanya ukaguzi na tathmini ya vihatarishi vya kiusalama kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Jumuiya yatakayochangia kudumisha amani na utulivu nchini.
Yaani kwa ukubwa wa tatizo jinsi ulivyo nchini waziri anasimama kutangaza kusitisha usajiri wa kataasisi hako kamoja tu?
NIlitaraji tangazo lake la kwanza lingeondoka na taasisi na ministry kama 1,000 hivi.
Hapo ndiyo mtaamini hizo taasisi zina mkono wa serikali au zimeanzishwa na serikali yenyewe ili kuzififisha dini kwa kuingiza viongozi na ministry za kitapeli ambapo itafika mahali wananchi wattaona dini ni utapeli tu na kuacha kuzifuata.

Mpango huu ni mbinu ambayo CCP iliwapatia CCM waitumie ili kuua ushawishi wa dini nchini. Mbinu hii haikuishia hapo, wameipeleka mpaka mdani ya Lanisa Katoliki amnapo ili ku discourage waumini wame introduce michango mingi sana isiyo na kichwa wala miguu.
Hata hiyo taasisi iliyofungiwa unaweza kukuta ilikua ni project ya serikali ni vile wameona approach hii imekua too much ndiyo maana wameishia kuifuta tu bila kuwachukulia hatua yoyote na hata ufutaji wake umekuja kwa kuchelewa sana.
Mchawi mkubwa wa nchi hii ni CCM na Serikali yake.
 
View attachment 2639633
Wizara ya Mambo ya Ndani imesitisha usajili wa Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/24.

Masauni amesema katika kudhibiti na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imesitisha shughuli za Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

“Jumuiya hiyo imefutiwa usajili kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kutoa ujumbe wenye kuhafifisha jitihada za kupambana na vitendo vya ushoga nchini,”amesema.

Aidha, Masauni amesema taarifa zimekusanywa zinazohusu idadi ya vituo vya kulea watoto na shule zinazotoa mafundisho ya dini kwa watoto wadogo.

Amesema lengo ni kutambua idadi ya vituo au shule za bweni zinazotoa mafunzo yenye mwelekeo unaokinzana na maadili ya nchi yetu ikiwemo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ambapo katika mwaka 2023/24 wizara imepanga kuandaa mwongozo wa taratibu za kuabudu na ithibati ya taasisi zinazotoa elimu ya dini, kuimarisha ufuatiliaji na utendaji wa Jumuiya za Kidini na zisizokuwa za Kidini.

Pia katika mwaka huo watafanya ukaguzi na tathmini ya vihatarishi vya kiusalama kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Jumuiya yatakayochangia kudumisha amani na utulivu nchini.
Huyu nabii mwenyewe anaonekana ni shoga
 
Back
Top Bottom