KERO Taasisi ya OSHA rudisheni hela yangu, nililipia training, mkanipotezea hadi nimefukuzwa kazi

KERO Taasisi ya OSHA rudisheni hela yangu, nililipia training, mkanipotezea hadi nimefukuzwa kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu naipeleka kwenye Taasisi ya OSHA - inayoshughulikia usalama katika eneo la kazi, niliomba training tangu mwezi wa 10 Mwaka 2025 na nikalipa ada ya Sh 300,000 kwa ajili ya training.

Sasa imepita miezi 5 tangu niombe kusoma, wamekuwa na majibu mepesi kiasi kwamba hawaoni umuhimu wa hiyo training!

Bahati mbaya kazini niliomba ruhusa ya masoma nikapewa wiki mbili lakini sikuweza kurudi kutokana na sikuwa na vyeti ambavyo nilisema naenda kusoma hivyo nikafutwa kazi (jobless now).

Sasa ombi langu naomba wanirudishie ada yangu mimi jitajua naenda kuifanyia nini maana hata hiyo training haina maana tena!!

photo_2026-04-15_16-28-56.jpg

Malipo yamepokelewa kwenda OSHA
Ankara: 991510258106
Kiasi: 300000 TZS
Risiti: 925285374636986
2025-10-12T20:18:09
Kupitia: 199d96df3bb5cbee

Wamekuwa hawanipi ushirikiano wowote zaidi ya kunipa kalenda kila siku naogopa nisije fanya fujo ofisini kwao wakaniteka bure.
 
Samahani mkuu...
Hizi ni hasira za kufukuzwa kazi, ama hasira za kushindwa kurudi kazini na cheti, ama nihasira za OSHA kushindwa kuku train kile mlicho kubaliana ulipe, ama njaa imesha anza kukuuma..??
 
Sasa kwanini hukurudi kazini wakat jambo lilikuwa nje ya uwezo wako...
 
Osha ukishalipia hiyo Ada ya mafunzo, siku ya ratiba iliyopangwa nenda darasani. Kama mafunzo yamesogezwa mbele, basi wewe pamoja na wengine mtapewa taarifa. Kwahiyo kama wewe hujasoma, basi na wenzako mlioomba hayo mafunzo hawajasoma.

Tofauti na hapo, basi ni wewe hukwenda kusoma kwa makusudi. Ratiba ya mafunzo, ikijumuisha tarehe, muda, na darasa/mahali vyote hivyo unavijua kabla hujalipa ada.

Pia kama ni wewe hujasoma, basi ukienda kuwaambia, watakupa ratiba ijayo na hayo mafunzo, na utasoma bila shida.
 
Back
Top Bottom